What is our National Ideology?Na kama Hakuna Nani anajukumu la Kuiunda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What is our National Ideology?Na kama Hakuna Nani anajukumu la Kuiunda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Apr 10, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wana JF naomba kujua kama mtanzania wa kizazi kipya, miaka ya nyuma Taifa la Tanzania lilikua na Ideology [Itikadi] ambayo kupitia mfumo wa chama kimoja Idelogy ya chama ndio ilikua Idelogy ya nchi. Lakini yapata miaka kumi na Tano Taifa liko ndani ya mfumo wa vyama vingi. Ndani ya mfumo wa chama kimoja itikadi ni UJAMAA NA KUJITEGEMEA.

  Lakini kama Taifa ndani ya mfumo wa vyama vingi ni LAZIMA NA SI HIARI Taifa kuwa na DIRA yaani ndio NGUZO, ambayo vyama vyote vinavyopigania Kugombea Madaraka ya kutawala kupitia sanduku la uchaguzi ni lazima kuijua hiyo ITIKADI na kuitetea bila kupindisha hata kama vyama vina mrengo tofauti kati ya chama kimoja dhidi ya kingine.

  Je ni sahihi kwa sasa kusema Tanzania ni nchi ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA, pamoja na kupitia mageuzi makubwa ya kiuchumi kutoka kwenye state control economy mpaka kwenye private sector economy.

  Itikadi ya Taifa ni dira na national Identity dhidi ya mataifa mengine,na inapaswa kufundishwa mashuleni, vyuoni, na hata kwenye vyombo vya habari kama radio,runinga nk.

  National Ideology ndio inayoshape patriotism kwa kutumia maelekezo na malengo ya umma.Kama Mtanzania napaswa kuijua na kuitetea popote pale haijalishi natokea chama gani, mkoa gani, wilaya gani ,kabila gani,bali sifa kuu ni kuwa raia wa Tanzania.

  Kama hakuna ITIKADI YA TAIFA [NATIONAL IDEOLOGY] tunaitaji kuwa na ITAKADI kabla ya kuwa na KATIBA MPYA.Ni muhimu kujua sisi tu taifa la namna gani kabla hatujaweka misingi mikuu [Katiba] ya kusimamia Taifa.Basi ni hakika kuwa Taifa lianaitaji Majadala wa kitaifa kuibua na kujadili aina ya gani ya ITIKADI TAIFA LETU LA TANZANIA linaitaji.

  Mimi binafsi sijui Taifa langu kwa hivi sasa limesimamia ITIKADI IPI? Ni ile ITIKADI ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA iliyoasisiwa na Mwl, Julius K Nyerere chini utawala wa mfumo wa chama kimoja ama ni ITIKADI ya Mfumo wa Kibepari, au ni ITIKADI ya mfumo wa soko uria [Grobalization] au ni mchanganyiko wa ITKADI zote au kuna aina mpya ambayo imepatikani kulingana na matakwa ya nyakati.


  Ningependa wadau tujadili ni aina hipi ya ITIKADI inayolifaha Taifa la Tanzania kulingana na zama, nyakati na mazingira yanayoizunguka jamii husika kwa sasa.Na ni kipindi kizuri jamii inakewenda kwenye kipindi cha mchakato wa ujenzi wa katiba mpya.MUNGU IBALIKI Tanzania na mungu ibariki Africa.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Ujamaa 50% ubepari 50%
   
Loading...