Wezi wa mali za Umma na J. Nassari nani anahatarisha amani Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa mali za Umma na J. Nassari nani anahatarisha amani Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naytsory, May 8, 2012.

 1. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wakuu katika akili ya kawaida isiyohitaji shahada wezi wa EPA, wahujumu uchumi na hawa Viongozi wa Chadema kina J. Nassary, Dr. Slaa, G. Lema na wengine wanaowaelimisha raia wasiendelee kunyanyaswa, kudhulumiwa haki zao, kuibiwa rasilimali zao na kutendewa maovu mengine mengi, nani alipaswa kuhojiwa na polisi wetu, na ikiwezekana kufunguliwa mashitaka? Je kwa hiki wanachofanya polisi chini ya ccm kuna tofauti gani na majambazi walioteka basi la abiria na kuwaamuru watu wote kuinamisha vichwa au kulala chini na kila anayetaka kunyanyuka au kuamka anashughulikiwa ili wengine wasithubutu, tukisema ccm na polisi ni sawa na majambazi wa aina hiyo sina hakika kama ni makosa. Sijawahi kusikia polisi wakiwahoji wezi wa mali za Umma na viongozi wabadhirifu hata siku moja ni mpaka Rais aseme, Polisi kuweni wazalendo hii nchi ni yetu sote hata ninyi inawahusu, siyo ya viongozi wa ccm peke yao? Nawasilisha.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwao mtu hatali ni yule anae hatalisha uwepo wa CCM....Ndiyo maana uliowataja wanatolewa macho kuliko Rostam Aziz
   
 3. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hiyo inaitwa polisiccm haina meno ya kuwang'ata wezi na wahujumu uchumi.
   
 4. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Police Wetu kevu 2
   
 5. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Rais Kikwete tunaomba kama unataka Watanzania tukukumbuke urekebishe hilo, vinginevyo tutaendelea kukulaumu wewe na kizazi chako na hasa kwa kuwalinda wahujumu uchumi na kuwadhalilisha wazalendo.
   
 6. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Hao wanaitwa polisi linda ccm!polisi linda mafisadi
   
 7. M

  MARKYAO JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 512
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Kaka uko sahihi kabisa. wabadhirifu ndo wanaonekana mashujaa huku wanaowafungua wananchi macho na kufichua uovu wanaonekana maadui. Polisi ifike mahali ijitambue kwa kuwa maisha ya duniani ni ya muda tu.
  CCM wanajiona no miungu wa Tanzania na waweza kufanya lolote regardless hiliwaumizi viongozi. Wanaoathirika ni wananchi wote wakiwemo wana CCM wasio na Madaraka. Wanatumiwa kuwavusha majambazi juu wakivali kijani.
  Wanajimegea nchi kama wanaishi milele, wanadharau watu kana kwamba hawako Tanzania, wanathamini wageni kwa kuwa wanawapa rusha, wanachi wa kawaida wanateseka kwa kuwa serikali ni rafiki wa wawekezaji. Mtanzania anakuwa Mkimbizi,mlipa kodi, mfumko wa bei ni kwa ajili yake, maisha dunini na mengineyo. Nani atawaelimisha? ni Lema, Slaa, Mbowe,Zitto,Sungusia,Nkya na wengine wenye mapenzi mema. CCM ni Hatari.
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Ni ulinganishi wa kijinga mkuu!
  Anayehatarisha umoja wa kitaifa na mwizi wa mali za taifa kuna ulinganishi wa aliye afdhali hapo?

  Jiulize mwenyewe mwizi wa kuku na mwizi wa bata nani zaidi? Jibu unalo mwenyewe na zaidi ya hapo changanya na za kwako.....
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Wewe kweli akili yako ndogo............. Mwandishi anajaribu kukueleza kuwa wanaohatarisha amani ya nchi ni mafisadi na magamba then wanajaribu kusingizia wapinzani halafu wewe unataka kuwaweka kwenye chungu kimmoja?? Tumia walau dakika kumi kufikiria kabla ya kuandika ili kuficha ujinga wako!!
   
 10. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sina hakika kama umesoma habari yote, na kama umesoma basi uwezo wako ni mdogo au umekurupuka, pole mkuu kama yanakuhusu.
   
 11. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Asante Mkuu!!! watu wengine wanatumia sijui Masaburi kufikiri? Halafu utakuta ni mtu mzima na akili zake kabisa....inashangaza kweli Wtz tunavyoshindwa kuiterprete very simple sentences....
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Bora ya mwizi wa mali za uma kuliko kilaza anayehatarisha amani ya nchi yetu nzuri Tanzania.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kushindwa kumshughulikia mwizi wa ngo'mbe hakuhalalishi mwizi wa. Kuku.

  Kama Wenye power hawachukuliani hatua kwa makubwa hakumaanishi walala hoi kuachwa kwa madogo.

  Siipendi CCM lakini pia sikubaliani na yeyote anayetaka kuhatarisha amani yangu kwa kigezo cha wizi wa CCM.

  So kama nassari kaonewa si haki lakini kama kavunja sheria basi wizi wa CCM isiwe kigezo cha yeye kuwa sahihi hata kama lakosea
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiyo kilaza wa kutupa! Hivi hujui kwamba sentensi ya kwanza kabisa katika Utangulizi (Preamble) ya PCCB Act ya 2007 inatamka wazi wazi kwamba ufisadi unaweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi? Nenda kaisome kilaza wee!!
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  JF imevamiwa na vilaza siku hizi. Nashukuru kwa kuliona hilo.
   
 16. M

  Midavudavu JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amepanda basi bila kuuliza wapi linaelekea.
   
 17. N

  Ndaskoniax Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aseee kweli kabisa
   
 18. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Polisi wote ni majambazi, yakiongozwa na Said Mwema ambaye pia ni gidi la kimataifa.
   
 19. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwa mawazo haya nawe ni miongoni mwao? Kama ndivyo lazima uhofu kwa sababu wanaoibiwa wakiamka usalama wenu utakuwa mdogo.
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Mediocre characters that dont merit my response.
  Wakuu tafuteni size yenu ya vijana wa darasa la saba, au kama wale wabunge wenu wa arusha.
   
Loading...