I like the last sentence!Nimeishia kuandika heading ya kimombo halafu huku chini natiririka kibantu.. Usinipige mawe.. Nimekosa maneno sahihi mafupi yanayotoshelea heading.. Ngoja sasa nifafanue
Denial state inatokana na neno deny.. Yaani kukataa ama kukataliwa.. Kwahiyo unapokuwa kwenye hiyo hali wewe ni makataa yani umekataliwa na hukubaliki tena.. Yani hata ufanye zuri gani litaonekana baya machoni pa wengi
Sasa ni afadhali kuwa kwenye denial state(makataa) kuliko kufikia hali ya kuwa condemned! Denial state is the primary level.. Condemned is the secondary level
Unapohukumiwa kifo hii inaitwa denial level.. Adhabu ya kifo inapotekelezwa unakuwa sasa wewe ni condemned! Ndio maana siku ya kunyongwa baada ya kumaliza taratibu zote chumba cha mwisho unachoingia kabla ya kufikia kitanzi (kifo chako) kile chumba pale kwenye mlango wake kuna maandishi makubwa mekundu yameandikwa kwa herufi kubwa CONDEMNED
Huo mlango ni wa njia moja tuu... Ni wa kuingia tu huwezi kuutumia kutokea.. Condemn kwa tafsiri ya Google ni laaniwa au laanifu.. Lakini pengine si neno sahihi sana.. Pengine Google wamelitumia kwakuwa LAANA haina TIBA ukishalaaniwa umelaanika hakuna rivasi.. YOU ARE CONDEMNED!
Kwahiyo sasa denial inavumilika kuna nafasi ya kurekebisha tena lakini condemn ni kwamba hufai tena.. Huna thamani tena..
Wengi wetu hupitia hii hali ya makataa (denial) kwenye jamii wakati wa makuzi yetu na kwenye harakati za maisha na sometimes kwenye mahusiano au kwenye mambo ya kijamii kama siasa, madaraka na uongozi.. Na hii yote husababishwa na tabia hulka ama nyota kufifia
Kuna baadhi hujistukia mapema na kuanza kutafuta suluhisho mapema sana na kuna baadhi huamua kuchagua njia sahihi ya kuishi na hiyo hali.. Shida ipo kwa wale ambao hawajikubali kuwa wana hiyo shida hivyo hujikuta ni watu wa kugombana na kila mtu kila mahali kila mahali na kujikuta wanajiona kama adui wa jamii (public enemy) hii hali ikiwa sugu unakuwa condemned na jamii na likikupata baya lolote badala ya jamii ikupe sympathy.
Ndio kwanza inashangilia na kufurahia...
Anakufa mtu mtaani kila mtu anasikitika na kuhuzunika sana na sifa zote nzuri anapewa yeye mpaka shetani anaona wivu halafu mtaa huohuo anakufa mwingine na jamii inalipuka kwa shangwe vifijo na nderemo..
Watu wana kunywa pombe kwa furaha
Wengine wanafanya karamu
Wengine wanataka waione maiti yako waipige mawe
Wengine wanataka kuitemea mate
Wengine bila kujali ni maiti bado wataendelea kuipiga na kuitukana
Wengine wanaweza hata kutafuta mafuta na kibiriti waichome moto
Ni usiku mwingi huu lakini niko macho.. Natafakari mengi mno.. Kuna binadamu tuna roho mbaya sana.. Huwa hatupendi kuona wengine wakipata ama kuwa na furaha.. Tutawatupia kimavi.. Makataa ya kishirikina (gundu la mavi) ogopa sana hii kitu.. Utakimbiwa mpaka na shetani..
Unajikuta unakuwa mtu wa mawazo mpaka unakonda.. Unatafakari nimewakosea nini hawa binadamu? Mbona najitahidi sana,? Tatizo ninini? Ni wakati unajiuliza haya kumbe nao wanakuwazia mabaya.. Unawashangaa wanakushangaa.. Mnabaki kuwindana.. Unawawinda ukiamini kuna wachache wanatumika kukuharibia kwa wengi.. Wanakuwinda useme tena watengeneze story za kukuponda
Katika magundu yote.. Ogopa gundu la kimavi cha kinyesi.. Pata picha pale unapohisi umekanyaga kinyesi tena na kiatu.. Hakuna maumivu unayopata lakini lazima uchechemee
Rest in peace Siad Barre.. Sorry Farrah Aidid also rest in peace....!!!! U 2...In advance !!!!?
Jr
sijalenga mtu ni mada ya woteMada fikirishi na ina mazingatio makubwa ndani yake ,inatokea sana kwenye maisha yetu ya kawaida hata kwenye mahusiano muhimu ni kuchange gia haraka kama unaona kuna sehemu unakosea kabla kufika stage mbaya zaidi.Hayo ndiyo nimejifunza kama kuna mtu kalengwa mambo yao nawaachia wenyewe .
Bagonza huyu bana... Unaweza kuwaza kuwa ni HEKIMA ya mwendawazimu... Lakini inatafakarisha sana... Waja wanaweza kuchuliana kifo sasaView attachment 1439340
Jr
Mkuui Mshana, hili jiwe 'ulilotupa gizani' nahisi limemgonga mtu kichwani.
Unapoteza muda kuumiza kichwa Chako kwa kitu ambacho hata ufanyeje uwezi kukuweka utakavyo.
Subiri kampen hamasisha watu vizuri, nenden mkaamue kwenye sanduku la kura.
Tofauti nahapo ndugu yangu n kilio Cha samaki machozi huenda na maji.
nakuombea best... BTW naikumbuka ile ishu yetuMshana Jr umetumia elimu kubwa.
Naona kama fumbo pengine waerevu wataling'amua.
Ila hicho kimavi ndo nshakisikia.
Wengine walitupiga hicho kimavi.
Ngoja koona iishe nina deal na wewe, ha haa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Denial state is not man made. Mostly inatokea ndani ya kichea chako mwenyewe.. it is pyschological condition.Hii denial state ni man made au inaweza tokea tu automatically you find yourself being denied?
Brother mshana. This is how unandika post inayoeleweka na deep thinkers. Ndio maana wale trash politicians huku kwenye post yako huwaoni.
Back to the topic hili jiwe ni special.. japokuwa kuna mtu ameguswa indirect.
Sent using Jamii Forums mobile app
NotedBahati mbaya sana, tena bahati mbaya sana wengi wetu tunakuwa tunapoteza muda huku mitandaoni ambako hata asilimia 10 tu ya watanzania wote haifiki. Ndio, 10% hatufiki, majority wanakubali yanayofanywa na "The condemned one"
He is not in denial state and he will not be condemned ever!