Wewe unatabia ya mnyama gani kati ya hawa?

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
461
392
Wafuatao ni baadhi tu ya Wanyama na tabia zao, ambazo Mimi, wewe tunazo na wakti mwingine ni vikwazo kwa watu wanaotuzunguka.

1. PUNDA: anaposema "Siendi" haendi hata umpige na gogo la mbuyu. kuna watu ambao waking'ang'ania wazo moja hata aambiwe ukweli aje, habadilishi wazo lake.
PUNDA

2: SIMBA: Huyu ni mgomvi" watu wenye tabia za simba wapo tayari kupigana kwa vyovyote vile na yeyote yule anayeingilia mipango ama matakwa yao.
SIMBA
3: SUNGURA: yeye ni kutimua Mbio tu. Watu wenye tabia ya Sungura siku zote hawatatui tatizo, wakiona ugomvi ama vuguvugu la ugomvi linataka kutokea haraka sana wanabadilisha maada. Hawa ni waoga
SUNGURA




4: NYANI: Anapumbaza na Mcheshi, Mara nyingi watu wenye tabia za nyani huwa wanapenda kuwa wachekeshaji sana na wanapumbaza wenzao pale wanapokua wanafanya mambo muhimu.


NYANI
5: NYOKA: Huyu huwa anapenda kujificha kwenye nyasi na huruka ghafla na kung'ata. Wapo watu wenye tabia kama za nyoka, Mara nyingi huwa wanakaa kimya kwa muda mrefu wakati jamii fulani ikiwa inashiriki kufanya jambo, lakini endapo wakisema jambo moja tu huaribu kila kitu kinachoendelea.


NYOKA


6: KOBE: Huyu upenda kujiingiza ndani ya nyumba yake endapo mazingira hayapo shwari, na hujitoa anapohisi hali imekua shwari nje. Wapo watu watabia kama za kobe, hupenda kujitoa kwenye jamii ama kundi endapo kuna matatizo, hawatoi mchango wowote ule, kama wa mawazo, pengine wangependa jamii isifahamu kama wapo ndani ya hiyo jamii ili wasisumbuliwe kabisa.


KOBE
7: TEMBO: Anatabia ya kuangusha miti barabarani, na kuzui njia ili chochote kisipite hadi atakapo amua yeye. Wapo Ndugu zetu wenye hizi tabia, wanakua wasumbumbufu, wababe huzuia kundi kuendelea na shuguli zake kufikia malengo yaliyopangwa.




TEMBO
8: MBUNI: Huona kila kitu kipo sawa wakati wote, hawafikiri kama kuna tatizo kamwe. Wapo watu wenye tabia kama za Mbuni, mara nyingi huinamisha kichwa chake kwenye mchanga, hukataa kabisa kukubali kama kuna matatizo.
MBUNI


 
Mallata Jr

tatizo lako uko kibiashara zaidi, jf ni sehemu watu wanajifunza mambo mbalimbali, kwa nini usiweke kila kitu hapa na ss tukajuwa vitu hadim kama hiv
 
Last edited by a moderator:
tatizo lako uko kibiashara zaidi, jf ni sehemu watu wanajifunza mambo mbalimbali, kwa nini usiweke kila kitu hapa na ss tukajuwa vitu hadim kama hiv

Xorry mkuu siunajua tuna mablog yetu tena sema nimerekebisha mkuu unaweza endelea kuchangia ni ipi tabia ulio nayo?
 
ah! churaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

ahaa sungura
2127082186_aec0e3dfc7.jpg
 
Kukudume hayupo ndio tabia yangu kuchapa mkia tu

Jogoo ni muongomuongo mara kamdanganya huyu ntakuoa mara huyu ntakujengea nyumba mara hao watoto hawana baba mimi ntawalea kumbe hana lolote anataka ile kitu ile si ushaijua mkuu.
 
TIGER.......... NI KAMA SIMBA TU SEMA YEYE MPOLE ZAIDI LAKIN AKIKASIRIKA HATARI ZAIDI NA ANA WINDA SUNGURA( miss chagga UMENIELEWA) KIVYAKE VYAKE HATEGEMEI COMPANY YA WENZAKE AKIAMUA KAAMUA
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom