Wezi wa mitihani kudhibitiwa..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,687
2,000
Wezi wa mitihani kudhibitiwa

Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 14th December 2010 @ 07:00

BAADA ya kukithiri kwa wizi wa mitihani katika Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), serikali imetangaza kununua mashine maalumu zitakazotumika kuandaa mitihani mbalimbali ya taifa na kupunguza wingi la waandaaji watumiao mikono ili kukomesha wizi huo kuanzia mwaka mpya wa fedha wa 2011/2012.

Aidha, imeelezwa kuwa, kiwango cha chini cha elimu ya Mtanzania kitakuwa ni elimu ya kidato cha nne, badala ya ile ya darasa la saba ya sasa, kuanzia mwaka 2015.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema jana wakati wa ziara yake kwenye Baraza la Mitihani la Taifa, Mwenge, Dar es Salaam, kuwa miongoni mwa mambo atakayoyapa kipaumbele katika wizara yake hiyo mpya ni pamoja na hilo la kukomesha wizi sugu wa mitihani ya Taifa.

Dk. Kawambwa alisema ili kutekeleza azma hiyo ya serikali, itatenga fedha za kutosha kununua mashine mpya kadhaa zitakazochukua nafasi ya watendaji waliokuwa wakiandaa mitihani hiyo kwa kutumia mikono yao, katika hatua zote muhimu, na hivyo kutoa mwanya wa wizi huo.

Alisema hatua hiyo itaziba mianya hiyo ya wizi, kurudisha imani ya Watanzania kwa Necta pamoja na kuifanya elimu ya Tanzania kuwa na heshima yake inayostahili.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, ingawa wana kazi nzito ya kuhakikisha watumishi wa baraza hilo pamoja na walimu wanaohusika kusimamia mitihani hiyo wanakuwa waaminifu, wameona kuwa mashine hizo zitakuwa tiba sahihi ya tatizo husika itakayoondoa kero hiyo kwa asilimia kubwa, na hivyo kuamua kuzitengea bajeti katika mwaka mpya wa fedha wa 2011/12.

“Mashine hizo ambazo kwa makadirio ya juu zitatugharimu shilingi za Kitanzania bilioni tano, zitafanya kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa na mikono ya watu wengi na hivyo kuruhusu usiri mkubwa wa mitihani hiyo, pamoja na kuondoa ulazima wa kupita mikononi mwa mikono hiyo,” alisema na kuongeza: “…Serikali imeamua kuwekeza katika hilo.

Tutahakikisha tunanunua mashine zenye uwezo wa kufanya kazi kubwa ya kukagua karatasi, kuchapisha na kuhifadhi mitihani kwenye vifaa maalumu vya kuhifadhia ili kuufanya uandaaji huo kuwa na usiri wa hali ya juu kiasi cha waandaaji wachache watakaokuwa wanahusika kushindwa kufanya mchezo wowote mbaya utakaoifanya isambae au kuibwa.”

Alisema ingawa wizara yake na hata NECTA hawajapanga idadi kamili ya mashine zitakazonunuliwa wala fedha zitakazotumika, wamekwishafahamishwa gharama ya kila mashine kuwa ni Sh bilioni tano.

“Mashine hizo zinapatikana na kwa makadirio ya juu, kila moja itatugharimu shilingi za Kitanzania bilioni tano. Tutazinunua kwa sababu tumeona kuna kila sababu ya kufanya hivyo sasa,” alisema Dk.Kawambwa.

Kuhusu kiwango cha chini cha elimu nchini kupanda hadi kidato cha nne, Dk. Kawambwa alisema kitawawezesha Watanzania wengi, hasa wanaotoka katika familia duni kupata nafasi katika soko la ajira zile za kati kwa kuwa wengi walikuwa wakikwama kwa kuishia darasa la saba pekee.

Alisema, hiyo ni moja ya mambo yaliyoainishwa katika Ilani ya CCM na kwamba atalisimamia kuhakikisha linafanikiwa kwa kuhakikisha elimu bora kwa kila mwanafunzi Mtanzania atakayeipata.

“Hakutakuwa na mwanafunzi atakayeishia darasa la saba kwa sababu za kukosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari, wote watachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na watapitia majaribio na mitihani mingine ya kawaida katika shule zao. Ule mtihani wa mwisho wa elimu hiyo ya kiwango cha chini sasa utafanyika kwenye ngazi hiyo ya kidato cha nne,” alieleza Dk. Kawambwa.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,687
2,000
BAADA ya kukithiri kwa wizi wa mitihani katika Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), serikali imetangaza kununua mashine maalumu zitakazotumika kuandaa mitihani mbalimbali ya taifa na kupunguza wingi la waandaaji watumiao mikono ili kukomesha wizi huo kuanzia mwaka mpya wa fedha wa 2011/2012.
Hivi jamani tuambiane ukweli ..................tatizo hapa ni mitambo au kuwa na watumishi ambao siyo waaminifu..........na kushuka kwa maadili nchi nzima............................................kama haya nisemayo ni kweli basi mitambo mipya kamwe haitaondoa tatizo la wizi wa mitihani..............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom