Wezi kupitia mizani wakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi kupitia mizani wakamatwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KiuyaJibu, Sep 22, 2009.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Wakala wa vipimo mkoani Morogoro baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa mji wa Ifakara, Kilombero kuhusiana na wizi unaofanywa na wafanyabiashara wa eneo hilo hasa katika bidhaa zinazofungwa katika mifuko kuwa mara nyingi wamekuwa wakipata ujazo pungufu ukilinganishwa na ulivyoandikwa katika mfuko husika. Meneja wakala wa vipimo mkoa Luppy Shirima aliyafanyia kazi malalamiko hayo Septemba 08,2009 na akatoa taarifa kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya kilombero na polisi hivyo kuamua kufanya operesheni ya kushtukiza.

  Ambapo iligundulika wafanyabiashara wamekuwa wakidanganya kwa kuuza mfuko mmoja wa sembe wa 25kg kwa maandishi wakati mteja anaambulia 19kg au 20kg; wafanyabiashara 21 walikamatwa kwa kosa hilo na walikiri kutenda kosa na kulipa faini ya kati ya Tshs 62,500/=hadi 100,000/=. Hivyo basi, mamlaka husika ilipata Tshs 2,000,000/= kutoka na malipo ya faini.

  Walichokua wakifanya wafanyabiashara hao ni kufungua na kufunga upya;Shirima alisema,pamoja na kulipa faini husika wafanyabiashara hao wapewa mwezi mmoja kuhakikisha kuwa maduka yao yameweka mizani ili kila mnunuzi (mteja) atakayenunua bidhaa lazima ahakiki uzito halali uliopo.

  Kama huko mambo yenyewe ndiyo kama hivyo,sipati picha kwenye miji/majiji mengine ambapo watu wako busy hawa jamaa siwanapiga mchanga wa macho (mazingaombwe) kwa kwenda mbele!!?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Asante kwa alert!
  Watu wengi sana huibiwa bila kujua, hasa kwa hizi bidhaa za njiani wakiwa safarini.
  Nilikumbana na kisa katika eneo liitwalo MtowaMbu huko Manyara nikiwa natokea Karatu. Nilikuwa nataka kununua mchele wa fasta wa kupeleka kwa watoto, lakini wauzaji wengi (ambao ni wadada), wametoboatoboa pua na wamevaa vipini viingi mno usoni kote. Kuna mzee mmoja akanambia niachane kabisa na wauzaji wa hivyo, ni matapeli wa hatari.Akatuonyesha sehemu salama ya kununua.

  HABARI NDO HIYO.
   
Loading...