Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Ikulu ya Marekani imeonesha wasiwasi wake baada ya shambulio dhidi ya huduma ya Exchange ya Microsoft ikitaka taasisi binafsi na za serikali zilizoathiriwa kuchukua hatua za haraka ili kuepusha madhara zaidi.
Katika ujumbe wake kwa waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki ametaja kitendo cha udukuzi kwenye seva za Microsoft kuwa shambulio la wazi, akisema mianya iliyoonekana katika seva hizo zilizotumiwa na wadukuzi inaweza kuwa na madhara zaidi.
Microsoft imeilaumu China kufadhili shambulio hilo la kidigitali ambalo limeathiri maelfu ya taasisi nchini Marekani, ikitaja "Hafnium" kuhusika. Shambulio hilo liliwekwa wazi siku ya Jumanne katika chapisho la blogu, huku ikiahidi kurekebisha mianya ya kiusalama iliyowaruhusu wadukuzi kupenyeza katika seva za huduma ya Exchange.
Shirika la Habari la Reuters limesema zaidi ya taasisi 20,000 zinaweza kuwa zimeathiriwa na shambulio hilo la mtandaoni, idadi hiyo ikiongezeka kwa nchi zingine duniani, ingawa baadhi ya wachambuzi wanasema idadi hiyo inaweza kufikia taasisi 30,000 nchini Marekani pekee.
Mshauri wa Usalama wa Ikulu ya Marekani amezitaka taasisi kuhakikisha zinachukua tahadhari kusasisha toleo jipya la kiwango cha usalama kwa vifaa vyao vya kidigitali baada ya shambulio hilo.
Hii ni mara ya nane ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo kampuni ya Microsoft imekiri kudukuliwa katika mashambulio yanayofadhiliwa na taifa. Ingawa "Hafnium" hufanya shughuli zake kutoka China, anadaiwa kutumia mtandao binafsi wa intaneti (VPN) wa Marekani, kwa mujibu wa Microsoft.
Chanzo: BBC