When you are in denial state..Make sure you are not condemned..!!!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,605
696,697
Nimeishia kuandika heading ya kimombo halafu huku chini natiririka kibantu.. Usinipige mawe.. Nimekosa maneno sahihi mafupi yanayotoshelea heading.. Ngoja sasa nifafanue
Denial state inatokana na neno deny.. Yaani kukataa ama kukataliwa.. Kwahiyo unapokuwa kwenye hiyo hali wewe ni makataa yani umekataliwa na hukubaliki tena.. Yani hata ufanye zuri gani litaonekana baya machoni pa wengi
Sasa ni afadhali kuwa kwenye denial state(makataa) kuliko kufikia hali ya kuwa condemned! Denial state is the primary level.. Condemned is the secondary level

Unapohukumiwa kifo hii inaitwa denial level.. Adhabu ya kifo inapotekelezwa unakuwa sasa wewe ni condemned! Ndio maana siku ya kunyongwa baada ya kumaliza taratibu zote chumba cha mwisho unachoingia kabla ya kufikia kitanzi (kifo chako) kile chumba pale kwenye mlango wake kuna maandishi makubwa mekundu yameandikwa kwa herufi kubwa CONDEMNED
Huo mlango ni wa njia moja tuu... Ni wa kuingia tu huwezi kuutumia kutokea.. Condemn kwa tafsiri ya Google ni laaniwa au laanifu.. Lakini pengine si neno sahihi sana.. Pengine Google wamelitumia kwakuwa LAANA haina TIBA ukishalaaniwa umelaanika hakuna rivasi.. YOU ARE CONDEMNED!
Kwahiyo sasa denial inavumilika kuna nafasi ya kurekebisha tena lakini condemn ni kwamba hufai tena.. Huna thamani tena..
Wengi wetu hupitia hii hali ya makataa (denial) kwenye jamii wakati wa makuzi yetu na kwenye harakati za maisha na sometimes kwenye mahusiano au kwenye mambo ya kijamii kama siasa, madaraka na uongozi.. Na hii yote husababishwa na tabia hulka ama nyota kufifia
Kuna baadhi hujistukia mapema na kuanza kutafuta suluhisho mapema sana na kuna baadhi huamua kuchagua njia sahihi ya kuishi na hiyo hali.. Shida ipo kwa wale ambao hawajikubali kuwa wana hiyo shida hivyo hujikuta ni watu wa kugombana na kila mtu kila mahali kila mahali na kujikuta wanajiona kama adui wa jamii (public enemy) hii hali ikiwa sugu unakuwa condemned na jamii na likikupata baya lolote badala ya jamii ikupe sympathy.
Ndio kwanza inashangilia na kufurahia...

Anakufa mtu mtaani kila mtu anasikitika na kuhuzunika sana na sifa zote nzuri anapewa yeye mpaka shetani anaona wivu halafu mtaa huohuo anakufa mwingine na jamii inalipuka kwa shangwe vifijo na nderemo..
Watu wana kunywa pombe kwa furaha
Wengine wanafanya karamu
Wengine wanataka waione maiti yako waipige mawe
Wengine wanataka kuitemea mate
Wengine bila kujali ni maiti bado wataendelea kuipiga na kuitukana
Wengine wanaweza hata kutafuta mafuta na kibiriti waichome moto
Ni usiku mwingi huu lakini niko macho.. Natafakari mengi mno.. Kuna binadamu tuna roho mbaya sana.. Huwa hatupendi kuona wengine wakipata ama kuwa na furaha.. Tutawatupia kimavi.. Makataa ya kishirikina (gundu la mavi) ogopa sana hii kitu.. Utakimbiwa mpaka na shetani..

Unajikuta unakuwa mtu wa mawazo mpaka unakonda.. Unatafakari nimewakosea nini hawa binadamu? Mbona najitahidi sana,? Tatizo ninini? Ni wakati unajiuliza haya kumbe nao wanakuwazia mabaya.. Unawashangaa wanakushangaa.. Mnabaki kuwindana.. Unawawinda ukiamini kuna wachache wanatumika kukuharibia kwa wengi.. Wanakuwinda useme tena watengeneze story za kukuponda
Katika magundu yote.. Ogopa gundu la kimavi cha kinyesi.. Pata picha pale unapohisi umekanyaga kinyesi tena na kiatu.. Hakuna maumivu unayopata lakini lazima uchechemee

Rest in peace Siad Barre.. Sorry Farrah Aidid also rest in peace....!!!! U 2...In advance !!!!?

Jr
 
Bahati mbaya sana, tena bahati mbaya sana wengi wetu tunakuwa tunapoteza muda huku mitandaoni ambako hata asilimia 10 tu ya watanzania wote haifiki. Ndio, 10% hatufiki, majority wanakubali yanayofanywa na "The condemned one"

He is not in denial state and he will not be condemned ever!
 
Bahati mbaya sana, tena bahati mbaya sana wengi wetu tunakuwa tunapoteza muda huku mitandaoni ambako hata asilimia 10 tu ya watanzania wote haifiki. Ndio, 10% hatufiki, majority wanakubali yanayofanywa na "The condemned one"

He is not in denial state and he will not be condemned ever!
You are trying to drag to somewhere we are not heading

Jr
 
Ni mada fikirishi

Shukran

Sent using Jamii Forums mobile app
.
tapatalk_1588345743413~2.jpg


Jr
 
Kuna mtu mmoja alinifanyia kibri, roho mbaya, ukatili, kutljaribu kupitisha maji yaririjie shambani kwangu ili shamba lake lisiharibike. Aligombana na majirani kadhaa, Mimi sikumuacha nilimtukana sana. Badae nikamuomba radhi lkn baada ya matusi.

Niliitwa kwenye mamlaka za serikali lkn niliomba radhi, majirani wakanizuia sana nisimuombe radhi lkn nilijua kwann niliomba radhi kuhofia denial. Ila makavu aliyapata kwa sasa ananiangalia kwa woga, kwa sabb nilitumia Maneno yoote yakaisha. Amebaki nayo, nahisi anajikataa sometimes, nilihisi nilifanya kitu Cha maana kwa sabb hatarudia Tena.

Kwa Sasa tunasalimiana. Heshima kubwa kweli kweli kumbe haya Mambo yapo
 
Bagonza huyu bana... Unaweza kuwaza kuwa ni HEKIMA ya mwendawazimu... Lakini inatafakarisha sana... Waja wanaweza kuchuliana kifo sasa
IMG-20200503-WA0026~2.jpg


Jr
 
Nilichojifunza kwenye maisha, wakati mwingine ni vyema kulegeza au kuacha kabisa baadhi ya principle zetu ili kuendana na jamii iliyokuzunguka.

Wakati mwingine jambo ulilozoea kulifanya kwenye jamii yako ukienda kwenye jamii nyingine linaonekana la ajabu; usilazimishe kuendelea kuliishi kwasababu utaendelea kuonekana wa ajabu tu, mpaka utakapoliacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom