What's wrong? Wabunge waliomaliza muda wao hawajalipwa na serikalini kazi zimesimama!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
WanaJF,
Kuna mdau mmoja amenihabarisha kwamba hali ya kifedha serikalini hususani kwenye mawizara na idara ni mbaya kupita kiasi. Inasemekana tangu bajeti ya mwaka huu wa fedha ilipopita mwezi julai 2010 hakuna fedha inayotolewa na serikali kwa shughuli yoyote ya maendeleo. Eti tangu mwezi julai 2010 watumishi wengi wa serikali wanasoma magazeti tu na kula mshahara. Mdau anaeleza kwamba kumbe hata wabunge waliomaliza muda wao katika bunge lililopita mpaka leo hawajalipwa mafao yao. Jamani wahusika ambao ni wanaJF tafadhali mtujulishe kuhusu suala hili, kama ni kweli?? Na kama ni kweli, kuna tatizo gani hapa na serikali ya jk?? Mbona wakati wa nkapa hali ya aina hiyo haikuwepo?? Kuna kitu kinafichwa hapa nini??
 
Hata sisi watu wa kawaida huwa wanatucheleweshea mafao yetu hebu wacha na wao waonje shubiri kidogo kama ni kweli hayo unayoyasema!
 
Enzi hizo wakati wanakaa kwenye mjengo full ac, kwenye magari full ac posho na allowances kupitisha mikataba bila kuangalia hali halisi ya watanzania wenzao sasa leo wako nje ya mjengo let them face reality
 
ha ha ha! Hao wabunge ka-muda kadogo tu hivi wanalalama, babu yangu alifanya EAC miaka ya 60-70 mpaka anakufa mwaka 2004 hajalipwa mafao yake, katuachia wajukuu tufatilie lakini tumeambulia patupu. wacha waionje shubiri ndo waijue serikali yao kwa mtanzania wa hali ya chini....
 
Sema kwa watu wa kawaida mishahara ikichelewa ndo suala la kujadili... Lakini ukisemea mawaziri na wabunge kutolipwa pesa nitakushangaa kidogo maana hawa watu wana pesa nyingi....... Kuna waziri mmoja ana wadogo zake watatu ameweka pesa kwenye account zao Marekani si chini ya $2,500,000.00. Ukitaka ushahidi tuwasiliane.
 
Serikali haina fedha hivyo basi tumerudi enzi ya mzee RUKSA JK amekula fedha zote na mwanaye RIDHIWANI,ni ukweli usiopingika maofisi hakuna fedha za maendeleo na hivyo watu wapowapo huu ni mwezi wa 8
 
WanaJF,
Kuna mdau mmoja amenihabarisha kwamba hali ya kifedha serikalini hususani kwenye mawizara na idara ni mbaya kupita kiasi. Inasemekana tangu bajeti ya mwaka huu wa fedha ilipopita mwezi julai 2010 hakuna fedha inayotolewa na serikali kwa shughuli yoyote ya maendeleo. Eti tangu mwezi julai 2010 watumishi wengi wa serikali wanasoma magazeti tu na kula mshahara. Mdau anaeleza kwamba kumbe hata wabunge waliomaliza muda wao katika bunge lililopita mpaka leo hawajalipwa mafao yao. Jamani wahusika ambao ni wanaJF tafadhali mtujulishe kuhusu suala hili, kama ni kweli?? Na kama ni kweli, kuna tatizo gani hapa na serikali ya jk?? Mbona wakati wa nkapa hali ya aina hiyo haikuwepo?? Kuna kitu kinafichwa hapa nini??

Kwa ufupi serikali haina pesa za kuwalipa kwani zilitumiwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi uliopita, ndo maana imebidi serikali kutengeneza pesa mpya ili kufidia pengo hilo.

Pia serikali ilizuia malip hayo ili kulipa DOWANS
 
Sema kwa watu wa kawaida mishahara ikichelewa ndo suala la kujadili... Lakini ukisemea mawaziri na wabunge kutolipwa pesa nitakushangaa kidogo maana hawa watu wana pesa nyingi....... Kuna waziri mmoja ana wadogo zake watatu ameweka pesa kwenye account zao Marekani si chini ya $2,500,000.00. Ukitaka ushahidi tuwasiliane.

Mkuu hicho ndicho tunachokitaka hapa jamii mweke hadharani 2mjadili halizipataje hzo hela!
 
Kwa ufupi serikali haina pesa za kuwalipa kwani zilitumiwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi uliopita, ndo maana imebidi serikali kutengeneza pesa mpya ili kufidia pengo hilo.

Pia serikali ilizuia malip hayo ili kulipa DOWANS

Mhh Mkuu, nina wasiwasi na uelewa wako wa fedha.... umenikumbusha during Idi Amin time walimwambia uchumi mbovu hakuna hela akaagiza central bank i-print more cash!!
 
Back
Top Bottom