Wezi wa kuku wanafungwa wezi wa mabillioni hawafungwi, why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa kuku wanafungwa wezi wa mabillioni hawafungwi, why?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 19, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi ametoa mwito kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini kuchukia rushwa kama njia ya kupunguza tatizo hilo nchini.

  Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wazo Hill, Mengi alisema wanafunzi wanatakiwa kufahamu kuwa aliyetoa na kupokea rushwa wote wana hatia na wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Alisema wanafunzi hao wakichukia rushwa, wawaambie wazazi wao pia kuwa inatosha kuwa na Taifa ambalo baadhi ya watu ndio wanafaidi raslimali za umma na kuwaacha wengine wakiwa masikini.

  “Waambieni wazazi wenu kuwa imetosha, lakini cha muhimu kwanza wewe mwenyewe chukia rushwa.

  “Kuna Watanzania wengi tu ambao wanafungwa kwa kuiba kuku, ila wanaoiba mamilioni ya fedha hawafungwi,” alisema Mengi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule hiyo, Valence Misaki alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa maabara.

  Lakini alimshukuru Mengi ambaye aliahidi kuisaidia shule hiyo kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo.
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu ingekuwa vizuri ungetaja hao wezi wa mabilioni
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tumemsikia.. kaka mengi
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ushahidi wa mwizi wa kuku ni yule kuku aliyemkwiba. Ushahidi wa wizi wa mamilioni ni vigumu sana kuukusanya.
   
 5. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Money talks mkuu. Wanauwezo wa kuugeuza uongo kuwa ukweli.
   
 6. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  jamani ninani aliyerudisha hizo 40b mpaka mengi alitaka kutoa chozi....
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Usiseme kwa sauti utakamatwa, hao wezi wa mabilioni ndiyo mabosi wa rais wako.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ipo siku watazirudisha.
   
 9. b

  blacktanzanite Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  40BILION KARUDISHA BILA LIBA,HATA WEWE UNGETAJIRIKA.16b madawati,walim,majengo na stationary za kumwaga.achana na mzigo wenyewe..walai mi naweza kudiliki kusema kuwa INATOSHA ukizingatia wenzenu hatuna chama wala itikadi,hatufungamani na yeyote katika kutengeneza maslai yao.ni kweli kila mtu anataka kuwa juu.. si kiivyo NOMA.LAKINI SI NDIYO HAYO MAPALECE(BANGALOOO)TUNAYOYAONA????///!!!!
   
Loading...