White House yataka taasisi kuchukua tahadhari baada ya Microsoft Exchange kudukuliwa

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
99
150
Ikulu ya Marekani imeonesha wasiwasi wake baada ya shambulio dhidi ya huduma ya Exchange ya Microsoft ikitaka taasisi binafsi na za serikali zilizoathiriwa kuchukua hatua za haraka ili kuepusha madhara zaidi.

Katika ujumbe wake kwa waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki ametaja kitendo cha udukuzi kwenye seva za Microsoft kuwa shambulio la wazi, akisema mianya iliyoonekana katika seva hizo zilizotumiwa na wadukuzi inaweza kuwa na madhara zaidi.

Microsoft imeilaumu China kufadhili shambulio hilo la kidigitali ambalo limeathiri maelfu ya taasisi nchini Marekani, ikitaja "Hafnium" kuhusika. Shambulio hilo liliwekwa wazi siku ya Jumanne katika chapisho la blogu, huku ikiahidi kurekebisha mianya ya kiusalama iliyowaruhusu wadukuzi kupenyeza katika seva za huduma ya Exchange.

Shirika la Habari la Reuters limesema zaidi ya taasisi 20,000 zinaweza kuwa zimeathiriwa na shambulio hilo la mtandaoni, idadi hiyo ikiongezeka kwa nchi zingine duniani, ingawa baadhi ya wachambuzi wanasema idadi hiyo inaweza kufikia taasisi 30,000 nchini Marekani pekee.

Mshauri wa Usalama wa Ikulu ya Marekani amezitaka taasisi kuhakikisha zinachukua tahadhari kusasisha toleo jipya la kiwango cha usalama kwa vifaa vyao vya kidigitali baada ya shambulio hilo.


Hii ni mara ya nane ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo kampuni ya Microsoft imekiri kudukuliwa katika mashambulio yanayofadhiliwa na taifa. Ingawa "Hafnium" hufanya shughuli zake kutoka China, anadaiwa kutumia mtandao binafsi wa intaneti (VPN) wa Marekani, kwa mujibu wa Microsoft.

Chanzo: BBC
 

Naby Keita

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,241
2,000
Nyie mnapenda vita za mabomu na mabunduki wenzenu wanawatandika kidigitali tu....
...
Mchina na mrusi wanamlia timing tu Mmarekani siku ajichanganye wamuonyeshe ni madude gani wanayafahamu baada ya udukuzi wao wa miaka mingi
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
10,112
2,000
Marekani waache kulialia maana wenyewe ni viranja wa kuwapeleleza wengine kwa njia ya kudukua
 

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
462
1,000
China inaweza kushambuliwa hadi ikaanguka, US atakuwa anasubiri China aingie kwenye kutegemea mtandao kisawasawa ili akipigwa shambulio moja tu asisimame tena.
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,736
2,000
Yaani wanakiri kabisa Kuwa wanadukuliwa na China wakati yeye Ni super power hawaoni aibu
 

Guasa Amboni

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
8,320
2,000
ni zamu kwa zamu,waliwadukua wengine,nao Sasa ni zamu yao kudukuliwa.
Waqt wazazi wetu walipogundua kuwa wanakaa na mijitu mijinga hapo nyumbani waliamua kutupeleka shule sasa huko tukakutana na matukio mengi mojawapo ni wezi wa penseli sasa panakuwa na mtu mbobezi wa fani hiyo sasa itokee aibiwe yeye siku hiyo atalalamika na kulialia siku nzima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom