What is Christmas? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What is Christmas?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by UMBEEE, Dec 22, 2015.

 1. U

  UMBEEE Member

  #1
  Dec 22, 2015
  Joined: Mar 5, 2014
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mwenye ufahamu na neno Christmas naomba tuelimishwe na kwa nini tunasherekea tarehe 25 je ni kweli YESU Kristo alizaliwa hiyo tarehe?
   
 2. Wonderful

  Wonderful JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2015
  Joined: Apr 8, 2015
  Messages: 6,359
  Likes Received: 3,744
  Trophy Points: 280
  Si kweli........
   
 3. PNC 1

  PNC 1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2015
  Joined: Feb 3, 2015
  Messages: 7,291
  Likes Received: 10,047
  Trophy Points: 280
  KRISTU ndio nani huyu mtu mimi namjua YESU KRISTO ambaye alizaliwa 25 December na kuhusu CHRISTMAS maana yake KRISTO MASIA
   
 4. hydroxo

  hydroxo JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2015
  Joined: Oct 19, 2015
  Messages: 814
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 180
  Thibitisha kwa ushahidi usiokuwa na shaka kwamba yesu alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12 na si kuleta maneno yako tu kwani hata mimi naweza kusema alizaliwa tarehe 4 mwezi wa 2 je utakubali nisipotoa uthibitisho usiokuwa na shaka?
   
 5. m

  markbusega JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2015
  Joined: Oct 12, 2015
  Messages: 429
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Swali zuri, sioni haja ya krismas uanasherehekea birthday isiyo ya kweli
   
 6. B

  Balacuda JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2015
  Joined: Mar 8, 2013
  Messages: 1,060
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ukishajua kazaliwa siku gani itakusaidia kwenda mbinguni? Je wewe unadhani iwe siku gani
   
 7. QUIGLEY

  QUIGLEY JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2015
  Joined: May 23, 2015
  Messages: 22,294
  Likes Received: 67,901
  Trophy Points: 280
  Yesu hakuzaliwa december, kumbuka bikira alibeba mimba june
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Dec 22, 2015
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Hakuna Ajuaye kazaliwa lini, hii ni kumbukumbu tu ya kuzaliwa kwake na sio tarehe rasmi aliyozaliwa
   
 9. w

  wakimataifa. JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2015
  Joined: Jun 7, 2015
  Messages: 1,366
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  msibishane sana muulizeni gwajima yeye anaelewa kila kitu
   
 10. pakaywatek

  pakaywatek JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2015
  Joined: Dec 28, 2014
  Messages: 2,955
  Likes Received: 1,922
  Trophy Points: 280
  Hii ya kwako ni mpya.
   
 11. m

  mtoto wa maskini JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2015
  Joined: Jun 28, 2013
  Messages: 1,155
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Kila mwaka lazima mtu aulize hili swali dah haya bana
   
 12. rehan

  rehan Member

  #12
  Dec 22, 2015
  Joined: Nov 25, 2013
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Yesu hakuzaliwa december,biblia inatuambia ya kwamba Samaritan wa kuzaliwa kwake wawindaji walikuwa nje wanawinda,hebu jaribu december 25 uende Jerusalem uenda kuwinda kama hujapata cha mtema kuni
   
 13. rehan

  rehan Member

  #13
  Dec 22, 2015
  Joined: Nov 25, 2013
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Samahani badala ya Samaritan niliandika wakati
   
 14. JOSEPH LUHUSA

  JOSEPH LUHUSA Senior Member

  #14
  Dec 22, 2015
  Joined: Dec 5, 2015
  Messages: 153
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Kuna jambo tusilolijua vizuri sana. Taratibu jamani.
   
 15. mkadiriajimajenzi

  mkadiriajimajenzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2016
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 308
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Historia ya Krismasi  Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira ya baridi.

  Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.

  Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Desemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Desemba.  Wakristo wa kale

  Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristo wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea mwezi wa Desemba kwa kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus, ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136 AD, askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”. Hata hivyo, kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo, kawaida ya Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.

  Katika mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Desemba. Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis Invicti”, ‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika mwaka 320 M, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Desemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo.

  Mnamo mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika kwa tarehe 25 Desemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Desemba.

  Hata hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25 Desemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitambua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni. Huko Uingereza England, Oliver Cromwell alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka 1649 na 1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu.

  Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi) walipokimbia uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani. Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800. Na, weka akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo.  Krismasi inaanza kuwa maarufu

  Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na kitabu cha Washington Irving The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall ‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria, alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi Christmas tree na Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za Kumsifu Yesu za Krismasi Christmas Carols (ambapo aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza Kuu la Marekani US Congress lilikutana Siku ya Krismasi). Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mnamo mwaka 1860, mfananishi illustrator wa Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi Father Christmas. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.  Nakuombea Krismasi Njema Have a merry Christmas

  Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa Desemba ya 25, wakati wa solstice. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Desemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangano wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans – au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative – watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa,” wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku za hivi karibuni.

  Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi?  Mazoea ya Krismasi  Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa ya Baba Krismasi Santa.

  Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?

  Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi.  Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia?  Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):

  “Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4).

  Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa Tyutoniki Teutonic na Skandinavia Scandinavia wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998)  Je, Yesu Alizaliwa Desemba ya 25?

  Si tarehe ya Desemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka 530 C.E kwamba mtawa monk aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni Desemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Desemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani.

  Mapagani wa Kirumi walisherehekea Desemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.

  “Mnamo karne ya pili A.D, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo mingi” (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995).

  ‘Waungu’ wengine wakipagani waliozaliwa Desemba ya 25 ni: Hercules mtoto wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani wa Roma.

  Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus?  Kama viumbe visivyokuwa binaadamu aliens watafika duniani katika wakati wa Krismasi, bila ya shaka wataamini Krismasi kuwa ni sherehe ya kufurahikia kuzaliwa kwa Baba Krismasi Santa. Majina ya ‘Santa Claus’, hayamo popote ndani ya Biblia.

  Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus) alikuwa ni mtu halisi, askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada ya kifo chake mnamo Desemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka.

  Baadaye Malkia Victoria aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Desemba ya 6 kuwa ni Desemba ya 24 kuamkia Krismasi.  Je, Yesu au Wafuasi Wake Waliwahi Kusherehekea Krismasi?  Kama Yesu alimaanisha kwa wafuasi wake kusherehekea Krismasi, angeliifanyia kazi yeye mwenyewe na kujikusanya pamoja na wafuasi wake. Hakuna sehemu iliyotajwa ndani ya Biblia kwamba kuna mfuasi yeyote aliyewahi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kama Wakristo wanavyofanya leo.

  “Kanisa halikupatapo kuweka sikukuu kwa ajili ya sherehe za tukio la Krismasi hadi ilipofika karne ya 4” (Angalia: Encyclopedia ya Grolier)

  Hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi ambazo sasa zinahusisha viingilio vya sherehe, biashara, na matumizi yaliyochupa mpaka, ni utovu wa akili kwa mfananisho wowote wa imani.
   
 16. CleverKING

  CleverKING JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2016
  Joined: Apr 24, 2014
  Messages: 6,666
  Likes Received: 14,653
  Trophy Points: 280
  Ngoja waje wenyewe....
   
 17. Kibao

  Kibao JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2016
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 60
  Mambo mengi yametokea baada ya biblia kuandikwa. Hatuwezi kuyapuuza kwasababu hayakuandikwa kwenye biblia. Mfano ni usafiri wa ndege haukutajwa kwenye biblia. Biblia inataja usafiri wa punda. Je tuanze kudharau na kuhoji usafiri wa ndege kwasababu haujatajwa kwenye biblia???? Mfano mwingine kutengeneza CD za kwaya na kuuza haijazungumziwa kwenye biblia. Mbona mnatengeneza CD za kwaya na mnauza???

  Haya mambo ya dini yanahusu imani ya watu. Na kuhoji imani ya mtu ni uchokozi. Kila mtu ana haki ya kuamini dini aitakayo bora havunji sheria.
   
 18. chipaka.com

  chipaka.com JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2016
  Joined: Dec 5, 2015
  Messages: 2,325
  Likes Received: 880
  Trophy Points: 280
  Mungu tunakuomba utupe macho ya rohoni,
   
 19. Yiyu Sheping

  Yiyu Sheping JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2016
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 1,499
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Hivi upumbavu nao ni karama za mungu? Maana kuna wenye hii talanta.

  Na washawsha!
   
Loading...