Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ya miaka 55, Mungu amenijalia kupita kwenye usafiri wa hewani na fastJet kutoka DSM kwenda Mwanza kwa bei ya sawa na usafiri wa Mombasa raha kati ya Dar na Mwanza. Aliyeleta idea hii ili na sisi wenzangu mimi tunuse hewa tamu ya karibu na mbinguni apongezwe sana.
Mimi ningekuwa Meneja wa Precsion Air ningemshauri ajipange upya na aje na mkakati mbadala wa biashara ya usafirinwa ndege ambayo tayari ni tishio kwenye kampuni yake. kama hawa Fastjet wataendelea, basi NAOMBA usikubali Precision ife kwa sababu ya kukosa soko,. Anza kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kuanzia sasa, punguza wafanyakazi wako ambao wengi ni ndugu zenu, kata intertainment allowances, na ukiweza punguza hata mishahara ya wafanyakazi ukianzia ule wa kwako mwenyewe, halafu ongeza idadi ya flights kule ambapo hawa jamaa hawaendi na mwisho punguza nauli ili uanze kushindana na siyo kutanua.
Naipenda Precsion kwani nilikuwa naiona hewani kila siku lakini nadhani naipenda sana fastjet kwani nimeweza kwenda nayo hewani leo.