Wezi wavamia na kuiba Ikulu ya Afrika kusini.

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,192
2,000
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya bbc swahili (Dira ya Dunia) Ikulu ya Rais wa Afrika kusini imevamiwa na wezi ambao wa wamefanikiwa kuiba. Inadaiwa kwamba waya wa ulinzi, uliondolewa bila polisi, maafisa usalama wa ikulu na walinzi maalumu wa ikulu kujua.

This is terrible, vipi kuhusu ikulu yetu? nadhani hili litatushtua kama tulikuwa katika usingizi.

Vipi usalama wa wananchi na watu wengine huko S.A kama wezi wanafanikiwa kuiba ikulu? Hatari tupu.
 

Sra

Member
Jul 5, 2007
44
70
Duh!! hiyo tena ni kali. ila bongo nadhani wapo makini kwa maana wahusika wenyewe ndio wezi sasa sidhani kama wanaweza kulala usingizi na kuwaachia wenzao wafanye mambo
 

think BIG

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
236
195
Walipanda juu kwenye paa ya nyumba anayoishi rais Mbeki na kuiba zile nyaya za kuzuia radi (nyaya za aluminium). Nyaya zenyewe zina dhamani ya kama Tsh milioni 5.

Kila mtu anashangaa nyumba hiyo ya rais ina ulinzi mkali sana, sasa imewezekanaje mtu kuingia na kupanda juu ya paa, na kutoka na hizo nyaya zote! Lakini askari wa getini wamehojiwa na kusema wao huwa hawakagui magari yanayotoka ndani bali yale yanayoingia tu!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom