Wezi wa EPA wafungwa miaka mitatu, sie wa kuku tunafungwa maisha

Ulipoambiwa kafungwa, vocha ikakata? Makusudi hadi kwenye siasa, duh! Haya tunasubiri baba.
 
Ni Hakimu Mkazi Kisutu (Fatuma Masengi) ndiye aliyewahukumu kwenda jela miaka mitatu. Na ni mtu na binamu yake, Rajab Maranda na Farijala Hussein. Katika moja ya hatua ya kesi hiyo, watuhumiwa hao pia walifutiwa shitaka moja kati ya mashitaka saba waliyotuhumiwa nayo. Shitaka lililofutwa ni la wizi wa zaidi ya shs. 600mil. za benki kuu, ni kwamba ushahidi hakuna.
 
Kafungwa miaka mingapi? manake kesi za ufisadi hua hazizidi miaka miwili
 
hii EPA wanafungwa watu waliochukua fedha ndogo tu.. wale waheshimiwa wenyewe kabisa wapo mtaani tuu hawana hata wasiwasi..
 
Duh, maiaka mitatu! Ngoja na mimi niwe fisadi! Miaka mitatu na mabilioni waliokwiba si issue!
 
waliofungwa ni kambale na dagaa....ma papa bado wako baharini wanaogelea na kuendelea kula bata tu
 
Ni Hakimu Mkazi Kisutu (Fatuma Masengi) ndiye aliyewahukumu kwenda jela miaka mitatu. Na ni mtu na binamu yake, Rajab Maranda na Farijala Hussein. Katika moja ya hatua ya kesi hiyo, watuhumiwa hao pia walifutiwa shitaka moja kati ya mashitaka saba waliyotuhumiwa nayo. Shitaka lililofutwa ni la wizi wa zaidi ya shs. 600mil. za benki kuu, ni kwamba ushahidi hakuna.
Haya majina hata siyakumbuki,unajuwa ile ssue imo humu inside out.Hawa watu role yao ilikuwa ipi kwenye EPA?
Halafu hizi adhabu mhn!Kama hivyo nani ataogopa kufisadi?Tena ukizingatia kama una pesa jela bongo unaishi kwa raha tu,godoro,ml safi unaletewa na ndugu,unachillout tu,cellphone, unahamishiwa gereza "zuri" kazi ngumu et etc.
 
Back
Top Bottom