trigeminal
JF-Expert Member
- Jan 9, 2015
- 1,920
- 2,197
Nimeipenda hii, kweli maisha mihangaikoHadi sasa hivi nimeshafanya kazi sehemu nne.
1.Dar es Salaam.
Nilikua nimemaliza internship,nafasi za serikali hazijatoka wala nini, niko tu kitaani napiga daywaka za vijiweni za kuunga unga hapa na pale, ali mradi nisile wali mkavu. Kuna chuo fulani hivi wakawa wametoa tangazo wanataka Tutorial Assistants,nikatupia application yangu, mimi na mshikaji wangu wa karibu sana, tukaitwa interview wote wawili. Siku ya interview tumeenda pale chuoni,tunacheki majengo ya chuo yamechakaa kinyama,tunaulizana na mshikaji wangu,hawa wataweza kweli kutulipa mpunga wa kutosha? Tulifika pale mida ya saa tatu asubuhi, ila kuja kuingia kwenye interview mimi niliingia kama saa kumi na moja hivi jioni!! Nimechoka mbaya, na interview kiukweli haikwenda poa, nilimbwela mbwela Sanaaa!! (kumbuka hii ndio ilikua interview yangu ya kwanza kabisa tangu nimalize intern). Baada kama ya wiki moja hivi,nikapigiwa simu kwamba nimefaulu interview, niripoti hapo chuoni kwa ajili ya kusaini mkataba na kuanza kazi!! Mimi na mshikaji wangu wote tulipata;Ila sasa mshikaji wangu yeye akawa amepata nafasi pia Bugando Hospitali (yuko hapo hadi sasa), so akapiga chini kule, kwa vile mimi nilikua sina option,nikatimba, nikasaini mkataba (permanent and pensionable), nikaanza kazi rasmi. Salary haikua mbaya sana (ukizingatia ndio ilikua my first salary apart from zile posho za internship).
Tatizo la pale bwana:kwanza ilikua unakuja asubuhi, unakaa tuu ofisini hamna lolote unalofanya, hamna cha kufundisha, au kuelekezwa au chochote, unakaa tuu unacheza na laptop hadi mda wa kazi ukiisha unarudi home (chuo kilikua kimepata matatizo kidogo,so walizuiliwa kudahili na NACTE wanafunzi wa first year,ambao mimi ndo kuna somo ilibidi niwe nawafundisha). Tatizo lingine ikawa wanachelewesha mishahara balaa. Miezi mingine hadi tarehe 10 ndo kitu kinasoma!! Nilikaa pale miezi mitatu tuu, nikaona hapa nimeingia cha kike!! Nikasepa.
2.Arusha.
A small NGO fulani hivi ya Waingereza ambao wanajihusisha na projects mbalimbali za afya,elimu,biashara. Kama kawaida, niliona tu nafasi kwenye zoom, nikatupia application, nikaitwa interview nikaenda, after a week nikapigiwa simu nikaripoti kazini.
Hapa nilianza kazi kwa salary ambayo ni ndogo kuliko hata kazi ya kufundisha niliyoacha. Sema huku apart from salary,kulikua na viallowance vya hapa na pale vingi, pamoja na pesa za dili za hapa na pale.
Tatizo la hapa likawa country director wa Tanzania alikua na matatizo matatizo sana...!! Alikua anaendesha ile NGO kama kampuni ya kwake binafsi. Kelele nyingiiii, micro-management kwa sanaaa!!! I stayed with this organization for 5 months tuu, nikasepa.
3.Mbeya
Hii ilikua ni kliniki kwa ajili ya watoto, ambayo iko funded na International NGO moja ya Wamarekani. Na yenyewe niliona tangazo kwa gazeti, nika apply, nikaitwa interview, nikapanda basi from Arusha hadi Mbeya (the longest journey by bus i have ever experienced), tuliingia mbeya saa saba na nusu usiku, saa mbili asubuhi nikagonga interview, ilienda vizuri sana (i was very very confidence by this time nilikua nimezoea interviews tayari, na nimejiandaa kweli kweli, na nikaulizwa maswali yale yale kama bahati ya mtende). After two weeks, nikapigiwa simu nimefaulu interview niende Mbeya kuanza kazi. Hii kazi kwa kweli benefits zake zilikua nzuri mno compared na kazi zangu zilizopita. I stayed at this organization for 1yr and 4months, then I left. Sababu zilikua mbili tatu; Kwanza, kulikua hakuna uhakika wa funds za kuendeleza mradi kutoka kwa wamarekani kwa mwaka unaofuata (though walikuja kupata wakaendelea), lakini pia management ya hii organization ya hapa bongo walikua very discouraging kwa wafanyakazi, na wanadharau wafanyakazi.
4.Mbeya
Mradi mkubwa dealing with HIV/AIDS in the Southern Highlands zone. Na yenyewe niliona tangazo, nika apply, nikaitwa kwa interview, nikatusua. (sio kirahisi hivyo,hii ilikua mara ya pili kuitwa interview hii organization,na mara ya kwanza nilidunda). It has been 1 yr 9 months now, and still counting, and i can confidently say that this has been my dream job!!
N.B.
1.Hapa nimeandika kirahisi sana kwa kujumuisha zile interviews nilizofanikiwa tuu, but safari hii haijawahi kuwa rahisi kwangu, nitafungua uzi wa kuelezea my failures katika interviews kadhaa ambazo nimewahi kufanya na nikadunda, ili kuwatia moyo vijana wanaotafuta ajira sasa hivi wakomae na wasikate tamaa!!!
2.Katika kazi zote ambazo nimewahi kuzifanya kama nilivyoeleza hapo juu, Sijawahi hata mara moja kupata kazi kwa sababu ya kufahamiana na mtu fulani kwenye hiyo organization, au kupewa 'memo'. I was purely depending on applying for the jobs, na kuitwa kwenye interview panapo majaliwa, na kuonyesha uwezo wangu wakati wa interview!! Kwa hiyo pia vijana mnaotafuta, msikate tamaa kwamba hujuani na watu kwenye hayo ma organization, pambana kweli kweliz ipo siku utafanikiwa!!