What is Wrong with Tanzania?!. Tunashindwa Nini Kufikisha Bidhaa Zetu Kwenye Masoko ya Kimataifa?!.

Huwa siedit comment ya mtu
886fe927c04eda8617ccc4d3b1ddccc4.jpg
 
Kutokana na malezi yetu enzi za ujamaa mindset ya kitanzania ni kuzuia. Miaka zaidi ya ishirini toka tuingia kwenye uchumi wa soko bado hili halijabadilika. Mwenzetu Kenya mfumo wa soko wanauelewa na kuutumia vilivyo. Wamejiweka vizuri kitaasisi na wanajulikana kimataifa. Hawana vikwazo kama tunavyokumbana navyo sisi. Pia elimu ni muhimu. Kwa elimu yetu hii ya kuokoteza siyo rahisi kuingia kwenye masoko ya kimataifa.
 
Inawezekana ccm wabovu lkn mbadala wa ccm bado hakuna kwa sab waliokuwepo ni wabovu kuliko ccm. Kwa mfano mamvi ndiye ataleta madiliko? Anayetaka urais ili amkomeshe kikwete? Mtu aliyethibitishwa kuwa ni fisadi na chombo chenye mamlaka kikatiba? Au chadema chama cha kifamilia? Au cuf chama chenye makundi? Tanzania upinzani wenye uwezo wa kutawala nchi bado haujatokea.
Wewe ndiyo unawasamea Watanzania? Leta katika mpya nzuri na Tume huru tuwaachie WaTz wazungumze.
 
Ninaamini maneno ya Mfalme Selemani kuwa kila kitu kina wakati wake chini ya jua! Na ninaamini huu ni wakati wa watanzania, tutapanda sana katika kila sector ya biashara! I do believe!
Kuna myahudi mfanya biashara alinifundisha kuwa ukitaka kufanya jambo lazima ujiamini wewe mwenyewe na utashangaa kila kitu kina unfold by itself, usiwe negative hata kidogo!
 
Wewe ndiyo unawasamea Watanzania? Leta katika mpya nzuri na Tume huru tuwaachie WaTz wazungumze.
Siwasemei bali dalili zinaonekana kwa mtu yeyote. Kwani mamvi sio fisadi aliyethibitishwa? Chadema sio chama cha mtei na mkwe wake? Cuf haina migogoro? Tume mbona ni huru ? Zambia Malawi na Kenya vyama vya upinzani vimechukua nchi kupitia tume kama hii acheni visingizio.
 
Tanzania ni gharama sana kufanya uzalishaji wa bidhaaa. Kwanza VAT 18% inapigwa kwenye bidhaa bila kujali una export kwa hiyo ukipeleka nje unapigwa tena VAT.

Bei ya Umeme ni ghali sana ukilinganisha na kwingine hivyo uzalishaji ni ghali

Regulation za ajabu ajabu na agency za Serekali zinazofanya kazi moja. TBS, TFDA, TRA, NEMC, OSHA bado Manispaa na wengine wengi na wote wanakuja kwenye kiwanda chako bila taarifa unasimamisha kazi kuwasikiliza.

Ukinunua Mahindi Tanzania ukayasafirisha hadi Kampala ukasaga ukapack ukarudisha kuuza Tanzania yatakuwa nafuu kuliko ukisaga hapa na kuuza hapa hill limefanya watu wengi kuhamisha viwanda
 
Having a great product sio tatizo,,, A great product is backed by several professionals (sales, marketing, business systems, management n.k) Mkitaka muuze nendeni mkarekebishe mengine hayo, product tayar mnazo
 
Inawezekana ccm wabovu lkn mbadala wa ccm bado hakuna kwa sab waliokuwepo ni wabovu kuliko ccm. Kwa mfano mamvi ndiye ataleta madiliko? Anayetaka urais ili amkomeshe kikwete? Mtu aliyethibitishwa kuwa ni fisadi na chombo chenye mamlaka kikatiba? Au chadema chama cha kifamilia? Au cuf chama chenye makundi? Tanzania upinzani wenye uwezo wa kutawala nchi bado haujatokea.
Chikundi,

Unachotaka kuwaaminisha wana JF ni kuwa mtu akiwa ccm, basi regardless yeye ni Bashite type or what , tayari anafaa kuongoza nchi . .? !

Ni lini hao wa vyama mbadala wamepata madaraka ya nchi wakashindwa kazi . . ?!
Ushahidi upo wazi, na ndio maana Paskal ameanzisha mjadala hapa, CCM wameshindwa ku support sekta binafsi kwa ujumla, wachilia mbali kufanya EXPORT . .
Sababu ntazitoa chache . . ,

1. Tanzania kisiasa, tangu tupate Uhuru . . , biashara kwa ujumla haikuwa ni jambo lililokuwa na Sera wezeshi na rafiki kwa watanzania . . Biashara zote zilikuwa zinafanywa na SERIKALI. Mashirika ya UMMA , RTC, BET, BIT, wahindi na wageni, BODI ZA MAZAO, VYAMA VYA USHIRIKA ndio waliokuwa exporters . . Mtanzania (mzawa) alipata taabu sana kufanya biashara nchi hii, nao waliitwa walanguzi tuu . .

2. Tanzania, na hasa ccm, walipoamua kukubali nchi iwe ya vyama vingi . . , bado wakaendelea kungangania Sera zao zilezile za UJAMAA . . , ila kwa HILA wao wakaanza kupora mali za UMMA kwa kisingizio cha UBINAFSISHAJI . .
Kwa sababu ccm walituingiza ktk siasa za kibiashara/kibepari kwa hila, ni wao tuu, viongozi wachache ndio waliokuwa na uelewa wa kuchangamkia fursa za biashara/export . . Walifanya hivyo wakishirikiana na watanzania wenye asili ya ki Asia na wageni wachache . .

3. SIASA ni sababu nyingine inayorudisha nyuma sana watanzania kufanya exports . .
Hata baada ya miaka zaidi ya 50 ya kujitawala, eti mtanzania hawezi kuuza mahindi yake kwa uhuru kabisa hata hapo Kenya tuu . . Kila exports ina cumbersome restrictions, ucheweleshaji wa documents processing for exports na mengi tu ya hovyo . .

Paskali, tatizo ni la CCM by 80% . . , ndio maana ni ngumu kufanya exports nchi hii . .
 
Siwasemei bali dalili zinaonekana kwa mtu yeyote. Kwani mamvi sio fisadi aliyethibitishwa? Chadema sio chama cha mtei na mkwe wake? Cuf haina migogoro? Tume mbona ni huru ? Zambia Malawi na Kenya vyama vya upinzani vimechukua nchi kupitia tume kama hii acheni visingizio.
Wewe Chikundi hebu acha kujiabisha kwa hoja za kijinga, unawaharibia CCM zaidi . . , kama huwezi kujadili kacheze mdako . .
 
Back
Top Bottom