Wezi wa laptop kwenye magari hapa dar je wana senser? Ni fedheha kwa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa laptop kwenye magari hapa dar je wana senser? Ni fedheha kwa taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kizamani, Oct 5, 2012.

 1. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa wakazi wa Dar mtakubaliana nami kwamba kwa sasa kuna wimbi la wizi wa laptop, kwenye magari madogo hasa kwa wale wanaotoka makazini na kulazimika kupita ama kwenye mikutano ya harusi au inayofanana na hiyo. Huna haja ya kupaki muda mrefu hata dakika mbili ukigeuka umeliwa. Najiuliza swali moja " je hawa wezi wanatumia nini kujua kama gari hii ndio yenye laptop na sio nyingine. Tulikuwa tumepaki magari kama kumi hivi kwenye kikao ila cha kushangaza gari iliyovunjwa ndo pekee iliyokuwa na laptop na ilikuwa kati ya magari mengine.

  Hii inanifanya nijiulize yafuatayo:
  1) Hawa wezi wanagunduaje kati ya magari mengi, hili ndo lenye laptop.
  2)Mbona hatuoni kama kuna juhudi zozote za jeshi la polisi kushughulikia matukio haya. Kila kukicha utasikia mtu analalamika (kwa jioni ya jana nimepata taarifa ya watu wawili waliovunjiwa na kuibiwa laptop. mmmoja tulikuwa naye kwenye kikao na mwingine ni coleague wangu kazini aliyepaka kwenye ATM, kuchukua hela na kurudi kakutana nao wanakimbia)
  3)Je hali hii itaendela hii mpaka lini?
  Nimesikia mpaka maboss wetu ambao ni wazungu wawekezaji wakilalamika, hatuoni linaipaka nchi yetu matope?

  Nchimbi uko wapi na vijana wako? Naamini polisi wanawajua kwani nilishaongea na polisi mmoja akaniambia kuna gari mbili Noah na GX 100 za magomeni ni noma.
  , na ndo hizo jana tumeziona na kugeuka tu laptop haipo.

  Nawakilisha.
   
 2. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,824
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Watu hawa wanashirikiana na polisi, ndio maana ukiibiwa kuna polisi atakuambia kabisa nipe pesa nikusaidie, hilo ni moja so usitegemee msaada wa Polisi lile nalo ni genge lingne hatari kabisa..kingne kinachosababisha hili jambo likue ni tabia za kishenzi za wakazi wa Dar,,,wana ubinafsi uliopitiliza wanaweza kuona mtu anaibiwa mchana hata usiku kila mtu hajali ndio maana mm nikiona kibaka hata kama haniibii mimi nahakikisha nampa kilema cha maisha ili aondoke kundini...
   
 3. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu, hata mimi nahisi kuna watu wenye maslahi hapo. Hawa jamaa wanatengeneza hela sana. Ameiba Dell original 2 kila moja 4m. Du, Tanzania ama kweli.
   
 4. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Moja ya mbinu wanayotumia wezi ni kuwafuatilia wahanga wao, mfano kwenye parking za mjini, jamaa wanaweza kupaki gari yao karibu na muda wafanyakazi wanatoka kazini. Wakisha m-spot mtu wanayetaka kumuibia kutokana na kumona na laptop au bag lake, basi wanaanza kumfuatilia, na popote atakaposimama, wako tayari na vifaa vya kufungua gari, na kutokana na expertize yao inachukua muda mfupi kutekeleza uhalifu wao
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu katika suala la usalama wako na mali zako, futa kabisa msaada wa polisi.Polisi wamekuwa tishio kwa usalama wetu na mali zetu.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  ndugu sahau msaada wa polisi kabisaaaaaaaaaa
   
 7. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sababu ni kwamba hapo da slam mnazaana ovyo ovyo ati kila mtoto anakuja na riziki yake!!!!! sasa riziki zenyewe ndo hizo uwizi. mimi nilishaacha kuja huko kama sina shughuli ya lazima kwanza mji mchafu, joto, vumbi, harufu, watu wasio na shughuli wamerundikana mitaani,wanavaa yebo yebo, kila mtu mwizi, wajuaji wa ujinga na upumbavu, maneno miiingi maarifa zero, wenyewe utawasikia "Da bana ndo kuna kila kitu"
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kikubwa hapa ni jamii, imekuwa kawaida kama mdau moja alivochangia hapo juu watu wanaona kibaka anamwibia mtu lkn kwakuwa c yeye basi hata habari hana. Tukishirikiana tutatokomeza hili bila kuwategemea Polisi hawa wa Chagonja
   
 9. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  ingia hapo-http://www.locatemylaptop.com/
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukikamata kibaka we chinja tuu itafika mahali wataacha!!:smash:
   
 11. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mkuu kabla haujapaki gari yako mahala popote, hakikisha unazichunguza kwa umakini gari zilizoko jirani. ukiona jamaa wamepaki tu kihasara kuwa makini
   
 12. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  acha kudanganya watu, kwa tz hiyo teknolojia bado sana
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Inaonekana wazi kabisa jibu unalo, kwama gari yako yenye laptop ndilo lililovunjwa na kuibwa, basi mwizi aliyachunguza magari yote na kujihakikishia gari yako ndiyo yenye laptop. Jitahidini sana kuweka vifaa vya dhamani sehemu ambayo si rahisi kujulikana. Kama ni gari dogo basi buti ya nyume inapendekezwa zaidi. Kama haina buti nyuma na huna njia nyingine teremka na bagi lako la laptop na utakaporudi rudi nayo.

  Mchimbi hahusiki na kusaka wenye mitaani wezi tunatakiwa kushiriki ulinzi shirikishi.
   
 14. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  HII technology ni worldwide,hata ukiwa kijijini kwako,its based in the united states,ukishajiandikisha which is free,once mwizi wako ana peruse internet-wewe ukiwa on any internet compatible device unapewa co-ordinates za laptop ilipo- i would advice you,next time think outside the BOX!!!!!!
   
Loading...