WhatsApp Unafanya Majaribio Ya Mfumo Wa Kutuma Na Kupokea Crypto

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Miezi sita iliyopita kampuni ya Meta ilitoa Wallet yake ya Crypto ambayo inaitwa Novi Wallet na inatumia Stablecoin ya Pax Dollars (USDP) ambayo ni crypto yenye thamani sawa na Dola 1.

WhatsApp imeanza majaribio ya kuunganisha Wallet ya Novi na WhatsApp hivyo utaweza kutuma na kupokea pesa moja kwa moja katika WhatsApp kwa kuunganisha Wallet ya Novi na app yako ya WhatsApp.

Majaribio hayo yameanza kwa watumiaji wa Marekani ikiwa ni sehemu ya kujaribu mfumo na kucheck utaratibu wa kupata vibali na kupima mfumo. Mfumo wa WhatsApp hauna makato katika mihamala!

Signal pia imeweka uwezo wa kutuma Crypto na ipo katika majaribio. Apps nyingi zinapambana kuweka urahisi huo ili kutangulia mbele katika ulimwengu wa malipo ya mitandao na umiliki wa fedha za kidigitali.
 
Crypto ya Facebook sio really crypto
Ni centralized na ipo backed up na US dollars
Kuiita Crypto ni marketing strategy tu, ila technically Novi ni digital currency service kama ilivyo Mpesa

Vodafone walijitoa hata kabla Libra haijabadilishwa jina na kuitwa Novi, wakasema wanarudi ku focus na Mpesa yao

Kwa sababu ni concept ile ile kama ya kwao, inahitaji Agents kama Mpesa

Tofauti Agents wake, ni kama Banks, Services kama Paypal, au Vodafone etc

Sio crypto kwa maana halisi ya crypto
 
Waangalie suala la makato wanaweza kupiga bao sana....hawa waliopo wameota mapembe
Hakika yaani hapa wakiwa na makato ya kawaida ukilinganisha na hawa waliopo basi pesa nje nje.
 
Crypto ya Facebook sio really crypto
Ni centralized na ipo backed up na US dollars
Kuiita Crypto ni marketing strategy tu, ila technically Novi ni digital currency service kama ilivyo Mpesa

Vodafone walijitoa hata kabla Libra haijabadilishwa jina na kuitwa Novi, wakasema wanarudi ku focus na Mpesa yao

Kwa sababu ni concept ile ile kama ya kwao, inahitaji Agents kama Mpesa

Tofauti Agents wake, ni kama Banks, Services kama Paypal, au Vodafone etc

Sio crypto kwa maana halisi ya crypto
Shukurani kwa nyongeza
 
Naziona Mpesa na Tigo zikiwa absolete
Haziwezi kuwa absolute itachukua muda. We jiulize na uwepo wa simu na huduma za malipo ni watu wangapi tz wananunua ma kufanya malipo online mpaka leo?
 
Sisi tupo na PI Network jiunge leo bila malipo
1π! Pi is a new digital currency developed by Stanford PhDs, with over 25 million members worldwide. To claim your Pi, follow this link Pi Network and use my username (Laureankiiza) as your invitation code.
 
Back
Top Bottom