Wezi wa epa,kagoda,deep green,na rada watajisalimisha kwenye kanisa gani na lini/ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa epa,kagoda,deep green,na rada watajisalimisha kwenye kanisa gani na lini/

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Seif al Islam, Jul 14, 2012.

 1. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Nimepokea kwa mshangao mkubwa taarifa kuwa eti mmoja kati ya watuhumiwa waliomteka na kumtesa dr ulimboka amejisalimisha na kuungama dhambi ya kumtesa dr ulimboka katika moja ya makanisa ya kiroho hapa jijini dar.nashindwa kuelewa imekuwaje huyu kijana anayedaiwa ni mkenya na ambaye hata picha yake haijawekwa hadharani alipofikishwa kisutu mahakamni imekuwaje akajisalimisha wakati wezi wa epa,kagoda,deep green, meremeta,rada na hata hawa walioiba fedha za safari za rais hapo wizara ya mambo ya nje hawajajisalimisha na kuomba msamaha wa mungu hadei leo?yani ina maana huo upako umemgusa huyo kijana huyo mgeni ambaye anadaiwa kutenda hilo kosa juzijuzi tuu hapa na ukashindwa kuwagusa wezi wengine amabo ni watanzania wenzetu na wengine wamewahi kuingia si mara moja katika makanisa haya na kusimama katika madhabahu na kutoa maneno ya vijembe dhidi ya wenzao? Kwa masikitiko sana nashindwa kutofautisha utendaji wa makanisa haya na waganga wanaoroga watu na kupiga ramli.kama kweli kuja upako naomba niambiwe hao wahalifu wengine tena ambao ni watanzania wa hapa hapa watasjisalimisha lini na katika kanisa gani?
   
Loading...