Wewe unaye soma hadithi hii badilika sasa na badili tibia yako. Msaidie rafiki au ndugu yako wakati wa matatizo yake

FROWIN

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
216
225
HABARI!
nyumba niliyo kuwa nikishi ilifikia kipindi nilitaka kufukuzwa Ndani kwa kutokulipa kodi. Nikaamua kuwashirikisha marafiki hata na boss wangu pia, wote wakaanza kunikwepa, hali nlivyoona hali hii nikaamua kushea na marafiki zangu Tatizo langu kwakupost Facebook kutafuta msaada, lakini nilicho kipata ni likes 2 "na comment "0."

Nikaamua kutuma msg 250 kwa watu wangu wa karibu niliowasave kwenye simu,kuomba mkopo wa Tsh 600,000 tu. Wakajibu watu 10 tu. 6 kati ya hao 10 walisema hawataweza kunisaidia. 1 aliamuakunisaidia kiasi kidogo sana na wengine 3 wakaniahidi ila baadaye wakawa hawapokei hata simu zangu, mwisho nikafukuzwa kwenye nyumba.

Sikuwa na pakulala. Nikiwa nimechanganyikiwa natembea gizani mitaa ya manzese, bahati mbaya kibaka akanipora kibegi changu kidogo kilicho kuwa na vitambulisho vyangu. Ila alipokimbia upande wa barabarani gari likamgonga na kufariki hapohapo. Wakaokota kibegi changu na kukuta vitambulisho, hivyo wakatangaza kwamba nimefariki.

Watu 300 wakaandika kwenye akaunti yangu ya Facebook njisi walivyo nifahamu na jinsi nilikua mtu mzuri sana na mstaarabu, kamati ya mazishi ikaundwa na rafiki zangu wakachanga Tsh 1,500,000 zakuweza kulisha watu kwenye msiba. Wafanyakazi wenzangu wakachanga laki 6 ya Jeneza viti na maturubai. Walipanga nizikwe kwenye Jeneza la Heshima la Tsh 300,000 walipoenda kununua muuza Jeneza akawauzia kwa Tsh 280,000 kapunguza Bei kwamba ndo mchango wake.

Familia wakakaa kikao wakachanga Tsh 3,000,000 kila mmoja alitaka kujionyesha kuwa yeye ni mchangiaji mzuri. Waka print t-shirts kwa Tsh 200,000

Fikiria sasa picha iliyotokea nilipoamua kujitokeza siku ya mazishi yangu.....

FUNZO:

*Ndo hivyo DUNIA ilivyo kwa sasa, ni ukweli wa kusikitisha lakini ni moja ya maisha tunayo ishi sasa hivi katika Jamii zetu kila siku. Wewe unaye soma hadithi hii badilika sasa na badili tibia yako. Msaidie rafiki au ndugu yako wakati wa matatizo yake. Usisubirie kifo chake ndo ukaonyeshe ufahari au mapenzi yako kwake. Hivyo haviwezi kumsaidia chochote. Tupendane hakuna anaependa matatizo ila Vyote ni vya Kupita tu hapa chini ya jua!*

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
866
1,000
Ktk Maisha Kuna kitu kinaitwa akiba ndg yangu,weka akiba kwa maisha yako ya baadae.utaziepuka fedheha.
 

sheremaya

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
2,861
2,000
Huwezi kupingana na sheria ya asili ya dunia
Pambana kutafuta vya kwako watu wanafurahi kukuzika ili usiwamalizie hewa
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,791
2,000
Dah ila maisha haya jamani. Sijui ni nature ina operate hivyo au ni kitu gani.


Ila ni kawaida mkuu, hapo ungekuwa uligongwa kweli na umevunjika miguu upo pale MOI ungewaona ndugu wachache sana wakija kukunywesha uji.

Hata hiyo michango isingekuwepo yakukusaidia. Inaumiza sana ukiwaza haya mambo ila ndio hivyo yani. Ndio uhalisia huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom