WhatsApp yasogeza mbele muda wa kuanza kutumika rasmi kwa sera yao mpya ya faragha

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya sintofahamu iliyoendelea kwa muda wa wiki moja sasa, WhatsApp imesema kuwa inasogeza mbele muda wa kukubaliana na sera yake mpya ya faragha hadi Mei 15, 2021 badala ya tarehe ya awali iliyokuwa imewekwa ya Februari 8.

Katika chapisho la blogu, kampuni hiyo ya mawasiliano inayomilikiwa na Facebook imesema kuwa inafanya kazi kuondoa taarifa potofu zinazosambazwa kuhusu sera yake mpya ya faragha, ikiwahakikishia watumiaji wake kuwa "unachokituma baina yako na rafiki na familia yako kinabaki kati yenu," hata WhatsApp haiwezi kuona kinachoendelea.


WhatsApp haikusema ikiwa itafunga akaunti za watumiaji itakapofika Mei 15, lakini imetaja kuwa mteja anaweza kuwa na "uchaguzi wa kibiashara" baada ya kupitia kwa umakini sera mpya ya faragha itakapofika Mei 15.

Chapisho hilo la WhatsApp limeongeza kuwa sera mpya ya faragha ya WhatsApp haiongezi wigo wake wa kukusanya taarifa, ikisisitiza kuwa haihifadhi kumbukumbu za simu zinazopigwa wala kuona taarifa za eneo la kijiografia alilopo mteja wala haishirikishi taarifa za mteja kwa Facebook kuhusu majina na namba za simu zilizopo katika simu ya mteja.

Kumeshuhudiwa kuhama kwa maelfu ya watumiaji wa WhatsApp baada ya taarifa kuhusu mabadiliko ya sera mpya ya faragha, huku mitandao shindani ya Telegram na Signal ikiwahakikishia wateja wake kuwa watakuwa salama. Lakini hakikisho hili jipya la WhatsApp linatoa matumaini kuwa changamoto ya usalama wa taarifa za wateja, kama ilikuwepo, inafanyiwa kazi.
 
Back
Top Bottom