Wezi wa madini ya TANZANITE hapo Mererani Mkoani Manyara watiwa mkononi mwa POLISI!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,216
Wale wezi waliotajwa majuzi kuiba madini yenye thamani ya mabilioni ya Tsh wametiwa nguvuni jana na police wakisadiana na raia kwa namna ya pekee! Wezi hao wamekamatwa katika kijiji cha jirani kabisa na makazi ya machimbo yalipo na wale wenzangu wanaoijua vizuri hapo Mererani ni wamekamatwa pale kijiji cha Naisinyai. Alikuwa amefukia madini yote ardhini na kupanda mboga juu yake,lakini polisi walipofika walinyookea pale pale mzigo ilipokuwa. Na mpaka sasa ni zaidi ya watu 19 wameshashikiliwa kwa upelelezi zaidi

Kwa kweli huyu aliyekamatwa ni mzembe katika wazembe wote yeye ndiyo wa kwanza na katika wajinga yeye ndiyo nambari wani.


UPDATES

Kesi inaendelea tarehe 17/12/2012 na imeahirishwa mpaka trh 19/12/2012

NITARUSHA YAJIRIO MWANZO MWISHO!
 
Una mpango mzuri wa kuiba, ila huna mpango kabisa wa kutoroka ! Bora usingeiba kabisaaaa !
 
Wange wapa kidogo hao polisi wangepiga kimya tuna wajua ni jaa sana...
 
Kwani walioibiwa si Riz1 na wahuni wake au...kama ndiyo naona wawaibie tu maana taifa halifaidiki kwa vyovyote riz1 ananua magari
Hivoe kwaiyo tusiwalaumugi wakifanyaga ivo sometimes...
 
Ally Kombo; Nakwambia ungekuwa unajua bei ya hiyo madini bila shaka huyu aliyekamatwa ni kwamba nimeshindwa kumjua alikuwa na lengo gani. Gram 1 ya tanzanite ni Tsh 900,000 bila hata kupungua shilingi sasa ukisikia mtu kama huyu amekamatwa Mi inanigusa sana. Makaburu wakisaidiana na mtoto wa jk wanaisombea South Africa.


QUOTE=Ally Kombo;5183365]Una mpango mzuri wa kuiba, ila huna mpango kabisa wa kutoroka ! Bora usingeiba kabisaaaa ![/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
Lazima kuna kiherehere aliwashwa akamwuza mwenzie.Hao makaburu hawana faida kwa maisha mtanzania.Bora yangebaki kwa mtz angetununulia bia.
 
MLERAI; kwa kweli kabisa hili watakuwa wameuzana tu!


Lazima kuna kiherehere aliwashwa akamwuza mwenzie.Hao makaburu hawana faida kwa maisha mtanzania.Bora yangebaki kwa mtz angetununulia bia.
 
Last edited by a moderator:
Duh kama kweli wamekamatwa roho imeniuma sana watu walivyokuwa wanavuatilia kununua huo mzigo...Dah nimeishiwa nguvu kabisa.
 
Roho inaniuma, sana, siungi mkono wizi ila kwa hili hapana, hawakujipanga vizuri, na watakuwa wamesalitiana
 
Ina onekana hawaja vunja ungo hao, wamenirusha roho kweli hao dah! Mi nili jipanga kulipa kash
 
babuwaloliondo; Hakika hakuna mtu anayeunga makono wizi ila kwa jinsi serikali tawala na chama chake kinachowafanya wanainchi kwa kweli kwa hili hakika niliunga mkono hoja!

Huu uzembe waliofanya hawa wahusika hakika Mi ninailaani mbaya mbovu!


Roho inaniuma, sana, siungi mkono wizi ila kwa hili hapana, hawakujipanga vizuri, na watakuwa wamesalitiana
 
Last edited by a moderator:
Ile kesi ya wadau hapo juu imeendea jana jumatatu na hata hivyo imesomwa tu bila ya kusikilizwa na kupigwa tarehe ya 19/12/2012 jumatano na ndipo waangalie kama jamaa watapata mdhamana,habari hizi nimezipata live toka mtu aliyetoka jana hapo Mkoani Manyara na hata hiyo asubuhi ya kesho atakuwepo tena mahakamani na habari alizonitonya ni kwamba madini yenyewe aliyokutwa nayo mshitakiwa imefika kitu kingine tofauti! Ama kweli hili neno linakamilika KUPASUKA KWA PAKACHA NAFUU KWA MCHUKUZI na hata hivyo tegemeeni news zaidi hiyo kesho! Ni hayo nimeyanyaka jioni hii na nikaona niwajuze! Asanteni na jioni njema!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom