Wewe unasema masikini na hawa wanao lala ovyo watakuwa hali gani? Fikiria sana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
375122_135578429969745_1183750356_n.jpg
 
Umasikini unatofautiana, sawasawa na ugonjwa, unaweza ukajiona unaumwa mpaka unatamani kufa...... Ukienda hospital unaweza kuta kuna mgonjwa zaidi yako tena mahututi kupita kiasi hapo waweza kiri we simgonjwa!
Na umasikini ni hivyohivyo waweza sema we ni masikini ukakutana na masikini chokest ile mbaya...... Mbona waweza jiita young billionaire bila kupenda?
 
umasikini unaanzia kwenye akili,mfano viongozi wa ccm wanajitahidi sana kuondokana na umasikini kibinafsi lakini kila wanapoingia mikataba feki na kujipatia hela wanajikuta bado ni masikini wanapeleka mabilioni uswis bado wanajiona masikini.ukitaka kuondokana na umaikini unatakiwa uanzie kwenye akili;na mfano wako uwe george washingto na nyerere au uruguay.
 
umasikin si kilema

Umasikini ni kilema. Tena kilema kikubwa sana zaidi ya kilema unachofikiria wewe.
Angalia ni walemavu wangapi wenye pesa wanaoishi katika hali bora ya maisha. Hawafikirii chochote juu ya ulemavu wao. Ukiwaona majukwaani wanaongelea ulemavu wa viungo ni kujiona tu wana kasoro katika miili yao. Haiwaathiri chochote katika maisha.
Masikini hana muda wa kuabudu,kukaa na familia yake, kujichanganya katika starehe na hata kupanga utaratibu wa kula.
 
mkuu umetetea hoja yako KI RAHISI sana,huwezi kamwe ukapigana na ukweli kwamba UMASIKINI SI KILEMA.
 
Back
Top Bottom