WhatsApp Kutofanya Kazi Baadhi Ya Simu janja December 31

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
Mtandao wa WhatsApp hautofanya kazi kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window 'Window Smartphone' kufikia Disemba 31, kwa mujibu wa mtandao wa Mirror.



WhatsApp

Mtandao huo unaotumiwa na mabilioni ya watu hivi sasa, una mpango wa kuondoa huduma hiyo kwenye simu janja za makampuni mengine wiki za hivi karibuni.
Simu zitakazoathirika katika miezi ya hivi karibuni ni pamoja na baadhi ya simu janja za Android pamoja na baadhi za iPhone.
Simu za Android toleo la 2.3.7 hazitakuwa na uwezo wa kutengeneza akaunti mpya au kuboresha (update) akaunti zao za zamani ifikapo Februari 1.
Pia simu za iPhone zinazofanya kazi kwenye mfumo wa iOS 8 pia hazitaweza kutengeneza akaunti mpya au kuthitisha akaunti zao za zamani ifikapo tarehe hiyo.
"Hautakuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window baada ya Disemba 31, 2019, pia WhatsApp inaweza isipatikane kwenye 'Microsoft app store", ulisema uongozi wa mtandao huo.
FsWUqRoOsPu.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Technolojia inatufanya muda wote tuende na speed ya mabadiliko yake! Android version ulizozitaja na iOS za iPhone ulizozitaja zoote ziko kwenye simu za zamani. Wenye simu za zamami jamani nunueni simu mpya technolojia ndo hivyo tena inawaacha! Jamani Technolojia haina huruma!
 
Rahisisha mkuu, no simu gani zitashindwa kupata whatsaap? Kwa lugha rahisi!
 
Hawa jamaa ndio mnasema wanasanabisha migogoro Afrika ili waibe raslimali?!
Mbona tutawapelekea wenyewe tu bila kupenda!

Hapo ni simu,kesho ving'amuzi vya TV,kesho kutwa TV zenyewe,baadae hata taa za Umeme watatengeneza za kilipia kama vinga'amuzi.Tutabaki na sitglers gorge ila tunalipa wenye akili.

Basi sawa wakati mwingine utumwa huwa unazoeleka.Mijadala ya watumwa wenye uwezo wataanza kutamba humu wakiwatukana watumwa wasio na uwezo wa kununua simu mpya.

Nakupenda Afrika


Sent using Jamii Forums mobile app
 
wazungu wamezidi usumbufu, kila siku kutusumbua tusiokuwa na teknolojia! Nashauri sasa tuhamie mitandao ya wachina ambao hawana usumbufu! tuwaache na whatsapp yao.
 
Hizi ndio njia za kutengeneza Pesa wanazozifanya Wazungu waendelee kuwa juu zaidi sisi wa Afrika tuendelee tu kuzubaa na sisi tuwawekee limit kuchukua raslimali zetu ili tuende sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu nauliza whatsap siku hizi iko Monitored na Facebook? Maana kila nikifungua baada ya kufanya update inaandika From Facebook

Screenshot_20191231-084419_1577771231829.jpg
 
Technolojia inatufanya muda wote tuende na speed ya mabadiliko yake! Android version ulizozitaja na iOS za iPhone ulizozitaja zoote ziko kwenye simu za zamani. Wenye simu za zamami jamani nunueni simu mpya technolojia ndo hivyo tena inawaacha! Jamani Technolojia haina huruma!
Unaweza ku-update firmware bila kubadili simu
 
Unaweza ku-update firmware bila kubadili simu
Handset (simu) hiko limited na kiwango cha firmware kutokana na hardware architecture za processor speed na storage na Ram kwasababu update version za firmware zinakuwa ni kubwa na nilazima ziendane na handset.
 
Hizi ndio njia za kutengeneza Pesa wanazozifanya Wazungu waendelee kuwa juu zaidi sisi wa Afrika tuendelee tu kuzubaa na sisi tuwawekee limit kuchukua raslimali zetu ili tuende sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Raslimali zetu ni zao sisi ni walinzi tu hata tukibaki nazo hazina thamani sisi tunamiliki mali wao wanamiliki akili at the end ni lzm tutegemeane
 
At the end watakuja na suggestions zingine wapige pesa hii ndo dunia ya biashara unatengeneza tatizo kupata Pesa kisha unatengeneza ufumbuzi unapiga tena pesa
 
Vipi Kuhusu hizi Smart Vitochi Nimesikia nazo Zitatumia Whatsapp, Je watakuwa salama kweli na bei yao ya 39,999.
 
Back
Top Bottom