Wewe unakumbuka nini miaka miwili nyuma

Mrisho com

JF-Expert Member
May 2, 2015
3,892
3,913
Kwakweli ndani ya miaka miwili au mitatu iliyopita tulipata kushuhudia vimbwanga vya kila aina, kuna muda unakaa unavitamani kuvisikia tena lakini ndio hivyo hakuna namna.

Toka hapo ulipo nenda Dodoma utakutana na aliekuwa spika wakati huo akijinasibu ya kwamba "atake asitake lazima tumuongezee muda". Huyuhuyu alileta ushuhuda wa Yesu akiwa na mkewe walikosa pa kulala huko Israel.

Wapo walikokuja kujinasib kama wao ndio watu wanaokula raha duniani na nyie wengine kubaki watazamaji na si wasindikizaji.

Hatukuishia hapo, kuna mmoja wetu alifikia mbali kabisa na kumfananisha na Yesu ili mradi kutengeneza mapambio ya kusifu baada ya vitu vya kusifia kumuishia.

Nenda kwa mlima pilipili hoho,alifikia hatua ya kutaka kuwatandika viboko wa staafu kwa sababu tu za kuingiliq mipango ya watu.

Yote tisa,wapo waliojinasibu kwamba waliokotwa majalalni wakila uchafu wakiwa hawana mbele wala nyuma nao hawakusita kuleta ushuhuda wao.

"WEWE UNAKUMBUKA NINI, TUKUMBUSHANE TU MAANA MAISHA MAFUPI HAYA""
 
Nakumbuka kuoga kila mda kila siku kwa mda ninaotaka na sio kwa kupangiwa ama nichague nioge ama nifulie
 
Nakumbuka bei nzuri za bundle, nakumbuka bei nafuu ya chakula, nakumbuka uwajibikaji kwenye sekta ya uma, nakumbuka sana
 
Nakumbuka halotel walikuwa wanatoa free internat kila usiku kuanzia saa sita hadi 12 asubui
 
Nakumbuka mvua kubwa ilonyesha pale bandarini Daslam.Mimi niliokota vichwa vya treni na wala sikuwa na majivuno!
Enheee...!Nilitaka kusahau.Kuna rafiki yangu ni "shujaa wa vita ila mwendo aliishia majiani" aliulizwa tu,chekechea alisonea wapi?Alifura kwa ghadhabu hadi yule muulizaji "akahama" nchi.🤔🤔🤔🤔
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom