Wezi wa BoT wazuiwa kusafiri nje

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Kuazia sasa, wale wezi wa fedha zetu pale Benki Kuu ya Tanzania wamezuiwa kusafiri na karibu wote hadi mchana walikuwa wamesalimisha pasipoti zao kwa jamaa wa usalama wa taifa.

Ninasema wote, ingawa wapo wawili watatu hivi wanaonekana kukwepa kwamba wao hawahusiki, ingawa wanatajwa tajwa sana. Yasemekana wamehojiwa, lakini wanashindwa kubanwa moja kwa moja na wizi huo wa kutisha wa fedha kwa barabara zetu, dawa zetu, elimu yetu na kila kitu chetu.

Miongoni mwa watu hao ambao wazungu wanasema bado wako at larger ni Jeetu Patel na yule muiran anayejifanya sana kuwa mwanaCCM wa damu na swahiba wa Kikwete.. si yule jamaa wa kule Unyamwezini. Yaani hamumjui had nimtaje...haaaaa huyo huyo. naye bado jamaa wa usalama nasikia na wanamuogopa kwa kuwa ni right hand man wa mkuu wa kaya.

Lakini kwa sasa acha wakome. Nasikia wengine wanatamba, hasa Maregezi kuwa hana wasiwasi atarejesha hizo blini 16 alizokwiba. Anasema alichofanya aliziweka benki kwenye fixed account sasa akawa anakula riba, sasa wakizitaka anazo. Anasema amesharejesha 10,000,000,000.
 
Habari hizi kama ni za kweli inabidi JK apewe pongezi kwani tunaona shughuli zake. Ahsante JK.
 
Sasa wakirudisha hizi pesa tuone kama kuna wengine wataingiza ktk hilo kapu maana hizo zimerudi pasipo kutegemea. Mimi nadhani ziende ktk project maalumu hasa ktk kuhudumia watoto yatima, wamama wajawazito, n.k maana zinzweza kuliwa tu tena na wahuni mafisadi.
 
..ina maana ukirudisha ndio inakuwa imetoka kesi hakuna au?

Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.
 
Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.

Ndugu Dar naona unakufa sana na JK lakini siku mambo ta Richmond na Bot wataamua yafike Mahakamani na ukakujua JK ana mkono gani pale nadhani hutakuja hapa kutaja tummwagie sifa huyu JK.Unaambiwa Muiran hata Usalama wanamuogopa kwa kuwa ni right hand man wa JK .Bungeni kaonyesha dharau na bado ana dunda leo unasema JK asifiwe ?
 
kuna siri kubwa sana katika epa accts, nitatoa snap na wengine walete picha nzima

epa funds were stolen in massive amounts beginning oct 2001 to oct 2004 appro 600 million usd.

uchunguzi uliofanywa ulicover only few months za 2005.

so majambazi wakisema watalipa hizo hela wanazosemwa kuiba ni true kabisa sababu ni small portion ya total funds walizoiba from 2001.

swali kubwa kwa jk ni je kwa nini hamtaki kuchunguza epa from at least 2000-2005//// hapo ni kazi ipo
 
Ndugu Dar naona unakufa sana na JK lakini siku mambo ta Richmond na Bot wataamua yafike Mahakamani na ukakujua JK ana mkono gani pale nadhani hutakuja hapa kutaja tummwagie sifa huyu JK.Unaambiwa Muiran hata Usalama wanamuogopa kwa kuwa ni right hand man wa JK .Bungeni kaonyesha dharau na bado ana dunda leo unasema JK asifiwe ?

Tungoje hiyo siku ifike na ninakuhakikishia mimi ndio ntakuwa wa kwanza kumlaani. Kuhusu ya Muiran nadhani six alitangaza bungeni habari zake siku ya mwisho ya bunge lililopita tungoje tuone kinachoendelea. JK nina uhakika hatokuwa na urafiki katika kutetea maslahi ya wengi, tumeona kwa Lowassa.
 
Habari hizi kama ni za kweli inabidi JK apewe pongezi kwani tunaona shughuli zake. Ahsante JK.

Hivi wandugu kwa nini tunapenda kutoa pongezi kwa haraka haraka hivi...yaani mtu kunyanganywa pasi ya kusafiria ndio nini..hawa watu wamechukua takriban Dola Milioni 200 (moelex23 anasema 600 Million $) kwa hela hiyo kuna haja gani ya kungangania pasipoti ya Tanzania.
 
Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.

Oh! No be serious, kuna tofauti kati ya Mikopo na Wizi. Mafisadi hawa waliiba. Mwizi wa kuku hufungwa miaka kadhaa jela hata kama amemrudisha kuku aliyemkwiba, hawa mafisadi adhabu yao inatakiwa iwe mara 100 ya mwizi wa kuku. Yaani kama mwizi wa kuku anafungwa miaka 2 basi mafisadi wahukumiwe kifungo cha maisha kwa jinsi ambavyo ufisadi wao umegharimu maisha ya watanzania wengi(Kufa kwa magonjwa yanayotibika), ajali nyingi kwa ubovu wa barabara na watanzania kuendelea kupata elimu duni.
 
kuwazuia kutoka nje peke yake haitoshi,warudishe fedha halafu waende kwa pilato. Kama muungwana JK unapitia hapa jf, hiki ni kilio cha Watanzania wote sio sisi tu tunaotoa kilio hiki hapa jf,tunakuomba muungwana JK wajibika kwa nafasi ulipewa na umma.
 
Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.

Hawa watu hata kama watarudisha bado wana kesi kama sita za kujibu.

1. Wizi wa kuaminiwa
2. Forgery (walitoa viambatanisho hewa)
3. Walihujumu uchumi na kuisababishia serikali na watu wake hasara ya mabilion ya pesa Ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa shilling ya Tanzania kwa 30%

4. Kukwepa kulipa kodi maana hakuna hata company moja iliyolipa fedha kutokana na malipo ya fedha walizopata
5. n.k
 
Ndg Dar,

Ninavyoelewa pesa za accounts za EPA si za mikopo bali ni uwizi na udanganyifu.
 
Hivi wandugu kwa nini tunapenda kutoa pongezi kwa haraka haraka hivi...yaani mtu kunyanganywa pasi ya kusafiria ndio nini..hawa watu wamechukua takriban Dola Milioni 200 (moelex23 anasema 600 Million $) kwa hela hiyo kuna haja gani ya kungangania pasipoti ya Tanzania.

Kama vile tupondavyo maovu kwa haraka haraka na ndivyo tutoavyo pongezi kwa kila jema kwa haraka haraka, jee kuna tatizo hapo?
 
..ina maana riba hawajaitia kwenye hesabu za marejesho au?

Yaani kama hakuna riba kweli ni wajinga waliwao. Sio marejesho tu bali na kodi pia bila kusahau kuzimama kizimbani na kuwa declared kuwa ni watu hatari kwa jamii.
 
Hawa watu hata kama watarudisha bado wana kesi kama sita za kujibu.

1. Wizi wa kuaminiwa
2. Forgery (walitoa viambatanisho hewa)
3. Walihujumu uchumi na kuisababishia serikali na watu wake hasara ya mabilion ya pesa Ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa shilling ya Tanzania kwa 30%

4. Kukwepa kulipa kodi maana hakuna hata company moja iliyolipa fedha kutokana na malipo ya fedha walizopata
5. n.k

Akishalipa inakuwaje? ndio swali lililopo. Kuiba na kukopa ni vitu tofauti na mahakama zipo. Nani uliemsikia akaiba halafu akarudisha?
Tuwache unazi kama kuna wizi umefanyika kwenye hizo account basi huu wizi ni wandani ukishirikisha watu wa nje, hawezi kukurupuka tu mtu wa nje kwenda kuchota benki? wenye bank walikuwa wapi? wamelala?
 
kwanza, fedha iliyoibiwa iwekewe na riba.
pili, irudishwe yote pamoja na riba yake
tatu, wafikishwe mahakamani.
nne, sio wa epa tu bali wa richmond na wabadhirifu wamali ya umma wote
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom