Where to invest in Africa: Tanzania yaondolewa kwenye 10 bora

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,924
3,072
Hii ni kulingana na ripoti ya Rand Merchant Bank iitwayo 'where to invest in Africa'. Ripoti imeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi zilizoshuka sana kwenye orodha yao ya sehemu bora za kuwekeza Afrika. Top 10 ya mwaka huu ni:
10. Tunisia
9. Ethiopia
8. Nigeria
7. Cote D'Ivore
6. Ghana
5. Rwanda
4. Kenya
3. South Africa
2. Morocco
1. Egypt
 
Rwanda sijui inaingiaje. Very limited natural resources, insufficient land, no/little skilled labor, no free judiciary, no democracy etc.

Labda element wanayoweza kujivunia ni hiyo ya kumbambana na rushwa na hali ya usalama iko vizuri kama vile hapa Bongo tu

Kama hakuna hila za mabeberu ilitakiwa na Tanzania iwepo, lakini South Afrika ni mabeberu na mtu na mjomba wake, so sishangai
 
Na huo uwekezaji wa Wachina na Wahindi wa kulipa watu wetu mishahara isiyokidhi mahitaji wala hauna faida kubwa sana kwa nchi

Zanzibar kwa mfano kuna uwekezaji mkubwa sana kwenye sekta ya mahoteli na utalii kwa ujumla unaofanywa na Wazungu hasa Wataliano lakini mchango wa sekta hiyo kwenye uchumi wa Zanzibar ni kidogo sana

Actually kuna arrangement zingine za safari za watalii zinafanyika huko nje ya nchi pamoja na malipp yote 100%, na mtalii anapoingia Zanzibar hatumii kabisa pesa mpaka anapoondoka. Sina hakika kama na serikali nayo inapata kodi stahili
 
Burundi yenyewe sijui hata kama hua ipo E/Africa, kwny kila Top 10 za maana haipo labda kwny Top 10 za Rushwa/maisha magumu/usalama duni/mazingira mabovu ya kufanyia biashara/watu kupotea

Uganda inakimbizana na Burundi kwny List.
 
Rwanda sijui inaingiaje. Very limited natural resources, insufficient land, no/little skilled labor, no free judiciary, no democracy etc.

Labda element wanayoweza kujivunia ni hiyo ya kumbambana na rushwa na hali ya usalama iko vizuri kama vile hapa Bongo tu

Kama hakuna hila za mabeberu ilitakiwa na Tanzania iwepo, lakini South Afrika ni mabeberu na mtu na mjomba wake, so sishangai
Siku ukijaliwa, tembelea ofisi za Rwanda Development Board (RDB) na za Tanzania Investment Center (TIC) utajua nani yuko serious na kuvutia wawekezaji.
Huko kwenu naskia hadi wizara ya uwekezaji iliundwa ili waziri mhusika akapumzike 😄
 
Siku ukijaliwa, tembelea ofisi za Rwanda Development Board (RDB) na za Tanzania Investment Center (TIC) utajua nani yuko serious na kuvutia wawekezaji.
Kuna yule tajiri felix mosha alisema kwny interview kuna eneo alikua anataka kujenga hotel nadhani ilikua Tanga akafukuzia kibali serikalini kwa karibu miaka mitatu wakawa wanamzungusha tu.

Sasa kuna kipindi akaenda Rwanda kwny mkutano wa wafanyabiashara,katika kuzurura zurura kuna eneo akalipenda akawa anataka kuwekeza,alivyoliulizia tu akaletewa hao RDB,Meya akaja chap,watu wa ardhi etc na within 48 hrs akawa amepata vibali vyote.

Na amejenga hotel ya nyota 3 huko.
 
Rwanda sijui inaingiaje. Very limited natural resources, insufficient land, no/little skilled labor, no free judiciary, no democracy etc.

Labda element wanayoweza kujivunia ni hiyo ya kumbambana na rushwa na hali ya usalama iko vizuri kama vile hapa Bongo tu

Kama hakuna hila za mabeberu ilitakiwa na Tanzania iwepo, lakini South Afrika ni mabeberu na mtu na mjomba wake, so sishangai
Mabadiliko ya kisiasa Tanzania ndiyo yanawaogopesha wawekezaji. Wawekezaji walichoambiwa na kuaminishwa kabla ya 2015 ni tofauti sana na sasa. Pia tutegemee utofauti mwingine baada ya 2025,ila kinachoshangaza wanaochukua nchi ni chama kile kile but different political perspective. Tusipobadilika tuendelee kutegemea wawekezaji wa vipindi vifupi vifupi kwa muda mrefu tu ndugu yangu,kila Rais atakuja na wawekezaji wake akimaliza tu muda wake nao wanatimka
 
Kuna yule tajiri felix mosha alisema kwny interview kuna eneo alikua anataka kujenga hotel nadhani ilikua Tanga akafukuzia kibali serikalini kwa karibu miaka mitatu wakawa wanamzungusha tu.

Sasa kuna kipindi akaenda Rwanda kwny mkutano wa wafanyabiashara,katika kuzurura zurura kuna eneo akalipenda akawa anataka kuwekeza,alivyoliulizia tu akaletewa hao RDB,Meya akaja chap,watu wa ardhi etc na within 48 hrs akawa amepata vibali vyote.

Na amejenga hotel ya nyota 3 huko.
Unamaana Tanzania hadi sasa hivi hatuwezi kufanya CHAP kama Rwanda eti
 
Hivi Mo ni jamii gani kati ya hao ulio wataja
Na huo uwekezaji wa Wachina na Wahindi wa kulipa watu wetu mishahara isiyokidhi mahitaji wala hauna faida kubwa sana kwa nchi

Zanzibar kwa mfano kuna uwekezaji mkubwa sana kwenye sekta ya mahoteli na utalii kwa ujumla unaofanywa na Wazungu hasa Wataliano lakini mchango wa sekta hiyo kwenye uchumi wa Zanzibar ni kidogo sana

Actually kuna arrangement zingine za safari za watalii zinafanyika huko nje ya nchi pamoja na malipp yote 100%, na mtalii anapoingia Zanzibar hatumii kabisa pesa mpaka anapoondoka. Sina hakika kama na serikali nayo inapata kodi stahili
 
Twambie nani yuko serious na uwekezaj baada ya tathmini yako
Siku ukijaliwa, tembelea ofisi za Rwanda Development Board (RDB) na za Tanzania Investment Center (TIC) utajua nani yuko serious na kuvutia wawekezaji.
 
Kuna yule tajiri felix mosha alisema kwny interview kuna eneo alikua anataka kujenga hotel nadhani ilikua Tanga akafukuzia kibali serikalini kwa karibu miaka mitatu wakawa wanamzungusha tu.

Sasa kuna kipindi akaenda Rwanda kwny mkutano wa wafanyabiashara,katika kuzurura zurura kuna eneo akalipenda akawa anataka kuwekeza,alivyoliulizia tu akaletewa hao RDB,Meya akaja chap,watu wa ardhi etc na within 48 hrs akawa amepata vibali vyote.

Na amejenga hotel ya nyota 3 huko.
Hapo kwenye kupata vibali na kuzungushana ndio tunapofeli kwa sana...!!
 
Unamaana Tanzania hadi sasa hivi hatuwezi kufanya CHAP kama Rwanda eti
Hapana mkuu inawezekana ila bado utashi wa kufanya hivyo kwa watendaji wa huku chini haupo tayari.

Jana tu kwny taarifa ya habari huko Bunda kuna jamaa anaitwa Kweka alikua analalamika kwa mkuu wa mkoa,kwamba amefuatilia vibali vya kujenga kiwanda cha kuchakata mazao na chakula cha kuku lkn ni miaka sasa anazungushwa so akasema ameamua kujenga hivyo hivyo bila vibali na atakayemsumbua basi yeye ataenda kumshtaki kwa rais maana rais aliwambia wajenge then mambo ya vibali yatafuata.

Unaweza ukapa picha sasa mkuu.
 
Back
Top Bottom