Whatsapp: Blue Tick Read Confirmation Inakukera ?

KIOO

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
6,154
5,680
Habari zenu wakuu.

Natumai mu-wazima kabisa.............well,kama uzi unavyojieleza hapo juu kuwa ni jinsi gani unaweza kuondoa double blue ticks za whatsapp pale mtu anapokutumia msg,kisha ukaifungua na kuisoma nae akajua kuwa tayari umeshaisoma lakini ukachelewa kujibu aidha uko barabarani unaendesha au ikatokea sababu nyingine tu ukashindwa kujibu kwa muda muafaka au kutojibu kabisa kutokana na sababu moja au nyingine iliyokupelekea kushindwa kujibu msg yake ilhali ukiwa tayari umeshaisoma.

Nimeskia wengi wakilalamika kuhusu hili na kushindwa kujua nini cha kufanya na wengine kutokufurahi hii new feature kutoka kwa Whatsapp developers.

Hivyo bila ya kupoteza muda hebu tuangalie unawezaje kusoma msg za mtu na yeye asione blue ticks kwenye screen yake na kumpelekea kuamini kuwa bado hujausoma ujumbe wake hivyo itampelekea kusubiri mpk aone blue ticks na kuamini kuwa tayari umeshaisoma msg yake japo ipo option ya kuweza ku-click akaona kuwa umesoma lakini sio kupitia double blue ticks.

whatsapp-azul-tick-doble1-660x400.jpg



Well,zipo njia mbili tatu hivi lakini leo tuelekezane moja ambayo ndio kubwa,kuliko ya kusoma msg ukiwa ume-switch on Flight Mode au kutumia Whatsapp widget au kuzima Internet Data Connection.Na bila ya kupoteza muda hebu tutazame njia hiyo kama ifuatavyo wakuu ;-

Kwanza kabisa hakikisha umeiruhusu simu yako kupokea applications from Unknown Sources kwa sababu application utakayoi-download haitokei Play Store utaipata kutokea Whatsapp Website hivyo ruhusu simu yako kupokea application from Unknow sources kama hii picha hapa chini inavyoonesha...

1443159_q1_3f6f0b7586f63da1a9a502a7bf122140.png


Baada ya kuruhusu simu yako kupokea application ambazo hazitoki kwenye Play Store utatakiwa kuingia kwenye Official Website ya Whatsapp na ku-download New and Latest Version ya Whatsapp 2.11.452 sidhani kama tayari wameshaiweka kwa Play Store sina hakika ila sisi tui-download kutokea Whatsapp Website kwa kuandika www.whatsapp.com/android/ au kwa urahisi unaweza uka-click hii link hapa chini ambayo itakupeleka kwenye website yao moja kwa moja,click haya maneno yaliyopigiwa mstari hapa chini...

NewWhatsapp.apk

1443159_3_882ec1bebf722ae3a1fcca7f2432429c.png


Baada ya kufika kwenye hiyo site kama picha inavyoonesha hapo juu uta-click on "Download Now" ikimaliza ku-download utaifungua na itakutaka u-Verify na Ku-Install kama hii picha hapa chini inavyoonesha pia...

1443159_3_a61b486176f9c2a7cbc68ab7479400b0.png


Click hapo ianze Ku-Install na ikimaliza Ku-Install itakueleza kuwa version hii ita-replace version iliyopita na data zako zote za nyuma zitaseviwa na hakuna data yoyote itakayopotea wala kubadilishwa utatakiwa click on "OK" itaanza Ku-Install ikimaliza Insallation itakujulisha kuwa tayari,then utaifungua kwa ku-click on "Open" iache ifunguke na itakupeleka moja kwa moja kwenye application yako mpya "new version" ya whatsapp kama inavyoonesha hapa chini...

1443159_3_347b1bd986c66775d9d15e6a5c3296bf.png


Utatakiwa ku-click on "Menu" kwenye simu yako kisha uta-click on "Settings" kama duara linavyoonesha hapo juu then baada ya ku-click "Setting" uta-click on "Account"

1443159_3_a39ab05e02376346bfb0bdaf61ef0b16.png


Ukisha-click "Account" utatakiwa ku-click on "Privacy"...

1443159_3_19c55b2095da0aaa5c1a4308b0c38828.png


Ukisha-click on "Privacy" kama inavyoonesha hapo juu then utatakiwa kushuka chini utaona sehemu ina "tick" na imeandikwa "Read receipts" utatakiwa ku-click hapo...

1443159_3_c7073906f30af6f242caf54593d33e82.png


Ukishaigusa hiyo tick hapo utakuwa umefanikisha zoezi lako la kuondoa double blue ticks kwa mtu atakayekutumia ujumbe hata ukiusoma ujumbe aliokutumia hataweza kuona tick za blue kwenye screen yake.Ila pia hii ni kama vile last seen kwa sababu hata wee hautaona blue ticks kama mtu akisoma ujumbe wako uliomtumia kwa hiyo hutajua kama amesoma au bado hajasoma ujumbe wako,
Ooups !.

Ila kitakachokuwezesha kujua kama amesoma au hajasoma utaugusa huo ujumbe uliomtumia kwa sekunde kama mbili hivi na kwenye screen yako itatokea hivi...

1443159_3_b745ded4a2372fbc0bb2b54c747a2725.png


Juu kabisa kwenye screen yako utaona alama ya (i) iliyozungushiwa kiduara hapo ndipo patakujulisha kuwa ujumbe wako umesomwa au laa.......lakini pia hapo napo kuna maelezo mawili matatu ya kuelezea ila kwa leo tupo kwenye kuelezea blue ticks pekee.

Am wishing you all the best kama kuna sehem nimekosea ruksa kurekebishwa coz najua BINADAM huwa wanatazama sana mabaya kuliko mazuri si mbaya na kama utakuwa umependezwa basi si mbaya kama utagonga...

images



================


Kwa wale wanaotumia iOS si mbaya kama utaingia kwenye hii link hapa chini then go step-by-step ku-disable hiyo feature,ALL THE BEST.

Blue Tick For iOS


THANKS A LOT.
 
Vipicha kwani umevi upload site gani mbona vidogo Mno vile nafikiri jishughulishe wewe usibadilishe wewe usisubiri mods wakupe msaada
 
Na yeye kule akibofya hiyo (i) si ataona kama na wewe umesoma msg yake? :-D mbona kituko sasa ichi?
 
Mi mbavu sina yotee hayo nini? Labda ungenishawishi kuniambia wasap wametoa apps mpya hapo sawa ila mmh
 
Last edited by a moderator:
Na yeye kule akibofya hiyo (i) si ataona kama na wewe umesoma msg yake?

Mkuu,sidhani kama una uhakika na unachokisema kiongozi kama utamtumia mtu msg halaf hata kama hajaisoma click hiyo (i) then uone nini kinatokea.

Na hapa point inayoongelewa ni kuhusu wanaokereka na blue tick kama kwako ni sawa basi si mbaya ukaiacha tu kiongozi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom