When can Tanzania get into this kind of seriousness?

Glucky

Senior Member
Dec 16, 2009
123
40
Kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada ya ulinzi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya dola Milioni 450 (Zaidi ya Tsh. Bilioni 580) kwa kutumia rushwa katika kukamilisha dili zake na Tanzania, Jamhuri ya Cheki, Hungary na Saudi Arabia.

Awali taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza iliipa mwezi mmoja BAE Systems kukiri makosa yake au kufikishwa mahakamani

Awali SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.

Ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani ambaye aliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.

Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka jana nchini Uswizi alikokuwa akijificha.

Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia ilituhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi kuiuzia nchi ya Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.

"Kampuni ya BAE inajutia yaliyotokea na inakubali kubeba mzigo kwa matatizo yaliyotokea", alisema mwenyekiti wa BAE, Dick Olver.

BAE ilikiri kuwa malipo ya kamisheni kwa mtekelezaji wa dili la rada ya Tanzania hayakuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kwasababu hiyo BAE imekubali kutoa paundi milioni 30 ambazo baadhi ya pesa hizo zitatumika kwaajili ya manufaa ya Tanzania.

Mkurugenzi wa SFO, Richard Alderman alielezea kufurahishwa kwake na makubaliano yaliyofikiwa na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa uchunguzi wao kwa kampuni ya BAE.
 
I wish; i wish ingekuwa kesho; niamke nsikie fisadi fulani amkamatwa amefikishwa kwenye mkono wa sheria na yale mabilioni amaye yeye ayaita vijisent yamechukuliwa na yametumika kuagiza mdawa kwa ajili ya hospitali na zahanati zote nchini; walau siku ya kesho mwancnhi wa kawaida anaweza akaenda akapewa dawa muhimu BURE walau kwa siku hiyo moja tu mwananchi asiyekuwa na uhakika wa matibau akahakikishiwa kuwa ataapewa matibabu na madawa husika kwa wakati na huduma hii itakuwa bure kwa siku hiyo 1 tu!

Mungu atusaidie.
 
Huu ni usanii mwingine wa serikali ya UK, tangulini mpokea rushwa hukumu yake ikawa faini? na kina Chenge, Mramba, na mafisadi wengine wapigwe faini yaishe?

Cheni ya wala rushwa ni kubwa inabidi kila alie husika apelekwe mahakamani si vingnevyo,
UK inatetea walarushwa hasa ikiwa ni kwa maslai ya nchi yao, hapa ndio utaona hizi nchi zinazodai zimeendelea ni wanafiki kiasi gani!! Shame on UK Gov, shame on BAE!!.
 
Back
Top Bottom