What is your Big WHY in LIFE (Life Investment Finance and Entrepreneurship)?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,470
5,462
Habari ya siku ya leo;
Ni muda mrefu tangu nilipoandika makala yangu ya mwisho katika jukwaa hili ambalo nimelichagua kama sehemu ya mchango wangu kwa jamii yetu.Ninaamini kwamba pamoja na kwamba maandiko na maoni yangu hayana upekee wala ukoo wowote ila kwa kuwa ninatumia rasilimali muda na maarifa katika kuyaandaa basi yanaweza kuwa na uvuvio ambao unaweza kumpa mtu mtazamo mpya na kumtia moyo katika lile analolifanya.

Leo nimeleta mada chokonozi ambayo nimeileta kwa muundo wa swali ambalo mimi huwa pia ninajiuliza.Swali Lenyewe kwa kiswahili ni NINI lengo lako kuu la KUISHI(MAISHA) ambalo kwa kiingereza nitauliza What is Your BIG WHY in LIFE ambapo LIFE inawakilisha maneno Life, Investment,Finance and Entrepreneurship.

Ninaileta mada hii kama mjadala ambao unalenga kuwapatia uongozi wa namna BORA ya kutambua na kushughulika na BIG WHY yako katika LIFE

Kama nilivosema L katika neno LIFE inasimama badala ya Life yaani Maisha.Na katika eneo hili Big Why yako inapaswa kuwa na maisha yenye AFYA na FURAHA ambayo katika kigezo cha msingi yanausisha kuishi katika mazingira mazuri,kutunza afya yako,kupumzika,kufurahia n.k.

Swali la kujiuliza ni JE katika Maisha yangu ninachukua hatua gani kuhakikisha ninakuwa na AFYA,FURAHA,AMANI na UTULIVU.BIG Y yako itakupa jibu la kwani UWEZA Afya Njema,Uwe na Furaha na Uwe na Amani na UTULIVU.Ukishaona umuhimu wake basi ujiulize iwapo hali yako ya sasa na maamuzi unayofanya yanachangia kukufanya uwe na afya njema,Furaha na Amani kwa mfano katika mtindo wako wa maisha,lishe,mahusiano n.k. Je yanalinda Afya na FURAHA yako au yanachangi kuiondosha afya na furaha yako?

Eneo la Pili katika LIFE ni herufi I ambayo inasimama badala ya neno INVESTMENT Je unafanya aina gani ya uwekezaji katika maisha yako?Je unajiongozi maarifa na ujuzi,Je unatengeneza connection ya watu na marafiki wneye TIJA?Je unanunua Rasilimali zinazoongozeka thamani?Je unaweka Akiba,Je unakuwa na BIMA?Je unalinda mahusiano na wengine kwa kuwa mwaminifu katika biashara na maisha.Je unatenda wema na ukarimu kwa wengine ila Uweze pia kupata fadhila?Je unakuwa na moyo wa shukrani na kuheshimu watu wote bila kujali hali zao?Uwekezaji unaweza kuwa katika Fedha au katika WEMA na Fadhila kwa wengine.Hata kuwapa watu ushauri pale wanapohitaji ni mbegu njema inayopandwa.Kuwasaidia wengine katika magumu na kuwaheshimu wengine ni mbegu ya wema ni INVESTMENT ambayo itakusaidia wewe baadae au hata watu wako wa karibu.

Herufi ya Tatu katika neno LIFE ni F ambayo ni Financial Freedom ama UHURU wa FEDHA.Uhuru wa fedha hautokani na kuwa na PESA nyingi au vyanzo vingi vya mapato tu.Uhuru wa Fedha ni matokeo ya kuwa Uhuru wa kutafuta na kutumia kipato chako na kutosheka nacho.Unaweza kuwa na uhuru wa kifedha bila kuwa na PESA nyingi kama ELON MUSK na unaweza ukawa na PESA nyingi zaidi ya ELON MUSK lakini usiwe na UHURU wa KIFEDHA.Yote hii inategemea na nidhamu na mahitaji yako.Kadiri unavokuwa na nidhamu kubwa ya fedha na mahitaji machache binafsi ndivyo unavokuwa na UHURU wa KIFEDHA zaidi.Epuka kuishi maisha ya maigizo na mashindano na watu pamoja na majigambo yasiyokuwa na msingi.


Herufi ya Mwisho katika neno LIFE ni Entrepreneurship.Entrepreneur ni mtu anayeamua kufanya jambo la kuleta mabadiliko(Innovation) katika jamii.Katika maisha yako jitahidi kuwa na UJASIRI wa kuwa MJASIRIAMALI kwa kadiri ya KARAMA zako.USikubali karama zako zipotee BURE kwa sababu ya uoga,wasiwasi na kuogopa kushindwa au kukosea.Kumbuka Kuogopa Kushindwa ndio Kushindwa.Kuogopa kukosea ndio Kukosea.

Nimeleta mada hii kama mjadala ili sote kwa pamoja tujadili namna ambavyo tunashughulika na BIG Y yetu katika maisha yetu.

LETS LIVE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom