Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,832
- 18,827
Sasa mkuu kwa Sababu Zanzibar na Mombasa zilikuwa chini ya Sultan kabla ya Wazungu kuja, Sultan angeweza kufanya negotiation na Waingereza kuwa walipowapa Uhuru 1963 wangemkabidhi Muarabu Zanzibar pamoja na MombasaSack natambua vyema kwamba sehemu yote ya pwani ilihodhiwa na waarabu wa Oman ila pia nataka utambue kuwa baada ya wazungu kuja Africa sehemu hiyo ya Zanzibar ikijumuisha Pemba ,Unguja na Mombasa ilimilikiwa na Waingereza na tena si baada ya kuporwa ila kwa makubaliano maalum yaliyofanyika huko jijini Berlin Germany
Heligoland Treaty ya 1890 kati ya Germany na Britain ndio iliratibu makubaliano ambapo Britain watakubali kuichukua Zanzibar na Pwani yote ila wakawaachia Germany Tanganyika pamoja na baadhi ya nchi za Africa kama Togo n.k.
Hivyo basi baada ya vita ya kwanza ya dunia na Germany kuporwa makoloni yake yote na mengi yakiwa chini ya usimamizi wa Uingereza haikuwepo namna ya kuifanya Mombasa tena iwe sehemu ya Tanganyika bali muingereza aliifanya iwe sehemu ya Kenya
Actually Sultan alikuwa na argument nzuri kushawishi Mombasa ikabidhiwe Zanzibar badala ya Kenya kwa Sababu, dola ya Zanzibar ilikuwepo miaka mingi kabla ya Kenya ku exist, na demographic na culture ya Zanzibar na Mombasa (Waarabu, Waswahili, Waislam) zimefanana sana kuliko Mombasa inavyofanana na Kenya ambayo Ni nchi ya Wakristo weusi