What's the story: Ulipataje kazi unayofanya au uliyowahi kufanya?

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
6,279
10,272
Habari wadau,

Huu ni uzi spesheli kwa waliowahi au walioajiriwa, kwa wale wataalamu wakujiajiri hapa siyo sehemu sahihi.

Kuna njia mbalimbali ambazo watu huzipitia ili kufikia kwenye ajira, wapo waliobakishwa baada ya kumaliza mafunzo yao, wapo walio-apply baada ya tangazo kwenye gazeti, website na mitandao ya kijamii. Wapo walioenda na bahasha zao maofisini na kuukwaa. Wapo walioshikwa mkono, wengine labda walitumia namna ambazo ni kosa kisheria, yote heri!

Nianze mimi ajira yangu ya kwanza niliipata kupitia rafiki yangu ambaye katika stori mbili tatu tulizopiga alinitaarifu kuna nafasi katika shirika analofanyia hivyo kama nipo interested ni-apply, basi nami bila hiyana kwa kuwa kipindi hicho ndiyo kwanza nilikuwa nimemaliza chuo, niliona hiyo siyo fursa ya kukosa, nili-apply na baada ya wiki mbili nilipokea simu ya kwenda kwenye usaili.

Watu walikua ni wengi hivyo waligawanywa mafungu matatu, fungu la kwanza Jumatatu, la pili Jumanne na la tatu Jumatano, kuna hivyo niliona hii siyo nafasi ya uhakika hivyo hata sikuwaambia nyumbani ili nikikosa nibaki na (aibu zangu).

Haya siku ya interview ilifika interview ilikua mnaanza in groups kwenye panel halafu baadaye ni one on one na interviewer watatu; nilijibu maswali yote kwa kujiamini japo majibu mengine nilikuwa na tunga tu. Namshkuru Mungu baada ya wiki moja kama na nusu hivi, nilipokea simu kuwa nimefanikiwa ku-pass interview na nilitakiwa ku-report kazini Jumatatu inayofuata.

Baada ya mkataba wa kazi kuisha, nilipata interniship na kampuni moja kubwa sana, nilipiga kazi as if sio intern hata baadhi ya wafanyakazi wa pale hawakujua kama nipo kwenye intrniship, basi baada ya miezi miwili Branch Manager alinitaarifu kuna nafasi ipo wazi kama unaweza nifanye, the good thing ni kwamba kitengo chenyewe ndiyo hichohicho nilikua nafanyia internship so haikua kazi for the transition, hivyo ndivyo nilivyojipatia hii kazi na namshukuru Mungu maisha yanaenda.

That's my story!

Funguka uliipataje kazi unayofanya au uliowahi kufanya? Uzoefu wako ni muhimu kwani siku zote wanasema experience is a good teacher. Na tunaweza kujifunza jambo kwenye uzoefu wako!

vvm
 
Nakumbuka ilikua kipindi cha kwenda field, kuna mwalimu wangu wa chuo alinichunuku sana akaniunganisha na kweli nikapokelewa field nikafanya kwa wiki tatu tu, nakumbuka nikatakiwa kurud chuo kulikuwa na pepa, nikawaaga kuwa narudi chuo.

Baada ya kumaliza mwalimu yuleyule alinipeleka ofisi moja tukashindwana kwenye malipo nikampigia nikamwambia kilichojiri akaniambia, "usichoke. Una wazo gani?" nikamwambia nataka kwenda kujaribu kuomba kule nilikokua nafanya field akanambia wazo zuri utakapofikia utanambia kweli nikaenda onana na mkurugenzi kupitia jina la huyo mwalimu nikakubaliwa nikawa hapo.
 
Nakumbuka ilikua kipindi cha kwenda field, kuna mwalim wangu wa chuo alinichunuku sana akaniunganisha, kweli nikapokelewa field nikafanya kwa wiki tatu tu nakumbuka nikatakiwa kurudi chuo kulikua na pepa nikawaaga kua narudi chuo baada ya kumaliza mwalim yule yule alinipeleka ofisi moja tukashindwana kwenye malipo nikampigia nikamwambia kilichojiri akanambia usichoke una wazo gan nikamwambia nataka kwenda kujaribu kuomba kule nilikokua nafanya field akanambia wazo zuri utakapofikia utanambia kweli nikaenda onana na mkurugenzi kupitia jina la huyo mwalim nikakubaliwa nikawa hapo
Safi Madame S story yako imezidi kuniaminisha kwenye hizi harakati watu ni mtaji!
 
Nakumbuka ilikua kipindi cha kwenda field, kuna mwalim wangu wa chuo alinichunuku sana akaniunganisha, kweli nikapokelewa field nikafanya kwa wiki tatu tu nakumbuka nikatakiwa kurudi chuo kulikua na pepa nikawaaga kua narudi chuo baada ya kumaliza mwalim yule yule alinipeleka ofisi moja tukashindwana kwenye malipo nikampigia nikamwambia kilichojiri akanambia usichoke una wazo gan nikamwambia nataka kwenda kujaribu kuomba kule nilikokua nafanya field akanambia wazo zuri utakapofikia utanambia kweli nikaenda onana na mkurugenzi kupitia jina la huyo mwalim nikakubaliwa nikawa hapo
huyu "mwalimu" mbona anajiongeza sana
 
Huyo mwalimu alikuwa jinsia gani?
 
Afadhali kwa mara ya pili...

Maana hii dunia hivi sasa ina watu na viatu
Yeah dunia imebadilika nakumbuka niliwah kwenda kwake mara moja tu na yote alikua na mtoto wake pasua kichwa sana bas akawa ananiomba nijaribu kua nae karib niwe namsemea semea nikakubali kulipa fadhila lakini haikusaidia mana binti tayar alishaharibika alikuja pata ajali arusha akiwa na mume wa mtu, akavunjika miguu na mume wa mtu alifariki ndio alipopata fundisho sasa hivi sjui yuko wapi
 
Sasa kwanini ulienda mara moja "tu" kwa mtu aliyekufanyia wema? Huna fadhila?
 
Yaani s kwamba sina fadhila isipokua tulikua tukiwasiliana kwa sim na mara nyingi anakua chuo akitoka kufundisha anakua ofisin kwake weekend ana mahali ana fundisha me jumamos kwa wakat huo nilikua naenda kazini so off yangu ilikua sunday muda ulikua unanibana sana na pia nilikua natoka late so yeye hua muda anaotoka sometimes ananipitia kunijulia hali na mengineyo hiyo kwenda kwake ni kwa ajili ya bint yake mana siku hiyo alimwambia usitoke ntakuja na mgeni ikabidi niondoe muhali tukaenda
 
Basi sawa... usiache kumbukumbuka hata kama binti yake hayupo tena. Hakika utabarikiwa wewe na vizazi vyako vyote
 
Back
Top Bottom