What are the legal terms and conditions for changing the name?

ropam

Senior Member
Aug 11, 2010
173
35
Natanguliza shukrani zangu wana-jukwaa...mimi ni kijana ambaye nimemaliza chuo kikuu mwaka huu. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimesoma elimu yangu yote mpaka hapa nilipofika kwa jina la upande wa mama (babu yangu upande wa mama), sasa mimi nataka kubadili hili jina nianze kutumia jina langu halisi lakini kuna maswali najiuliza nashindwa kuelewa itakuwaje...maswali kuhusu vyeti vyangu ambavyo kuna vingine ni certifications za kimataifa! Naomba msaada wenu wana-jukwaa, nahitaji kujua kama kuna uwezekano wa kutambulika kwa jina langu halisi (hili jipya ninalolitaka) huku vyeti vilivyo na ubini tofauti vikiendelea kutambulika kama vyeti vyangu halali stil! Akhsante.
 
nenda mahakamani kana jina lako la zamani sema la sasa, then ukiwaa unatumia hivyo vyeti vyako itakubidi uambatanishe cheti ulichopewa mahakaman na cheti chako cha zamani chenye jina lako
 
Nenda kwa mwanasheria yeyote akutengenezee document inayoitwa deed poll,ipeleke kwa msajili wa nyaraka(Wizara ya ardhi) uisajili.
 
Akhsante sana mkuu...na swala lingine, kutahitajika kiapo chochote cha mzazi?
 
nenda mahakamani kana jina lako la zamani sema la sasa, then ukiwaa unatumia hivyo vyeti vyako itakubidi uambatanishe cheti ulichopewa mahakaman na cheti chako cha zamani chenye jina lako
Shukrani sana...na vip kuhusu viapo vya wazazi, kuna umuhimu wa mzazi kuapa?
 
Nenda kwa mwanasheria yeyote akutengenezee document inayoitwa deed poll,ipeleke kwa msajili wa nyaraka(Wizara ya ardhi) uisajili.

Halafu kwa nini wizara ya ardhi? Inahusiana vipi na kubadili jina?
 
Sidhani kama mkubwa hapo kamanisha uende wizara ya ardhi....bt ofisi za msajili wa nyaraka ndo zipo maeneo ya wizara ya ardhi!
 
nenda mahakamani kana jina lako la zamani sema la sasa, then ukiwaa unatumia hivyo vyeti vyako itakubidi uambatanishe cheti ulichopewa mahakaman na cheti chako cha zamani chenye jina lako
Hii hapa ndio njia halisi, hata mimi nilipo zaliwa nilikua na jina lingine (Yasmin), na babu yangu akanipa kashamba. baadae kidogo nilipoanza shule nikapewa jina lingine (RussianRoulette) na nilivo fika miaka kama 20 nikaenda land tittle kubadili makaratasi ya shamba nikaambiwa lazima nilete document toka mahakamani kuthibitisha kwamba Yasmin na Russian Roulette ni mtu mmoja. Mahakamani waliomba cheti cha kuzaliwa, vyeti vya wazazi na mashaidi wa2 wasio wa familia. karatasi zilitoka within a month na sasa nikitumia cheti cha kuzaliwa naambatanisha na certified copy ya mahakama na that is enough.
Ila nikuuliza swali: kwa nini unasema ulikua unatumia jina la babu sasa unataka utumie lako mwenyewe? hilo unalo ita lako si la babu yako pia? au baba upande wa mama? alikua wapi wakatu wanakupanga la upande wa mama? uko huru utumia jina unalo litaka ila hakikisha arguments unatumia haliwaumizi watu wako wa karibu. samahani kwa kuingia katika mambo yako binafsi bila kualikwa....
 
Akhsante RussianRoulette....mimi nina story complicated haswa, nusu ya umri wangu nimeeishi na mama na nusu nyingne nimeishi na baba, sasa wakati nilioishi na mama ni wa utoto wangu ambao mama baada ya kuachana na baba alirudi nyumbani kwa baba yake...hivyo mimi nilianzishwa shule na babu mzaa mama na akaniandikisha kwa jina lake (babu mzaa mama), but nilipofika darasa la 5 nilihamishwa shule na mkoa kwenda kuishi na baba ambaye ndo nimekuwa naishi naye mpaka leo...sasa katika maisha ya kawaida mimi najulikana kwa jina la upande wa baba hawajui kama jina langu official la kwenye vitambulisho ni la upande wa mama, kuna wakati wananitumia package kwa jina langu la upande wa baba but napata shida kuvichukua sababu vitambulisho vyangu vina jina tofauti....then umri umeenda Roulette saa yeyote familia itaingia ndani ambayo itahitaji kubeba jina langu, watabeba jina gani na mimi natumia jina la watu?
=> vyeti vya wazazi ulivyovisema hapo ni vya kuzaliwa? na ni lazima?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom