Wezi wa EPA wafungwa miaka mitatu, sie wa kuku tunafungwa maisha

Hawa watakuwa wamesomeshwa kama ishu ya Balali kuwa wakitoka hapo waongezewa senti tena kuishi kama wako peponi.
 
Ndo serikali ya CCM hiyo iliyoamua wezi wa hela zetu (Malanda) na wenzake kufungwa miaka 3 sie wezi wa kuku maisha sijui usawa uko wapi, eti ushahidi haukuwatia hatiani kweli?
 
Ndo serikali ya CCM hiyo iliyoamua wezi wa hela zetu (Malanda) na wenzake kufungwa miaka 3 sie wezi wa kuku maisha sijui usawa uko wapi, eti ushahidi haukuwatia hatiani kweli?

Wakikaa gerezani miezi 3 wanatolewa kwa msamaha wa Rais!!!!! Hii ndio TZ bwana!!!!!!!


Tiba
 
tusubiri mwezi december, uhuru ceremony, hawa jamaa wanatoka, na pesa haijarudishwa na haitarudishwa....
 
Nonsense,hakuna mwizi wa kuku aliyewah kufungwa maisha.Labda kama wabakaji/wauwaji kwako ni wezi wa kuku
 
Sasa hapo tumepewa mfano gani... Basi bora na mie nianze kufikiria kufanya uwizi wa million 500 kama ni miaka 3 tu hamna noma niko tayari kunyea debe najua kila mwaka kuna msamaha wa rais nitatoka niendelee kutesa mtaani na hela za uwizi... Its ridiculous...
 
Eti kifungo cha miaka mitatu kwa wizi wa mabilioni ya hela huku mwizi wa kuku akijinyakulia miaka 30, swali langu hapa hizi hukumu mbona siyo adhabu kwa wahukumiwa? Maana hata kama ni mimi nipewe haya mabilioni ya hela alafu nifungwe miaka mi3 ni shwar tu kwani nikitoka naendelea kuneemeka
 
Huu ndio utoto mwingine ambao tumeendelea kuhushuhudia na nina sikia walisha anza kutumikia kifungo kwa hiyo siku si nyingi watatoka!
 
Kesi imefungwa Mnaweza sasa kuizungumzia Ruksa!!!
Mbona Yule Alex Masaw3 aliiba kisha akafungwa alipomaliza kifungo akaanza kutumia pesa zake alizoiba
 
Ni Hakimu Mkazi Kisutu (Fatuma Masengi) ndiye aliyewahukumu kwenda jela miaka mitatu. Na ni mtu na binamu yake, Rajab Maranda na Farijala Hussein. Katika moja ya hatua ya kesi hiyo, watuhumiwa hao pia walifutiwa shitaka moja kati ya mashitaka saba waliyotuhumiwa nayo. Shitaka lililofutwa ni la wizi wa zaidi ya shs. 600mil. za benki kuu, ni kwamba ushahidi hakuna.

Makidai yote yale anakwenda kunyea debe? Duuh, sheria msumeno. Na inaelekea kweli hakuwa miongoni mwao
 
Danganyd toto, watatoka kwa msamaha wa rais. Pesa ilishatumiwa na magamba, ukizingatia maranda ni mweka hazina wa magamba Kigoma.
 
washawatengenezea vyumba vya executive ukonga eeeh! wanakaa hapo miezi kadhaa then msamaha wa "rahisi"
 
Wanabodi Heshima Kwenu,Hii habari ya kada wa CCM kushiriki kwenye wizi EPA na pesa hizo kutumika katika kufanikisha uchaguzi na bado chama chake mpaka leo hakijawahi kutoa kauli yoyote ya kumkana au kumvua uanachama kinaleta maswali mengi yasiyo majibu: Soma hiyo habari:

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka 18 jela Kada wa CCM, Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein katika kesi ya tuhuma za kuchota Sh2.2 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mahakimu wawili katika jopo la waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo waliwatia hatiani watuhumiwa kwa makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa.

Source: Mwananchi

Mytake: CCM Mnajitanusua vipi kwenye wizi?Wananchi wangependa kupata ufafanuzi wa mambo kama haya siyo propaganda mnazoendesha kina Nape na Mwigulu
 
Back
Top Bottom