Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Na hii hapa chini maeneo ya Msasani
Hapa ni njia ya kituo cha Polisi cha Msimbazi kama kinavyoonekana kwa mpiga picha. Nimepata picha hii toka kwa Evarist Chahali FB;
Ninajiuliza:
a. Uchafu huu ulianza kujirundika lini hapo? Ni wazi haikutokea siku moja ghafla bin vuup!
b. Ulipoanza kujirundika wahusika walikuwa wanafikiria nini? ni maua yanaota pembeni au mbolea?
c. Je kuna uwezekano wa wataalamu wa biolojia na viumbe hai kufanya utafiti kuona kama kuna jamii mpya ya viumbe hai imeanza kuishi humo na hivyo kutangaza eneo hilo kuwa ni hifadhi ya viumbe hai na kuwa ni "protected area"!?
d.Watu wanaoishi jirani na eneo hilo wanasubiri mwekezaji kutoka nchi gani kuja kuwasaidia kuwaonesha kuwa huo ni uchafu? au wanaamini "somebody's trash is someone's treasure"?
e. Inawezekana sisi ni taifa la watu waliozoea uchafu kiasi kwamba uwepo wake hautushtui tena kwani tumetengeneza some sort of immunity towards uchafu? Yaani hatuoni tatizo kupita na suti zetu, kupaki magari yetu na hata watoto kucheza mbele ya uchafu?
d. Do you see any similarity ya wananchi wa Tanzania na viongozi wabovu?