kutega visoda relini treni ikivikanyaga vinanyooka kisha tunatengeneza nakamba
Si vyema suala la kutandika watoto viboko kulifanya kuwa ni la kurithisha toka kizazi hadi kizazi, lakini kusema kweli ni vigumu kwa wengi kuwa na saikolojia ya watoto kiasi cha kuweza kujua njia mbadala ya malezi. Hata baadhi ya nchi ambazo sasa zimeacha malezi kwa viboko zamani zilikuwa zinafanya hivyo na kuna misemo yao (mfano Spare the rod spoil the child) ambayo mpaka leo wahafidhina wanaikumbuka na wengine wanajuta kwa nini wameondosha bakora katika malezi.Do me a favour,ukipata muda shusha uzi maalum tujadili pros na cons za malezi haya ya bakora vs non bakora ( I for one i treat it as domestic violence)
ADI, afu nilipokua kua ka teen, ndo enzi hizo mabreka(b reak dance) yamapamba moto.
Usipoalikwa kwenye sherehe kuwa stage show unaenda kunywa sumu hapo late 80's.
I do remember the times I had my report form at hand (mind you I was a bright kid) the feeling that came in my mums eyes when she opened it and later the whole house went happy because of me, tunapikiwa chips and promises of going out. I think those are the very best moments when I think of my childhood.
I will never forget mchezo wa baba na mama, mi nlikua baba wakat mwingine mtoto yaani nikikumbuka nataman kurudi utoton ila basi umri umekwenda.
Yaani AD we acha tu! nikikumbuka utoto najidharau kwa kweli namshangaa huyu hapa chini anautaka ubaba wa utotoni, naona huu ubaba wa ukubwani mgumu!
Hahhaahha hahahaha,nitakupm unambie style ya kupanga mito unapolala na uwepo wa big shem lol!
Asa kuna kituko kingine bana hiki mpaka kesho huwa nikikumbuka nacheka sana,
Kwanza nilikuwa napenda sana kuvaa vitu vya mama,km viatu na nguo,
Siku ya siku nakumbuka padri wetu alikuja hm,
Mie nikuwa nimelala na baba chumban asa mama akaja kumwamsha baba padri kaja baba alipotoka tu na mie nikashuka kitandan kulikuwa na tenga flan la kuwekea ngu chafu nikazana na kuibuka na brazia ya mama nikajitupia na kutoka seblen nikaenda kusimama katikati ya sebule watu walichanganyikiwa nakumbuka mama alikurupuka na kuja kuninyakua km mwewe anavonyakuwa kifaranga yani nilisabababisha b onge la aibu aisee!!!
- Siku niliyokula pilipili kwa makusudi na kuenda kliniki nikidai nina homa. Dokta kunipima, nilikuwa na sijui madigrii mangapi. Hadithi ndefu lakini uongo ule ulinilazimu kulazwa hospitali wiki moja.
- Siku hizo vitabu na vifaa vyote tulipewa bure, tukimaliza mwaka tunarejesha na kupewa vyengine. Kumbe katika kitabu kimoja kulikuwa na barua aliyonijibu "mchumba wangu". Mwalimu aloikamata akatishia kumwambia baba yake ambaye alikuwa daktari wa meno. Siku ya pili daktari alikuja shule (kumbe kwa ukaguzi wa kawaida wa afya zetu) lakini mimi nilidhani ndio amekuja kunishikisha adabu. Sikuwa na raha muda wote mpaka alipoondoka. Badae mwalimu aliniita na kunionya nisizowee, kusoma kwanza mademu baadae.
- Pamoja na yote hayo walimu waikuwa wananipenda kwani nilikuwa hodari. Sikusoma darasa la 2 nikapelekwa la 3, sikusoma la 4 nikapelekwa la 5 na sikusoma la 6 nikapelekwa la saba. Nilikuwa ninafurahia zawadi za mwanafunzi bora.
Hehehehe.......... Mwalimu mkuu, usiniulize jinsia yake tafazali.....
Jamani.... another post on a wonderful Mom.... inanifanya nitafakari if I am doing the same thing for my son.... Kwamba na yeye siku moja somewhere ambako hamna anae nifahamu atasimulia haya mnayo simulia hapa. I guarantee you huko your mom would be very proud if she reads this post..... Thank you for sharing Gamba chovu..... be good to all the women basi in courtesy of your mama.... Pamoja saana.
Hiyo red ya juu maelezo yake yako "faraghani".I wish I knew you right now ili nirelate story ulotoa na what you are, what you do, na what you portray...
Na I think walimu wako understood you, ndio maana walikua nakupenda... Kwa kweli naomba nitoe pongezi... kuruka madarasa hivo, ulimaliza primary upo darasa la ngapi? Na have you got any kid ambae amefuata intelligence zako ki hivo? Jibu if only you don't mind... Thank you for sharing....
Zipo nyingi ila hii inaniumiza hadi leo. Tulikua kampan ya watoto sita na mimi nlkua fundi mzuri sana wa kutengeneza magari ya mabati ya kuvuta na kamba, sasa tukawa tunaua mijusi tukawa tunaitengenezea majeneza ya gamba la mgomba tunapakia kwenye hayo magar nlyokua natengeneza tunasafirisha hadi shambani kwa mmoja wetu tunazika na tulkua tunafanya kama msiba wakweli na tukafanya hvyo mara nyingi na hatukuwah kuzika shamba tofauti na hilo mara zote, kilichokuja kutokea kwenye hiyo familia ndo kinanfanya nkumbuke kwa uchungu tukio hili hadi leo japo ilkua utoto, familia karibu yote imetetekea akiwapo tuliekua tunachezanae wa hiyo familia tulikua tunaenda kuzika mijusi kwao naye akishiriki bila kujua tunaichulia familia yao, ilikua miaka kati ya 92 na 95. INANIUMA SANA JAPO SINA UHAKIKA UHUSIANO WA MISIBA YA KWAO NA UTUNDU WETU.