Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,523
Waheshimiwa Wabunge,
Naomba kuwasilisha ombi rasmi kwenu na kuwataka muwe sauti za Wazee Wastaafu na Wafanyakazi wa Tanzania.
Wazazi wangu ni wastaafu, kutoka ajira za mashirika ya Serikali. Viinua mgongo vyao kila mwezi ni Shilingi elfu ishirini (20,000.00) tu!
Wazazi wangu na maelfu ya wastaafu wengine ambao wamelitumikia Taifa kwa moyo mkunjufu na uvumilivu tangu tupate Uhuru na kutujengea Taifa mpaka hapa tulipo, wanaendelea kuishi maisha ya dhiki na duni, huku wakipuuzwa na Serikali yao wanapoanzisha mijadala au mazungumzo ya kubadilisha miundo au namna viinua mgongo vyao (pensheni) zinavyofanya kazi.
Hata pamoja na kuwa kima cha chini ni bado hakiridhishi na ni cha kimasikini sana, lakini kukosekana kwa uwiano wa mapato ya Wafanyakazi walioko katika ajira sasa hivi na wale walio wastaafu, si haki au utu.
Nafahamu fika kuwa Taifa letu ni bado changa na linajaribu kujitutumua kutoka Umasikini. Lakini kuendelea kuishi na kufanya kazi kwa Umasikini si jawabu, bali ni kumaliza nguvu za mwili ambazo huzaa juhudi na kupumbaza mawazo ambayo huleta maarifa.
Mfumo wetu wa Pensheni umeendelea kutoa upendeleo kwa kundi dogo sana la Wastaafu. Badala ya kuwa na uwiano ili kila aliyelitumikia Taifa ajivunie alichofanya na kuona anathaminiwa, sisi kama Taifa na Serikali yetu, hatuwathamini tena wale wote ambao wamestaafu.
Wale waliokuwa waajiriwa wa Shirikisho la Afrika la Mashariki, bado wanadai mafao yao huu ukiwa mwaka wa 30 tangu jumuiya ivunjike. Tunajua tulipewa pesa na wafadhili ili kufanya malipo haya, lakini kwa sababu za "kiserikali" wastaafu hawa waliotumikia EAC wa Tanzania wakalipwa takribani 10% ya haki yao na wakaambiwa washukuru Mungu kuwa wamepata japo hiyo 10% ya haki yao.
Najiuliza, kipato cha Shilingi Elfu Ishirini kwa mwezi kinamtosha nani Tanzania? Awe mstaafu au mwajiriwa, je wanawezaje kuishi kwa kutegemea shilingi Elfu Ishirini?
Kilo moja ya Sembe si chini ya Sh. 1000.00, Ratili moja ya Nyama ni Sh. 1200+, nauli ya daladala si chini ya sh.400, nauli kutoka Arusha Mjini kuja Dar NPF (NSSF) au PPF si chini ya sh. 25000.00, kodi ya nyumba au chumba kwa mwezi si chini ya sh.10000.00. Hapo bado hawajalipia huduma hospitali au kununua madawa ukizingatia kuwa uzee wao unahitaji kupata huduma za matibabu mara kwa mara.
Sasa jiulizeni wakati mlipotamka kuwa nyinyi kama Wawakilishi wetu mnataka mishahara na marupurupu makubwa kwa kuwa hali ya maisha ni ngumu, je mwananchi mwajiriwa aliyeko kazini au aliyestaafu anaishije?
Ikiwa Rais Mstaafu atalipwa 80% ya mshahara wake wa mwisho mpaka siku Muumba anamchukua, huku akiwa na marupurupu kama nyumba ya bure, gari, dereva, wahudumu, huduma za afya na mafao mengine kwa kazi aliyoifanya kwa kipindi kimoja au viwili vya miaka 10, au Waziri mkuu ambaye naye hulipwa na kupata marupurupu karibu sawa na hayo kwa kazi hata ya muda mfupi kama Lowassa ya miaka miwili, na wake zao kuwa na haki ya kuendelea na marupurupu na kupokea pensheni ambayo ni karibu 40% ya mshahara wa mwisho, je hamuoni ulazima wa kuhakikisha si viongozi na vigogo pekee ambao wanapata ahueni bali ni hata wale wa kawaida wastaafu, madereva, mataarishi, wahasibu, waalimu, wauguzi, waganga, wahandisi na wengine wote ambao wengi wao wamelitumikia Taifa katika ajira kwa zaidi ya miaka 30?
Mmeomba muongezewe Mishahara na Marupurupu, lakini kilio cha wafanyakazi kutaka kuongezewa mishahara mmekifungia macho na kuziba masikio kama vile si wajibu wenu au ni tatizo lenu. Mnadai pensheni nono na marupurupu, lakini kila mwaka bajeti za wizara ya kazi na utumishi zinapita bila kusikia hata sauti moja ikihoji ni vipi Taifa liwatumikie wale wote waliolitumikia kwa moyo?
Wastaafu hawa waliolijenga Taifa letu wanapuuziwa hata kukaribishwa na kupewa kazi za kuwa washauri au kuziba nyufa za ukosefu wa wataalamu. Mfano, je kuna ubaya gani kwa halmashauri zetu za mamlaka ya mikoa au wilaya kuendelea kutoa ajira kwa Waalimu, Wauguzi na Waganga ambao wameshafikisha umri wa kustaafu ili kuziba pengo la uhaba wa wataalamu katika fani hizo?
Naomba sana mnapokaa katika kikao hiki cha bajeti, msikimbilie kukoromea ufisadi pekee, bali muanze kutetea haki za Wananchi wenu, wapiga kura wenu kwa kuwasilisha muswaada wa kubadilisha mfumo wa pensheni za wastaafu, kuunda mbinu mpya za kuhakikisha kuwa wastaafu wa ngazi na kazi za aina zote wanaendelea kuthaminiwa na kuhudumiwa, kuhakikisha wale wote wanaodai Serikali na Mashirika masalio ya Pensheni zao wanalipwa na muhimu zaidi ni kuhakikisha kuwa mfumo mpya na mishahara mipya inatangazwa rasmi na Bunge na kufanya iwe ni sheria na si kama kauli ya Waziri wa Kazi au Utumishi ambao walichokifanya mwaka jana ambayo imekuwa ni kituko.
Msisubiri kulifanya hili Juni ya 2010, lifanyeni sasa mna nafasi ya kulijenga Taifa na kuwaenzi Wastaafu na Wafanyakazi wote.