Wezi wako Tofauti ?

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wana ndugu

Jana nimesoma walimu wamepigwa miaka 14 jela, Viboko na kazi ngumu kwa ajili ya wizi wa pesa za shule ya msingi shilling za Kitanzania 800,000.
Waliotiwa hatiani ni walimu 3 yule wa nne aponea chupuchupu.

Swala la Msingi.
Hivi huu wizi unatofautiana? mwizi si ni mwizi tu jamani? sasa kwa nini anayeiba kidogo anahukumiwa mapema na adhabu yake ni kali - huyu mwizi mwingine anayeiba mamillioni yeye kwanza kesi yake inachukua muda, then inafikia hatua mahakama inakosa kifungu cha kumtika hatiani kulikoni?

Inaniuma sana kuona wezi hadi wanadiriki kurudisha pesa walizoiba serikalini na wanapewa risti ya Received by Goverment of Tanzania - lakini hadi leo tunao mitaani na suala la wao kufungwa hilo kwa yeyote hapa JF atakubalina na mimi kwamba hafungwi hata mmoja wa hao jamaa.

Sheria iwe msumeno kama mwizi ni mwizi tu hata kama Umeiba bata au mamilioni ya shilling. Sheria ya wizi isibakie kuwahukumu walalahoi tu.

Hili ni tatizo na lipo katika mfumo mzima wa utoaji haki hapa nchini kwetu. kuna mkongomani mmoja aliniambia - "In Tanzania if you have money you will never go to jail" Nimeamini
 
Mwizi wa kuku anapigwa hadi kufa, na labda huyo kuku ni wa kitoweo yeye na wanawe menye njaa ya ajabu. Mwizi wa mamilioni anasifiwa kwa magari anayoendesha,nyumba anazomiliki na kuimbwa na kila bendi bila kujali kuwa katika wizi huo serikali imeshindwa kununua dawa na mamia wanakufa as a result thereof, na pia kuwa hiyo ilastahili kuwa mishahara ya waalimu.

Watanzania tunasikitisha sana.
 
wezi wakubwa Ruksa,
Wanaleta uchumi kwa wananchi moja kwa moja, kwanza ukoo wake na ndugu wanaomzunguka wananeemeka. Vibarua wanapata neema bila kuwasahau wapambe wake. Na watanzania halisi Ajira zao nyingi Zinapatikana huko.
Serikali imekosa uchumi wa kumnufaisha mtanzania halisi, ni bora zaidi ya hawa watu kuzichukua na kuzitawanya, kuliko kwa pesa kuishi ndani ya makabati kwa jina Strong room.
Haha....
 
Mkuu unaumia kwa hilo katika nchi hii? Chunga sana usije ukafa siku si zako kama wasemavyo waswahili. Nji ina wenyewe hii!
 
Mkuu Elnino mi mwenzio sasa hivi nimeamua kuwa sugu.
Kwani nilikuwa naumia sana kwa matukio kama hayo lakini sasa hivi nishazoea, moyo umekuwa sugu.
Hii nchi hii. Tuache tu ndugu yangu kwani hakuna wa kumfunga paka kengele.
Tulio hisi ni Wazalendo wametusaliti.
 
Unaogopa kufa wakati watanzania tulikwisha kufa??? Tunavyoishi, tunavyofikiri sisi ni mizoga. Kumbuka kuwa Nchii hii ni yetu wote na rasilimali ya nchii hii ni yetu wote hakuna mwenye nchi. Amka ndugu yangu drifter
 
Mkuu Elnino mi mwenzio sasa hivi nimeamua kuwa sugu.
Kwani nilikuwa naumia sana kwa matukio kama hayo lakini sasa hivi nishazoea, moyo umekuwa sugu.
Hii nchi hii. Tuache tu ndugu yangu kwani hakuna wa kumfunga paka kengele.
Tulio hisi ni Wazalendo wametusaliti.

Kwa nini tuache???? Zile hadithi za kumfunga paka kengele zilikuwa ni za kizamani, suala sio kumfunga paka kengele suala ni kutowapa ridhaa ya kutawala na hivyo itafanywa kwa kupiga kura dhidi yao na kuchagua viongozi mbadala. Hao waliotusaliti si tumewapa ridhaa sisi wenyewe ni kuwanyima hiyo ridhaa basi.
 
Mkuu unaumia kwa hilo katika nchi hii? Chunga sana usije ukafa siku si zako kama wasemavyo waswahili. Nji ina wenyewe hii!
Mkuu hayo mambo ya kuogopa ogopa ndiyo yanatu-cost, hata kuhoji tu vitu vya msingi kama hivi mtu unaogopa eti utakuwa pointed out, kwani nchi haina katiba? Wenyewe ni akina nani?
 
Kwa nini tuache???? Zile hadithi za kumfunga paka kengele zilikuwa ni za kizamani, suala sio kumfunga paka kengele suala ni kutowapa ridhaa ya kutawala na hivyo itafanywa kwa kupiga kura dhidi yao na kuchagua viongozi mbadala. Hao waliotusaliti si tumewapa ridhaa sisi wenyewe ni kuwanyima hiyo ridhaa basi.

mkuu usemayo ni kweli kwamba kutokuwapa ridhaa ya kutawala ila swala linakuja kwamba uwachague au usiwachague lazima wanashinda tu njia iliopo ni moja tu naomba nisiitaje kwa ss
 
nchi ya maajabu hii..............unaadhibiwa kwa kosa la kuiba kidogo.....ukiiba sana unapongezwa
 
Back
Top Bottom