What does this picture say about Us the People?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928

Na hii hapa chini maeneo ya Msasani

Hapa ni njia ya kituo cha Polisi cha Msimbazi kama kinavyoonekana kwa mpiga picha. Nimepata picha hii toka kwa Evarist Chahali FB;

Ninajiuliza:
a. Uchafu huu ulianza kujirundika lini hapo? Ni wazi haikutokea siku moja ghafla bin vuup!
b. Ulipoanza kujirundika wahusika walikuwa wanafikiria nini? ni maua yanaota pembeni au mbolea?
c. Je kuna uwezekano wa wataalamu wa biolojia na viumbe hai kufanya utafiti kuona kama kuna jamii mpya ya viumbe hai imeanza kuishi humo na hivyo kutangaza eneo hilo kuwa ni hifadhi ya viumbe hai na kuwa ni "protected area"!?
d.Watu wanaoishi jirani na eneo hilo wanasubiri mwekezaji kutoka nchi gani kuja kuwasaidia kuwaonesha kuwa huo ni uchafu? au wanaamini "somebody's trash is someone's treasure"?
e. Inawezekana sisi ni taifa la watu waliozoea uchafu kiasi kwamba uwepo wake hautushtui tena kwani tumetengeneza some sort of immunity towards uchafu? Yaani hatuoni tatizo kupita na suti zetu, kupaki magari yetu na hata watoto kucheza mbele ya uchafu?
d. Do you see any similarity ya wananchi wa Tanzania na viongozi wabovu?
 
Huku ndio kufa kwa maadili, kila mtu anaangalia mwenzake kuwa ndio atalishughulikia hilo tatizo. Kama mwanakijiji alivyoandika, tangu linaanza hawakuona?. Ni kutegeana wakati madhara kuanzia harufu, usumbufu na maradhi watapata wanaoishi hapo na hata wanaopita.
 
Mkuu hiyo picha inasema tumeridhika na huo uchafu na ni tabia yetu kuwa wachafu ndio sababu kubwa mkuu wa kaya hachelewi kukimbilia nje ya nchi angalau huko kusafi kidogo.
 
Huku ndio kufa kwa maadili, kila mtu anaangalia mwenzake kuwa ndio atalishughulikia hilo tatizo. Kama mwanakijiji alivyoandika, tangu linaanza hawakuona?. Ni kutegeana wakati madhara kuanzia harufu, usumbufu na maradhi watapata wanaoishi hapo na hata wanaopita.

mfumwa inawezekana huo uchafu hautoi harufu au wenyewe wameuzoea kiasi kwamba hawasikii harafu?
 
Mzee Mwanakijiji hali ni mbaya sana sio hapo tu mitaa mingi ina hali ya uchafu wa kutisha.Watanzania inabidi tuamke kwani hii ni aibu.Charity begins at home.
 
...........Polisi wazima wanakaa na uchafu kama huo, mbona aibu!!
Ila si ajabu afya za polisi zenyewe mgogoro ndio maana wanaona sawa tu kukaa na uchafu kama huu.
 
msiniambie kuwa hakuna mtu anayefikiria kufanya kitu kama kampeni ya usafi hapo mtaani..
 
Mbona mnatushangaza jamani ?kumekuwapo na watu wanao nadia katika magazeti na mablogs mara kwa mara na kuwambia ulimwengu kuwa Jiji letu ni mmoja kati ya miji Tambarare ya Ulimwenguni sasa Utambarare umetokomea wapi ?
 
hahaha Babylon sasa hutaki?

16badyu.jpg

Huyo kwenye hilo jumba la bilioni 1.4 ukimwambia bongo siyo tambarare atakubali?
 
Mbona mnatushangaza jamani ?kumekuwapo na watu wanao nadia katika magazeti na mablogs mara kwa mara na kuwambia ulimwengu kuwa Jiji letu ni mmoja kati ya miji Tambarare ya Ulimwenguni sasa Utambarare umetokomea wapi ?

.........Bongo wala sio tambarare kivile, kuna baadhi ya sehemu ambazo ni chache kweli ni tambarare kama hiyo picha aliyoonyesha Mwanakijiji.
Lakini sehemu nyingi ni uozo mtupu.
 
Hakuna kipya hapo. Wengi wetu humu tumekulia ktk mazingira hayo. Tumekula chipsi mayai na chipsi dume zilizopikwa karibu na matakataka kibao. Halafu nzi wakija kufukuzia msosi wetu tulikuwa tunawapenga (swat) tu halafu hao tunaendelea kula.

Tumekula sana maembe ya pilipili yaliyokuwa yanauzwa nje shuleni. Tumekula sana mabungo na vitu vingine vingi tu ambavyo baadhi yetu leo tukiambiwa turudie hali ile tunaweza tukapoteza fahamu kabisa.

Kwa hiyo binafsi sishangai na sishangazwi kabisa na huo uchafu. Hii haina maana siuoni kuwa ni tatizo. La hasha. Ni kwamba tu hakuna jipya. Kama ilivyokuwa mwaka 1990 ni ndivyo ilivyo sasa 2010.

Na kama mnaona huo ni uchafu kupindukia basi hamjaona uchafu bado. Nendeni Lagos kwa Wanaija mkajionee. Kwa kifupi ni ndivyo tulivyo.
 
msiniambie kuwa hakuna mtu anayefikiria kufanya kitu kama kampeni ya usafi hapo mtaani..
Ndugu MMKJ nani afanye kampeni ya usafi ukiona siku kiongozi au mtu yeyote akifanya kampeni ujue kuna kitu anakitafuta sehemu hiyo kwanza atauliza kama kamera zipo hivi ITV watakuwepo ili aonekane akifagia kifupi hatuna hulka ya usafi wakati usafi wala hauhitaji fedha za kigeni

hapo msimbazi kuna familia za polisi na watoto zinaishi wao ndio wa kwanza kumwaga uchafu madirishani kituo cha polisi kipo around the corner polisi hajali anafikiri si kazi yake familia zinazotupa taka dirishani nazo zinasema si kazi yao kusafisha kuna jiji watakuja jiji nalo linasema si kazi yao kusafisha hadi majumbani tatizo linabaki pale pale watanzania tu wavivu tungependa hata kupata mtu wa kuflash choo baada ya kujisaidia
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom