WhatsApp kufanya maboresho kwenye mfumo wa ujumbe sauti (Voice notes)

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
8,440
2,000
Mtandao wa WhatsApp unao milikiwa na kampuni ya facebook unafanya maboresho kwenye ujumbe sauti yaani voice notes.

Awali mtandao huo ulikuwa unalazimika mtumiaji kurudi kwenye Application yake endapo akitumiwa ujumbe wa sauti.
Hivyo mwanzo ukitumiwa ujumbe wa sauti endapo haupo kwenye Application ya WhatsApp yaani ukiwa nje ya WhatsApp ilikuwa lazima urudi kwenye Application hiyo ili kuusikiliza na kuujibu.

Lakini kwa sasa maboresho hayo yatamruhusu mtumiaji wa WhatsApp kusikiliza ujumbe sauti hata akiwa nje ya Application ya WhatsApp hivyo ataujuta ujumbe na kuucheza kama alivyo kuwa akijibu ujumbe wa kawaida.
Hivyo atasikiliza/kucheza ujumbe sauti na kuujibu hata akiwa nje ya WhatsApp na option hiyo italeta jina/kikundi ujumbe uliko toka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom