What is this? Naombeni mawaidha

KUNANI PALE TGA

Senior Member
Feb 6, 2009
138
7
habari zenu wakuu,
kuna rafiki wangu mmoja ndio amenielezea kisa chake na anaomba ushauri.
Yeye anampenda sana binti mmoja,wako pamoja kwa karibu mwaka sasa,lakini shida kubwa ni huyo mwanamke anamwambia sometimes kuwa hana feelings naye,na sometimes feelings kwake zina kuwa za nguvu sana.kwenye mwaka mmoja hiyo inatokea mara nyingi sana.wote wawili ni wanafunzi wa masters,na kwa sasa binti ame kwenda kwao nyumbani,kama kwa ajili ya mwezi,na wakiongea kwenye simu,binti ka mwambia kwa siku mbili zilizopita hana feelings,hajui kama anampenda au hapana.kusikia hivyo rafiki wangu akamwabia basi kama ni hivyo bora tuachane,mwanamke akamwabia sitaki,ukiniacha nitaku miss.rafiki yangu akakata simu,na baadaye mwanamke kaanza kumpigia na kumwabia anam miss sana,anaomba asiachwe.yaani mwanamke anam miss sana,lakini sometimes hana uhakika kama anampenda.
sasa rafiki wangu haelewi chakufanya...
anaomba msaada wa dhati kutatua tatizo hili.
ahasanteni.
 
Mapenzi gani haya...?, mbona yana harufu ya utoto utoto?\..How come watu wazima na waelewa, level ya Masters wanakuwa na ubabaishaji na mizaha ya hivyo?...Huyu msichana hana lolote, na inaonyesha ana mtu mwingine anaemsumbua, SO YUKO kwenye Dilemma!.Dawa ni kumpa nafasi ya mwisho(ultimatum), na baada ya hapo ni kumwachilia mbali!
 
...unajua kazi ya boya la kujiokolea? enhee, linalotafutwa wakati wa dhoruba bahari inapochafuka? naam, hilo hilo...

... jipe muda. Mwaka mmoja huenda kwako ni mwingi lakini kwa mwenzio bado bado kwanza.
 
Dawa ni kumpa nafasi ya mwisho(ultimatum), na baada ya hapo ni kumwachilia mbali!
Mkuu usiseme hivyo! Watu hapa bado tunamachungu ya kufanyiwa unyama kama huo! Roho inauma kinyama lkn jamaa tu kajichokea huyo ndio anahudumia mzigo kwa sasa! Same story as above! Its real!
 
, level ya Masters wanakuwa na ubabaishaji na mizaha ya hivyo?...

Je huyo mwanamke amekaa muda gani toka amalize bachela? Kama ameunganisha, basi bado ni mtoto ambaye anamawazo ya ndoto za Alinacha. Mawazo hayo ni ya kawaida kwa wanawake wa vyuo vikuu. Nadhani huyo kidume akate mawasiliano kwa muda bila taarifa then aangalie reaction itakuwaje au aamue kumchanganya na amonite reaction then aamue kama kuna mapenzi au la.
 
nakupenda sikupendi za kitoto hizo, anakupotezea muda, sepa kijana. utazeeka kungoja mtetea uanze kutaga, je ukichinjwa kabla ya kutaga?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom