vvm
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 6,303
- 10,334
Habari wadau,
Huu ni uzi spesheli kwa waliowahi au walioajiriwa, kwa wale wataalamu wakujiajiri hapa siyo sehemu sahihi.
Kuna njia mbalimbali ambazo watu huzipitia ili kufikia kwenye ajira, wapo waliobakishwa baada ya kumaliza mafunzo yao, wapo walio-apply baada ya tangazo kwenye gazeti, website na mitandao ya kijamii. Wapo walioenda na bahasha zao maofisini na kuukwaa. Wapo walioshikwa mkono, wengine labda walitumia namna ambazo ni kosa kisheria, yote heri!
Nianze mimi ajira yangu ya kwanza niliipata kupitia rafiki yangu ambaye katika stori mbili tatu tulizopiga alinitaarifu kuna nafasi katika shirika analofanyia hivyo kama nipo interested ni-apply, basi nami bila hiyana kwa kuwa kipindi hicho ndiyo kwanza nilikuwa nimemaliza chuo, niliona hiyo siyo fursa ya kukosa, nili-apply na baada ya wiki mbili nilipokea simu ya kwenda kwenye usaili.
Watu walikua ni wengi hivyo waligawanywa mafungu matatu, fungu la kwanza Jumatatu, la pili Jumanne na la tatu Jumatano, kuna hivyo niliona hii siyo nafasi ya uhakika hivyo hata sikuwaambia nyumbani ili nikikosa nibaki na (aibu zangu).
Haya siku ya interview ilifika interview ilikua mnaanza in groups kwenye panel halafu baadaye ni one on one na interviewer watatu; nilijibu maswali yote kwa kujiamini japo majibu mengine nilikuwa na tunga tu. Namshkuru Mungu baada ya wiki moja kama na nusu hivi, nilipokea simu kuwa nimefanikiwa ku-pass interview na nilitakiwa ku-report kazini Jumatatu inayofuata.
Baada ya mkataba wa kazi kuisha, nilipata interniship na kampuni moja kubwa sana, nilipiga kazi as if sio intern hata baadhi ya wafanyakazi wa pale hawakujua kama nipo kwenye intrniship, basi baada ya miezi miwili Branch Manager alinitaarifu kuna nafasi ipo wazi kama unaweza nifanye, the good thing ni kwamba kitengo chenyewe ndiyo hichohicho nilikua nafanyia internship so haikua kazi for the transition, hivyo ndivyo nilivyojipatia hii kazi na namshukuru Mungu maisha yanaenda.
That's my story!
Funguka uliipataje kazi unayofanya au uliowahi kufanya? Uzoefu wako ni muhimu kwani siku zote wanasema experience is a good teacher. Na tunaweza kujifunza jambo kwenye uzoefu wako!