Whichever way you look at: JK ni wa Kulaumiwa

sun wu

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
2,020
1,418
Vyovyote vile ukiangalia kutokuwajibika kwa Mawaziri na Nchi kwenda kama kipofu mlevi.., wa kulaumiwa ni mmoja tu.., nae ni mkuu wa nchi..

Kabla sijasema ni kwanini naomba nielezee kisa kimoja cha Sun Tzu (The Art of War) kilichotokea hapo zamani

Sun Tzu alimwambia Mfalme kwamba anaweza akambadilisha mtu yoyote na kuwa mwanacheshi.., basi mfalme akamwambia afundishe makahaba 180.., Sun Tzu akawatenga makahaba katika makundi mawili na kuchagua Officers wawili wawasimamie..,

Sun kwanza akawaambia hao Officers waangalia mbele (wenyewe wakaanza kucheka cheka..) Hapa Sun akasema labda makosa ni yake, sababu hakueleweka.., akarudia tena kuwa-command (wale makahaba wakaendelea kucheka cheka). Sun akaamuru hao Officers kuuliwa, baada ya mfalme kuja juu, Sun akasema Kama Kiongozi akitoa command asipoeleweka (basi ni makosa ya kiongozi) kama akieleweka na officers wasipofata basi ni makosa ya hao Officers. Baada ya hao viongozi kuuliwa, na wengine kuchaguliwa wale makahaba walifuata commands bila matatizo

Hivyo basi tutaona kwa vyovyote vile kama JK anatoa maelekezo, either haeleweki au kama anaeleweka na watu wake hawafuati.., basi hana meno ya kuwawajibisha au hataki kuwawajibisha...

Kwahio ili huku kucheka cheka.., na kuchekeana kuishe inabidi aanze kuonyesha kwamba yupo serious
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom