What do you have to say about TAMBALIZENI?

He know nothing, he is there as a trumpetor. Jamaa hajui lolote kuhusu issues, ndio wale watu wanaonsema ukichagua CCM kila kitu safi, hata kama ni jiwe linagombea kwa tikiti ya CCM wao wanaunga mkono tu.
 
Tumekosa ya kujadili, hili nalo ni topic, kweli tumeishiwa, yaani hata waimba ngonjera tunatakiwa kujadili du!!! kweli taifa lina matatizo kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja mpaka juu kabisa!
 
Kwa ya mara kwanza leo naungana na Kilitime kwamba kweli tumekosa ya kijadili . Kumjadili yule tumbotumbo ni sawa na sisi kuingia kumjadili Mtoto wa Bushoke,na mwimbaji wa wimbo wa presha sijui anaitwa nani yule dada tipwatipwa hali kadhalika Khadija Kopa na John Komba .Wao ni kula tu na njaa zao ndiyo mbele.Nadhani tuokoe muda hawa watu JK kuomba msaada na kupiga picha na G Bush na Pope ni sera tisha ya kuwafanya waseme CCM inapaa.
 
..wakuu!

..someni vizuri hiyo sentensi mtagundua hoja iliyotolewa...ambayo ni tafasiri ya msanii kuhusu safari ya kiongozi au usanii wa wasanii kutetea matendo yao!

..nadhani mmenipata hapo!
 
Ama kweli Nchi yangu ya tanzania .Leo nimemsikia Sheikh Yahya kupitia radio fulani ya kidini akimwaga sifa za ajabu kwa JK akisema amevunja record ya kutoa hotuba kwa masaa 3 bila ya kuchoka na ilikuwa kama chakula kwa kila mtu aliyekuwa akisikiliza maan walikaa kimya muda wote na kufurahia hotuba yake ambayo ni kama nguvu za muujiza ama Mungu. Kasema JK analinganishwa na Castro wa Cuba ila tofauti ni kwamba JK harudii maneno ya speech wakati castro hurudia . Akasema sifa ambazo ni zile zile walizo muimbia wakati anaomba kura .Tambalizeni hana tofauti na huyu pia
 
Ila huyu Tambalizeni huwa namkubali sana katika masuala mazima ya ushairi. jamaa siyo siri ana kipaji.

Ila kwa nini huwa hawamteui hata ubunge wa kuteuliwa?. au kazi yake maalum ni kuwatumbuiza NEC kupitia mashairi
 
lakini jamani kwani hapa tunamjadili huyu mtuu? (Mimi simjui nimejaribu kutafuta hata kwenye net simpati) kwani yeye ni nani? nielewesheni.


Mimi naona mtoa hoja hapa sio kumjadili huyu bwana/bibi Tambalizen bali ni hoja ambayo huyo bwana alitoa kuwa naomba ninukuu "Tambalizeni anasema JK anatafuta misaada Tanzania Inufaike.je ni kweli hii?"

Nadhani ni hilo je hiyo misaada ambayo inachangia 40% ya budget yetu ambayo JK anasafiri kila siku kuiomba inanufaisha Tanzania? Nadhani hii ndio hoja aliyotoa mtoa thread jamani.
 
Ndugu watz ni lazima tuamke. Kama tunataka Tanzania ipige hatua inabidi vyombo vinavyofanya maamuzi yanayohusu maslahi ya nchi yetu, iwe kwenye mihimili mitatu ya dola, iwe kwenye mhimili wa nne wa dola(civil society) au hata kwenye vyama vyote vya siasa na vyombo vyake vya maamuzi (vilivyo madarakani na visivyo madarakani, ni lazima kuwe na watu wenye uelewa wa dunia na mambo yanayohusu maslahi ya nchi. Mpaka leo mimi naona it is a joke kuwaweka watu kama Kina Komba, Khadija Kopa, Tambalizeni,Asha baraka kwenye vyombo vya maamuzi vya CCM, huku ni kuchezeana kweli,
Same applies kwa chama kama CUF, hasa pemba ambako kuna wabunge unaweza kuquestion hata uwezo wao wa kujiwakilisha wenyewe lakini unasikia ni members wa baraza na wawakilishi na bunge. Sijui rationale ya hii kitu ni nini. Nadhani kama wakitaka Komba aingie kwenye Mkutano wao anaweza kuingia akiwa na kwaya, alkini bado naonaona ni ajabu sana kwa baadhi ya members kuweko kwe sehemu kama hizo.Labda sijui vizuri role zao mle ndani, je ni kuhamasisha watu kwa kuwaburudisha wajumbe, au wao wenyewe wanafanya maauzi makubwa?????????..........Matokeo yake ndiyo hayo mtu anakuja kusifia safari za JK nje ya nchi wakati sasa hivi Wizara nyingi zinasuffer kwa kukatwa migao kutokana na serikali kutumia mapesa kupita kiasi. Ukweli wa mambo kutoka serikalini kwenyewe unaonesha vingine na kauli ya Tambalizeni inaonesha vingine, watu design hii kweli hawasaidii sana, wawe na role zinazohusu fani zao.
 
Tambalizeni anasema JK anatafuta misaada Tanzania Inufaike.je ni kweli hii?

Si kweli. Ni maajabu tu ndiyo yataiwezesha Tanzania kunufaika, kwa maana ya maendeleo, kwa kupitia misaada. Kuna semi zilitumika sana wakati wa Mwl. kuwa mtegemea cha nduguye ufa maskini, na nyingine ni ile ya 'omba omba Nyerere alikataa'. Semi hizi mbili zilikuwa na maana halisi ya kujenga uwezo binafsi wa mtanzania na Tanzania kujitegemea.

Mwl alijaribu kuelezea kwa usahihi ni namna gani twaweza kujitegemea. Mwl. akupuhuza misaada na ndiyo maana alisema source ya maendeleo 'Development' ipo huko nje. kwa maana ya huko Msh anakokwenda kutafuta misaada. Lakini kuonyesha kuwa kunajambo kabla ya kwenda huko linapaswa kutimizwa Mwl alisema kuwa kama nchi ni lazima kutumia resources tulizonazo kwa kiwango cha hali ya juu kabisa. Kwa maana hiyo utafutaji msaada nje unakuja baada ya kuonyesha namna nzuri ya matumizi ya rasilimali za nchi, kama mali ya asili na rasilimali watu. Na huu haswa ndio msingi wa nchi huru. Kwa hiyo anachosema Tambalizeni si msingi wa uchumi wa nchi huru bali ni msingi wa kufunganisha uchumi wa nchi yetu na sera za mataifa mengine ambayo hata baada ya uhuru wa nchi zetu dhana halisi ya ukoloni bado haijafifia akilini mwao. Bado wanaitaji masoko kwa ajili ya bidhaa zao za viwandani, mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao na hata cheap labour. Why Japanese are Financing most of the Road projects? Simple, just count their cars. Kwanini wasi-invest Nyumbu pale kibaha tukatengeneza magari yetu kwa wingi tukauza tukapata fedha tukajenga barabara zetu wenyewe.

Kama watanzania tunahitaji kupia hatua Msh Rais anapaswa kutujengea misingi ya kujitegemea ambayo kwangu mimi kadri tunavyotanga mbali nayo ndivyo nchi yetu inadumaa na kubakia ktk takwimu za maendeleo yasiyo kuwa na msingi dhabiti. Ni kutokana na misaada hiyo ndo maana serikali haitambuwi uzito wa mawaziri zaidi ya 60 kwenye serikali, serikali haiwezi kutambua gharama za uendeshaji mashangingi kwa watumishi wake. Ni misaada hii inaifanya serikali kulala ktk vita dhidi ya ukimwi na kuwaachia USAID/Crinton Foundation. Ni kupitia misaada hii serikali haiwezi hata kupambana na kutokomeza malaria.
Ukitegemea misaada unapoteza ufahamu juu ya uwezo wako ktk kujiendeleza na hivyo usishangae kumwona Mkuu wa Mkoa wa Dar akihitaji msaada wa wananchi ili kujenga shule. It is a shame to our nation kutokuwa na priority kwenye key issues zinazogusa majority wananchi. Kodi zetu zinatosheleza kuendesha serikali na pesa ya maendeleo inatoka nje. Poor Tanzania
 
nimemsikia Sheikh Yahya kupitia radio fulani ya kidini akimwaga sifa za ajabu kwa JK akisema amevunja record ya kutoa hotuba kwa masaa 3 bila ya kuchoka na ilikuwa kama chakula kwa kila mtu
Huyu Mganga nae anatupa hadithi gani? tumeshiba kusikia longo longo zake msanii JK
hotuba yake ambayo ni kama nguvu za muujiza ama Mungu
.
Duh! hii kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom