Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Tulipokuwa shule ya msingi kulikuwa na wanafunzi wawili walikuwa na sifa ya kuiba vichongeo. Wakati wa mapumziko wanazuga wakizunguka karibu na mlango na kwenye korido ili wanafunzi wengine waende kula halafu wao wanakagua kompasi moja baada ya jingine.
Mmoja anasimama mlangoni akitazama nani anayekuja halafu mwingine ndiye mwizi mwenyewe. Watu wakirudi darasani wanakuta vichongeo vimeshaibiwa. Hakuna aliyewashtukia kwa muda wote wakifanya wizi huo.
Maishani hawa watu wawili hawawezi kushindwa kuchora mchoro wa wizi wa mabilioni ya fedha iwapo wanapata vyeo kwenye mashirika ya umma au serikalini.
Wizi kama yalivyo maendeleo, ni kitu ambacho hakijali itikadi au imani ya dini ya mtu. Mafisadi wapo CCM wapo ACT, wapo CHADEMA. Sio kwamba mtu akitoka CCM na kuhamia CHADEMA basi anageuka malaika, kama alikuwa ni mwizi wa vichongeo shule ya msingi, tabia chafu anahama nayo.
Sio kwamba kwa sababu mwanasiasa akihama kutoka CHADEMA na kuingia CCM tayari anageuka kuwa mmoja wa malaika. Halmashauri zinazoongozwa na CCM zina sifa ya wizi, zile za CHADEMA na zenyewe zinao wapigaji wa kiwango kikubwa.
Ni aina fulani ya ukwepaji wa majukumu kuamini kwamba chama fulani cha siasa kimejaa uadilifu na kingine kimejaa ufisadi. Wezi wa vichongeo wamejaa kila mahali, hawa ndio wa kupambana nao kwa nguvu zote.