Wewe Unakumbuka nini.....?

Nokla

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
3,164
1,696
Mimi nakumbuka haya wewe je?
1.Kung'olewa jino kwa uzi
2.Kicheza huku umeshikilia kaptula kisa kifungo kimetoka
3.Kunyolewa msalaba shulen kisa nywele ndefu
4.Kukata ndala eti kifutio
5.Kuoga nje
6.Kuchonga penseli kwa meno
7.Kidonda kuweka unga wa rangi mbili
8.Kunyolewa kwa mkasi
9.Ku-rewind mkanda kwa peni

..........................
Wewe je?
 
10. Kutuma barua ya kuomba fedha nyumbani wakati ukiwa boarding school
11. Kula ugali na chai wakati maharage hayaivi na yameoza balaa
12. Mwalimu kukucharaza fimbo, hata zaidi ya thelasini.
 
13.kupiga picha huku ukiwekan poz la dole gumba
14. kutumwa dukani ulete ASPRIN halafu ulete ASPIRO.
15. kutembea kilometa nzima kwenda kwenye sinema, na ukifika sinema ndio inaishia.
16. Kuficha chapati na kuingia nayo kanisani ndani ya seminary na harufu yake inasikika ila ukisachiwa haionekani.
17. Kwenda shule peku na ukitaka kwenda msalani unamwazima mwenzio ndala.
18. kuvaa kaptula yenye lastiki mfano wa rubberband moja tu kiunoni na imetoboka mbaya na ndani hujavaa chu***p!
19. Kula maharage yote jikoni na kujaza maji mengi kisa kuonja!
20. Kucharazwa viboko uwanjani wakati wa UMITASHUMTA kisa unasimama nyuma ya goli kuzuia magoli.
 
Kucheza gorori wakati wa mapumziko shuleni vutanikuvute na wagambo mt kongo kupiga chabo vyoo vya madem fole i ya mihogo wakati wa mumziko atc.....
 
13.kupiga picha huku ukiwekan poz la dole gumba
14. kutumwa dukani ulete ASPRIN halafu ulete ASPIRO.
15. kutembea kilometa nzima kwenda kwenye sinema, na ukifika sinema ndio inaishia.
16. Kuficha chapati na kuingia nayo kanisani ndani ya seminary na harufu yake inasikika ila ukisachiwa haionekani.
17. Kwenda shule peku na ukitaka kwenda msalani unamwazima mwenzio ndala.
18. kuvaa kaptula yenye lastiki mfano wa rubberband moja tu kiunoni na imetoboka mbaya na ndani hujavaa chu***p!
19. Kula maharage yote jikoni na kujaza maji mengi kisa kuonja!
20. Kucharazwa viboko uwanjani wakati wa UMITASHUMTA kisa unasimama nyuma ya goli kuzuia magoli.

Ha ha ha mkuu hiyo 13. Ya kupiga picha umenikumbusha mbali sana dah!
 
10.Kuvaa mikanda ya SKY WAY na kuifanya kuwa saa ya mkononi
(sky way ni kandambili za zamani)
 
Kakata kanda mbili utengeneze matairi ya gari, chupi za VIP zilivyokuwa zikikatika uzi kwa chini ukishtuka iko kifuani.
 
16. Kuficha chapati na kuingia nayo kanisani ndani ya seminary na harufu yake inasikika ila ukisachiwa haionekani.
Ha ha ha umenikumbusha mbali sana,
 
kuvaa viatu vya raba za kuchumpa za fila na nike vijana wa leo wanaita supra.
 
1. kusugua sufuria kwa mchanga,
2. kutambiana kupigana kwa kuchora msitari wa kati na kutambiana wa kuuvuka,
3. kutotaka taa izimwe wakati nataka kulala kwa hofu,
4. kuchapwa bakora na walimu (ilikuwa kama kaoperation fulani) baada ya kugundulika kuwa una mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzako
5. kuibiana penseli/kalamu mashuleni kwani sikumbuki kama kuna wanafunzi walikuwa wakimaliza wino katika kalamu zao zaidi ya kupotea
6. Kuandikiana barua za kimapenzi mashuleni
7. kuwahofu form two wakati ninyi mkiwa form one
8.Mchezo wa baba na mama ingawa mimi sikuexperience huo mchezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom