Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 55,120
- 69,554
Wajameni naomba kuuliza hivi ina maana mapadre, wachungaji na masheikhs wetu hawaoni serious irregularities zinazoendelea katika demokrasia yetu? Na mbona wako kimya? hawakemei? hivi nani hajui kuwa NEC imemuweka Kikwete madarakani? Hivi unafiki utaendelea mpaka lini? Hivi ina maana Pengo haoni uovu unaondelea au sheikh Mkuu Mufti Shaaban Simba haoni jinsi demokrasia inavyobakwa au Askofu Malasula hana habari na jinsi majimbo yalivyochakachuliwa? hivi ina maana sisi ni mambumbu kutotambua sacrifies yiliyofanywa na viongozi wa dini Kenya kuleta mabadiliko hata KANU kutolewa madarakani? Hivi mpaka lini hawa viongozi wetu wa dini wataendelea kuwalamba miguu CCM? hivi kuna mahali kumeandikwa utawala ni wa CCM tu? Hivi hii amani ya ukandamizaji ni kwa matakwa ya nani haswa? imani inanitoka!