What's the story: Ulipataje kazi unayofanya au uliyowahi kufanya?

Mchizi wangu alituma kipande cha picha ya Gazeti kwenye group letu la secondary. Kipande hicho cha gazeti kilikuwa na tangazo la nafasi za kazi ya taasisi fulani.
Kipindi hicho nilikuwa nafanya field kwenye kampuni moja hivi kubwa tu ya Mheshimiwa mmoja.
Niliandika maombi ya kazi na CV kisha nikatuma kwa wahusika wenye taasisi yao.
Mungu si Athuman, baadae jina langu lilikuwa miongoni mwa majina ya walioitwa kwenye interview.
Kimbembe kilikuwa hiyo interview yenyewe maana ilikuwa inafanyika kipindi ambacho ni cha mitihani ya mwisho wa semester katika taasisi niliyokuwa naendelea na masomo yangu ya Shahada ya kwanza.
Bahati nzuri interview ilikuwa ni ya siku mbili, siku ya kwanza sikwenda kuhudhuria interview kwa sababu nilikuwa na paper mbili siku hiyo. Siku ya pili nilienda kuhudhuria interview kwa kuchelewa sana nilikuwa mtu wa mwisho kwa sababu nilikuwa ndo natoka kwenye mtihani, siku hiyo nilikuwa na mtihani mmoja tu.
Nilifanya interview na namshukuru Mungu Baba mwezi mmoja baadae niliitwa kazini.
Hapo nikafanya taratibu za postponement maana kazi yenyewe nilikuwa naenda kufanya mkoa mwingine. Hawakuamini wenzangu niliokuwa nasoma nao kama kweli nilikuwa naahirisha masomo na kwenda kuanza kazi hukooooo mkoani.
Nina miaka kadhaa sasa kazini, pia nimerudi darasani chuo kingine mkoani, naendelea na kitabu nitimize ndoto yangu kielimu, umebaki mwaka tu kuhitimu level niliyoondokea.
hicho chuo kingine ulianza mwanzo au uliendelea pale ulipoishia?
 
Soon after graduation nilibahatisha namba ya bosi nikaomba kujitolea, kumbe huyo bosi alikuwa na ofisi nyingine nyingi zaidi ya ile niliyoifahamu.
Nilijitolea miezi kadhaa nikilipwa posho kidogo.

Baada ya kufanya kazi ilifika kipindi nikaona wana uhitaji wa wafanyakazi nikaacha kazi ya kujitolea nikatulia geto.
Baada ya siku mbili nikapigiwa simu nikaanza kazi rasmi.....
Soon naacha hii kazi nshapata exposure ya kutosha.
hakika kujitolea kuna fungua milango. vijana changamkieni fursa ya kujitolea. changamoto huwa ni ntaendaji kufanya kazi wakati sina hela ya kujikimu? tafuta sehemu ya karibu ambayo inaweza fikika hata kwa mguu ambayo unaweza unga gari moja likakusogeza then unatembea kwa mguu, vile vile chamgamkieni ofisi za mikoni hakuna stress na hakuna competition.
m nakumbuka nilifanyaga field taasisi fulani kubwa mpaka wakanishauri baki tukuajiri, semister zilizobaki soma online halafu ukimaliza cheti chako peleka tcu wakihakiki, i turned down their offer kwa sababu another great opportunity was waiting for me
 
Wakati nasoma nilikuwa nafanya biashara nilipata vipesa nikasema ngoja nilime kilimo cha kisasa nikatafuta heka tatu morogoro nikalima nyanya.

Daah ikatokea mvua kubwa ikasomba kila kitu. mwaka uliofuata nikamaliza chuo..sikutaka kutafuta kazi nikaendelea na biashara ya Mifugo kwa Wakenya wanajua mnada wa n'gombe unaoanzia Pakase kiseriani hadi Nai.

kuna vile tunataka tuishi ila wazazi nao wana namna ambavyo wanataka tuishi. mwisho nikaingia maliasili na utalii.. nikafanya kazi.

Niliingia kwa Mgongo wa mtu sikutaka jinsi alivyokuwa ana nitreat hata kama kanifanyia mpango wa kazi....sikuwa free hata kutoa wazo hasi... RRONDO sijui kama unakumbuka mwaka 2016 mwishoni nilikuomba ushauri fulani.... nikaacha kwa kisingizio cha kusoma.

Wengi mnapenda kuwa na watu kwenye taasisi wawaingize kazini ila ni mbaya saana malipo yake utayaona ukishaajiriwa...japo siyo wote wapo hivyo.
Hahaa umenikumbusha tulipiga ka joint-project ka kilimo Mlali, tukiwa hatuna class hao tung'oa maana sio mbali na tulipokua tunasomea, mwishoni mazao yakasombwa na mvua

Ka boom ka kujibana bana kakawa kamesepa.
 
hicho chuo kingine ulianza mwanzo au uliendelea pale ulipoishia?
Bahati mbaya kozi niliyokuwa nachukua kwenye chuo cha zamani haitolewi na institution nyingine yoyote ile mkuu.
Hivyo nilishindwa kufanya credit transfer na ikabaki kuwa hivyo huko mpaka leo.
Nilianza tena fresh mkuu lakini siku hazigandi hivi sasa ndo namalizia, Mungu mkubwa.
 
M
Hahaa umenikumbusha tulipiga ka joint-project ka kilimo Mlali, tukiwa hatuna class hao tung'oa maana sio mbali na tulipokua tunasomea, mwishoni mazao yakasombwa na mvua

Ka boom ka kujibana bana kakawa kamesepa.
Bila shaka Mlali unayoiongelea mkuu ni ya pale jirani na Mzumbe
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Baada ya kumaliza chuo nilisota mwaka mzima nyumbani. Kuna siku nikaona tangazo benki fulan wanataka watu, basi kama kawaida nikatuma maombi.

Baada ya wiki mbili hiyo siku kuna mtu alikua ananisumbua sana kwenye simu mpaka tukagombana nikaacha kupokea simu zake basi akaamua kubadili namba tofauti nikawa napokea ila nilipogundua ni yeye nikawa
nakata.

Basi baada ya dakika kam 20 za usumbufu namba mpya ikaingia nikajua ndo yule yule nikapokea na kuanza kuporomosha matusi bila hata kusikiliza upande wa pili, yule mtu akaniuliza unanijua mimi ni nan? Nikamjibu ndio wewe si fulani.....akakata simu. Baada ya dk 2 nikacheki namba m-pesa nikaona jina na kuamua kumsearch google mara nikaona kumbe ni hr wa hiyo benki, acha nipagawe nikapiga tena ile namba ikaita weeeee haikupokelewa, nikapiga tena nikaanza kuomba msamaha na yeye acha aanze kunisema kwann napokea simu bila kumsikiliza mtu naanza kutukana, ikabidi niwe mpole ndo akaniambia ninahitajika kwenye interview.

Mpaka leo nipo kwenye hii ofisi ila nilijifunza kitu
Kweli we ni Winlicious......
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Haha yeah ishu ni kubeba vifaa,tablets nlitumia once iko vzr ingawa ni ngumu kupika data ukifananisha na ile ya kuandika hahahaa nlikua napenda watoto wadogo walivyokua waoga kupanda mizani....
Karibu RUKOMA AP ipo jirani na Ruhita.
Eeeeeh bwana eeh Jamii forums inachanja mbuga hadi Ruhita. Duh
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Mchizi wangu alituma kipande cha picha ya Gazeti kwenye group letu la secondary. Kipande hicho cha gazeti kilikuwa na tangazo la nafasi za kazi ya taasisi fulani.
Kipindi hicho nilikuwa nafanya field kwenye kampuni moja hivi kubwa tu ya Mheshimiwa mmoja.
Niliandika maombi ya kazi na CV kisha nikatuma kwa wahusika wenye taasisi yao.
Mungu si Athuman, baadae jina langu lilikuwa miongoni mwa majina ya walioitwa kwenye interview.
Kimbembe kilikuwa hiyo interview yenyewe maana ilikuwa inafanyika kipindi ambacho ni cha mitihani ya mwisho wa semester katika taasisi niliyokuwa naendelea na masomo yangu ya Shahada ya kwanza.
Bahati nzuri interview ilikuwa ni ya siku mbili, siku ya kwanza sikwenda kuhudhuria interview kwa sababu nilikuwa na paper mbili siku hiyo. Siku ya pili nilienda kuhudhuria interview kwa kuchelewa sana nilikuwa mtu wa mwisho kwa sababu nilikuwa ndo natoka kwenye mtihani, siku hiyo nilikuwa na mtihani mmoja tu.
Nilifanya interview na namshukuru Mungu Baba mwezi mmoja baadae niliitwa kazini.
Hapo nikafanya taratibu za postponement maana kazi yenyewe nilikuwa naenda kufanya mkoa mwingine. Hawakuamini wenzangu niliokuwa nasoma nao kama kweli nilikuwa naahirisha masomo na kwenda kuanza kazi hukooooo mkoani.
Nina miaka kadhaa sasa kazini, pia nimerudi darasani chuo kingine mkoani, naendelea na kitabu nitimize ndoto yangu kielimu, umebaki mwaka tu kuhitimu level niliyoondokea.
Mkuu nifumbue hili linawezekana kama uliishia mwaka wa pili chuo flani ukaenda mkoa mwingine kule ukapata chuo na kuendelea na mwaka uleule na kwa kozi zinazolingana? Hii imekaaje tafadhari!
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Kazi ya kwanza, walikuja darasani (kupitia kwa mkuu wa idala enzi hizo), FoE tukakusanya makaratasi yetu then usahili then nikapata kazi (wazungu), ya pili mshikaji aliiona imetangazwa gazetini... Nikaomba kwa kutuma CV tu... Nikaitwa nikafanya usahili nikaipata.... Ya tatu, idala yetu kwenye kazi ya pili ilikuwa OUTSOURCED... then tukahamia kwa muajili mpya... Ya nne, kuna jamaa alikuwa anafanya kazi ya kuitengeneza ofisi ya kampuni mpya inayoanzishwa, mwenye tenda ya matengenezo hayo, alikuwa ni supplier wa kampuni yangu ya tatu... Nikauliza wakaniambia, then nikampa CV akaipeleka... Baada y amiezi SITA nikaitwa kwenye usaili then nikaipata.... Ya mpaka sasa, kuna mtu nilikuwa naye kwenye ile ajira ya kwanza, akawa ametangulia huku niliko sasa.... walipokuwa wanahitaji watu wa aina yangu, wakaitangaza magazetini, lakini wakapata FRESH GRADUATES... wakati wao walikuwa wanataka mtu atakayeweza kuachiwa mitambo ( mwenye uzoefu) Basi aliponipigia simu kuniulizia kama namfahamu yeyote mwenye sifa wanazozitaka, NIKAMWAMBIA NTAKUJA MIMI MWENYEWE... BASI KWA VILE WALIKUWA WANAWATAKA WAWILI, THEN NIKAMTAFUTA NA MWINGINE ALIYEKUWA SUBORDINATE wangu kwenye ajira ya pili na ya tatu
Mkuu kama kampuni uliyopo ina department ya Mechanical naomba unishike mkono, nimegraduate pale COET mwaka jana
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Mkuu nifumbue hili linawezekana kama uliishia mwaka wa pili chuo flani ukaenda mkoa mwingine kule ukapata chuo na kuendelea na mwaka uleule na kwa kozi zinazolingana? Hii imekaaje tafadhari!
huo ni mfumo unaitwa credit transfer simple tu unaenda chuo unachotaka kuhamia unauliza kama kuna nafasi unawaelezea ulikosoma ukaishia then unarudi chuo ulichokuwa unasoma mwanzo wanakupa utaratibu wa kuhamisha credit zako
kama ulikuwa na mkopo wa bodi then unaenda bodi ya mikopo wanakupa utaratibu wa kuhamishia mkopo wako chuo husika
 
Anhaa shukrani mkuu.
 
Back
Top Bottom