What is wrong here | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What is wrong here

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 4X4byfar, Jan 4, 2009.

 1. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za leo wapendwa,

  Jamani naombeni kuuliza, hivi ni kwa nini my hubby akienda kwenye vikao na wenzake ni mpaka nipige simu mara ishirini ndo unamuona anarudi home. Nisipofanya hivyo anaweza kuja saa nane au hata asubuhi. Nikimuuliza nini hasa ni tatizo, hana la kujibu zaidi ya kusema samahani. Then next time the same thing tena anarudia! Je hii nini naombeni munisaaidie maana nakereka sana na hii tabia yake. Nimeanza kupata na wasiwasi if our marriage will work out yani!
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  your new year resolution:

  ...next time kabla hajatoka kwenda 'vikaoni', nawe jiandae, jipodoe na uvae kihasara hasara... akikuuliza unaenda wapi, mwambie "nipo tu!"

  ...huyo hata akitoka atajibanza mtaa wa pili kuchungulia, au huko aendako baada ya dakika tano atarudi kuchunga mzigo wake.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Kama ana tabia hii kila siku iendayo kwa mungu, basi inabidi mkae chini mzungumze na wewe umwambie tabia hii ya kutoka kila siku mpaka usiku wa manane huipendi na samahani zake inaelekea si za kweli maana anakuomba samahani halafu kesho yake anarudia jambo lile lile alilokuombea samahani jana. Vinginevyo nendeni wote huko kwenye vikao ili mkaburudike wote.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,174
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mama. Your Hubby takes your love for granted. Ni mtu asiyethamini thamani ya mapenzi na haswa pale anapotambua anapendwa yeye. Dawa ni kumweleza kwa kina jinsi usivyoipenda tabia hiyo na vitabia vingine vyake vidogo vidogo baada ya hapo akitoka usimpigie simu mpaka arudi mwenyewe bila simu. Mzee anakugeuza kengele, mpaka kengele ikilia ndio ajue muda wa kurudi nyumbani.
  Baadhi ya wanaume wakijua wanapendwa, basi ndio wanadeka. Next time atakuja fanya funny things na ataomba msamaha, na kwa vile unapenda, utasamehe na kwa vile he takes you for granted, atarudia tena. By the way, vile vikao vimepungua, ua sasa ndio vimehamia huko?.
   
 5. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Probably anakatiza mitaa kuminimise all the nagging you drop on him the minute he walks in.
  Kwani we una matatizo gani mpaka aku-avoid? Unajua kupika au mambo ya housegirl? Una mambo ya muhimu kuongea nae au stori zako zipo zipo tu (nikimaanisha unachemsha ubongo wake positively au story zako za kiuswahili swahili tu)? Mlioana kwa mapenzi au basi tu? Uling'ang'aniza hiyo ndoa kwa kumtega? Mmeoana kwa muda gani?
  Sijaoa, ila kutokana na majibu utakayotoa twaweza kufikiria kama yeye (God forbid) as a man.
   
 6. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  It sounds like a mere joke lakini kabla hata hujachukua hatua za kumkalisha chini uongee nae, fanya hii uone ata-respond namna gani. Then utaangalia uendelee kuongea nae au uchukue plan B
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Japo huu ushauri utakuumiza kwa muda fulani. Lakini kujua kama anakupenda na anafanya hayo kwa makusudi fanya haya, akitoka usilale mpaka arudi,vuta kiti kaa karibu na mlango, akigonga tuu fungua, na usizime taa, ili ajue hujalala. Lazima atakuuliza mbona hujalala mpaka muda huo, mwambie sijisikii kulala mwenyewe, naona raha tukiwa wote. Ukirudia hivyo kila wakati utamuona anawahi rudi. Kama bado anakupenda. Akishindwa acha hiyo tabia ya kuchelewa rudi baada ya hilo, omba wazee (wajomba, shangazi nk) wa upande wake waongee naye, wazee ni dawa.
   
 8. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...I like this!!! Unajaribu sumu kwa kuonja kwa ulimi??? Mh!!! I doubt if it can work any way!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280

  Wanaume wengi hawajui kusema samahani! Kama una mwanaume anayeweza angalau kusema neno samahani elewa hiyo pekee ni bahati kubwa!Anaelekea kuwa ni mwanaume unayeweza kukaa na kuzungumza nae.

  Kuhusiana na hiyo tabia ya kuchelewa kurudi, je imeanza lini? Tangu mlipooana? Je unawafahamu hao marafiki anaokutana/kaa nao usiku?

  Naaamini suluhu bora zaidi itapatikana kwa mazungumzo (communication) kati yenu wawili. Unayo haki na wajibu wa kujua sehemu anapokuwa mumeo na watu anaokuwa nao katika hizo saa za usiku. Jaribu tena kutafakari maisha yenu na mwenendo wako pia (inawezekana wewe pia umebadilika ktk mambo fulani). Hii itakusaidia kujenga mategemeo (to build expectations) katika mazungumzo yenu.
   
 10. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilijarubi hiyo style ila haikufanya kazi. Maana nilishawahi kumwambia kwamba naenda town kutembea so akimalizana na vikao vyake aniambie kwa kweli ndo ikawa nampa mda wa kukaa zaidi.
   
 11. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio eti ni tabia ya kila siku, anafanya kazi pia. Ila most huwa during w/ends. Sipendi kumfatafata huko kwenye vikao maana naona kama namnyima uhuru wake.
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,118
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndo starehe moja iliyopo Tanzania, kukaa nyumbani panachosha, mwachie apate space yake mara moja moja.
   
 13. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndoa hazifanani dada yangu, kwahiyo acha ajaribu hiyo aliyopewa kwanza. Lakini inavyoonekana, ingawa hatujui ndoa yenu ina muda gani sasa, huyo bwana alianza kutingisha kuona kama imeisha. Wewe hukugundua kama anatingsha, ukakaa kimya mwisho akazoea sasa hatingishitena bali imekuwa starehe kwake. Kwa hiyo unachotakiwa ni kumwambia aache kutingisha, bado haijaisha. Nina maana unatakiwa kuwa serious na umuoneshe kuwa wewe bado unampenda na unathamini ndoa yenu, na kwamba kitendo anachokufanyia (kama wewe huna tatizo) kinahatarisha ndoa yenu. Na Kwa jinsi nionavyo mimi huyo bwana hana tatizo kubwa, kinachomsumbua ama ni ulevi tu au kuna kitu anakikimbia hapo nyumbani. Hivyo ukishindwa plan A hapo juu tafuta siku moja muombe mwende wote huko anakoenda. Kwasababu inaonekana bado anakuheshimu lazima atakubali, huko utajua ni kwanini anachelewa kurudi.Kuanzia hapo unaweza kutafuta nini cha kufanya. Jaribu kujenga tabia ya kumwomba utoke naye mara kwa mara, ni haki yako. Na wewe mwenyewe jaribu kuboresha life style yako, inawezekana kuna kitu kina "m-boa" anashindwa kukwambia tu ila anakupenda bado.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  This is perfectly natural behavior and it should be encouraged. The man is a hunter and he needs to prove his prowess with other men. A night out chasing young single girls is great stress relief and can foster a more peaceful and relaxing home. Remember, nothing can rekindle your relationship better than the man being away for a day or two (it's great time to clean the house too!) Just look at how emotional and happy he is when he returns to his stable home.

  The best thing to do when he returns home is for you to prepare hot water for him to take shower and then cook him a nice meal.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Mmmh...Kibs...ni wewe kweli huyu au kuna mtu kakuandikia?
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  It seems you don't have plan 'B' what I could advise you nenda kapime afya yako baada ya hapo uangalie kama bado unataka kuendelea kufurahia maisha yako hapo au 'raha ujipe mwenyewe'. Maisha ni matamu lakini ni mafupi sana, endapo tayari una mtoto/watoto basi ujue enzi za kubembeleza mapenzi kwa mume/mke zimekwisha, pigania kulea watoto kwani hiyo ndiyo kazi kubwa kuliko kazi zote.
   
 17. BrownEye

  BrownEye Member

  #17
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It has been tested and worked out for several people, Lakini mwanamke inabidi uwe mjanja sana maana vinginevyo mzee anaweza akakugeuzia kibao ukaonekana unabanjua pembeni pia.
   
 18. BrownEye

  BrownEye Member

  #18
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiona mume wako hana chembe ya kajiwiivu na wewe (ujue kuna mahari kashapata anapumzika huko) na hivyo hata ukimuaga unaondoka nyumbani hatakuuliza muda unaorudi wala unakokwenda. pia ukichelewa kurudi atakuwa kimya. Akifanya hivyo kwa zaidi ya mara mbili ujue hana shida sana na wewe, na wala si kwamba eti anakuamini sana. Anataka na wewe usimfuatilie nyendo zake full stop.
   
 19. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hii ni balaa kabisa hata kamba haifai pole dada
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mbona jibu jepesi tu, akirudi saa nane wee unarudi saa tisa. Akilala huko siku moja wee unarudi baada ya siku 2. Nina hakika atakuuliza mwenzangu kulikoni, mwambie ulikuwa na vikao na wenzako. Siamini kama mkuki kwa nguruwe ni mtamu kwa binadamu. Atashika adabu yake kama anakupenda.
   
Loading...